KUOMBA KUNAKOLETA MAJIBU




=MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU, Rum 8:27 / Yoh 14:16-17

¤Yesu alisema, Roho mtakatifi ni msaidizi wetu, anatusaidia na kutufundisha yote, na kutukumbusha yote yaliyo mema, kwamaana sisi bila yeye hatuwezi neno lolote, na sisi peke yetu hatuwezi kuomba ipasavyo bila ya Roho Mtakatifu, maana yeye anajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo,

Hivyo basi, kabla ya kuanza maombi, au kusoma neno, au Ibada, au Safari, au Mtihani, au Kikao, nk jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu na uombe msaada wake ili akupe Ufanisi / Ubora katika yote yakupasayo kuyafanya,

Tambua Uungu wake (Roho Mtakatifu ni Mungu halisi katika nafsi ya tatu) (Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu,
#Roho_Mtakatifu)

Jikabidhi katika nguvu na uongozi wake,

Na kutii kila uongozi anaokupatia,

HATUA_YA_PILI

=FANYA TOBA YA ONDOLEO LA DHAMBI / UTAKASO , Isa 59:1-12 / Yoh 9:31 / 1Yoh 1-10,

¤Sikio la Bwana si zito kusikia, wala mkono wake si mfupi hata ashindwe kututendea mambo tumwombayo, bali maovu yetu ndio yanayotufarakanisha na Mungu wetu,

Mungu hawasikii wenye dhambi, hivyo, chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za Mungu, na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha kweli, Mungu ni mwaminifu, atatusamehe na kututakasa na uchafu wote (Isa 1:18) lakini kabla ya kufanya toba yako binafsi, kuna mambo ya kufanya

Kwanza, WASAMEHE WOTE WALIOKUKOSEA hata kama hawajata kukuomba msamaha, maana usipowasamehe walio kukosea, na Mungu naye hataweza kukusamehe wewe (Math 6:14-15)

Pili, NDIPO UFANYE TOBA YAKO na Mungu atakusamehe, Hata kama dhambi zako ni nyekundu sana, zitasafishwa kabisa, nawe utakuwa safi (Isa 1:18 / Isa 43:25)

HATUA_YA_TATU
 
=MSIFU NA KUMSHUKURU MUNGU, Zabu 147 / Zab 148

¤Msifu Bwana kwa matendo yake makuu,
¤Mwabudu Bwana Uzuri wake, na Sifa zake,
¤Mwadhimishe Mungu kwa tabia zake, Wema wake, Fadhili zake, na Baraka zake mbali mbali anazo tutendea,

Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa tayari kukupa haja za Moyo wako,

Mahitaji yetu yamefichwa nyuma ya sifa, Ndio maana neno lake linasema ,, Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu, na kumshukuru) naye atakupa haja za moyo wako (Zab 37:4)

Yesu anatuonyesha mfano, Angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake, ni, BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE (Math 6:9) anaanza Maombi kwa kumsi Mungu Baba,

Unaweza ukamsifu Mungu kwa kuimba, kusema, au hata kuyaelezea matendo makuu ya Mungu,

ukifanya sifa vizuri ya kumfurahisha Moyo wake, atakupa hata vile ambavyo haukuomba, wala haukutegemea kuvipata au kuwa navyo. MFALME SULEIMANI aliomba Hekima, lakini Mungu akampa Akili na Utajiri, ni kwakuwa tu , Mungu alipendezwa naye, na akamtadha awe Mfalme.

HATUA_YA_NNE,

MWELEZE MUNGU MAHITAJI YAKO (HAJA ZAKO) Waf 4:6-7,19 / Isa 43:26

¤Mweleze Mungu zile haja zako zilizo kusukuma kwenda kumwomba, Nenda mbele za Mungu kama kuhani, (1petro 2:9) kwa unyenyekevu, na heshima, lakini kabla ya kumweleza Mung mahitaji yako binafsi
. . . .(A) FANYA MAOMBEZI KWAAJILI YA WATU WENGINE. Kama vile,
@Viongozi mbalimbali wenye malaka,
@Watumishi wa Mungu,
@Marafiki zako,
@Shirika lenu, ofisi yenu,
@Chama chenu, nk
Usianze kujiombea wewe mwenyewe tu, Zoea kuwatanguliza wengine katika maombi yako, kwamaana, ukiwaona wenzako ni bora kuliko wewe, ndipo na Mungu atakuona wewe ni bora kuliko wengine

.....(B) KISHA FANYA MAOMBI YAKO, ombea, Omba haja za moyo wako (Math 7:7-11)

Baada ya kuwa umesha ombea wengine, ndipo uanze kumweleza Mungu haja na Shida zako, Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli, japo yeye anayajuwa tunayo yahitaji hata kabla hatumwomba, lakini yeye ameagiza kwamba tumwombe, ndipo yeye atafanya,

Aombaye hupokea, yaani asiye omba hawezi kupekea,

Mungu anasema, Tumpelekee hoja zetu zenye nguvu (Isa 41:21) Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upate kupokea.

somo_litaendelea nitakuletea hatua ya 5,6 na 7,

By mwinjilisti Gerald Robert

 

Comments