KUPITIA NENO LA MUNGU AMEMILIKI BIASHARA YAKE MWEYEWE


God Paid my School Fee

MTOA SHUHUDA: Maria Paschal USHUHUDA:
 Alikuwa hana mtaji, hana biashara... lakini Alivyopokea NENO la Jumapili iliyopita na Kutii,... Ndani ya Week tu Amepata mtaji na Sasa ana Biashara yake. Mwana wa MUNGU Maria Paschal wa Eneo la Upendo Mwanzo Mpya, Efatha Mwenge Dar es Salaam-Tanzania, leo aliamua kuja mbele ya Wana wa MUNGU, kuja kushuhudia Mambo Makuu ambayo MUNGU wetu Amemtendea ndani ya week baada ya KUTII Neno alilopokea.

Maria alianza kusema kuwa alikuwa hana mtaji, wala biashara yeyote. Jumapili iliyopita baada ya kuhudhuria Ibada kanisani, aliondoka na lile la Mahubiri ya Mtumishi wa MUNGU la ''UTII''. Toka siku anasema kuwa aliamua kuwa MTII, kuanzia Nyumbani mpaka Zone. Jumanne alihudhuria Ibada ya Zone kwenye Eneo lake, Askofu wake alitangaza siku ya Kushuhudia, Maria anasema Aliamua kutii hilo tangazo, na alifurahi sana kwani Anapenda sana Kushuhudia. Alhamisi tena kulikuwako na Tangazo kuwa wakina mama wote wanatakiwa kukutana Nuru Centre, ... Naye Maria anasema alitii na akaja hiyo Alhamisi Nuru Centre.

 Baada ya mkutano wa akinamama, alirudi nyumbani... Usiku wa Manane, Usiku wa Tisa Maria anasema alishangaa Simu yake inalia, inaiita. Alipoipokea, aliambiwa kuwa ''Nimekutumia Hela kwenye Simu yako, Nimekutumia Mtaji'', Haleluya. Maria anasema alishangaa sana, ... basi hakuchelewa asubuhi aliamka na kwenda kununua mchanga kwa ajili ya kuanza kufanya biashara. Alipofika pale kwenye hilo eneo la kununua mchanga, aliambiwa kuwa Serikali imekataza kuchimba mchanga hapa, kwa hiyo hakuna sehemu ya mchanga kuuza hapa.

Maria Anasema hakukatamaa, akanza kumwambia BWANA YESU...''BWANA YESU Si unona hapa hakuna mchanga, na mimi nataka mchanga'' Basi mara akashangaa, malori ya mchanga yakatokea pasipokujulikana, madereva wa wale wenye mchanga wakaanza kumwambia, ''mama chukua huu mchanga, chukua huu, Chukua mimi hela nitafuata baadaye, chukua hela nitafuata tu...''. Haleluya MUNGU wetu ni MZURI sana, ANAWEZA katika yote, leo hii mwana wa MUNGU Maria Paschal ana biashara yake ya Matofali, na inaendelea Vizuri sana, Haleluya. Haleluya MUNGU wetu ABARIKIWE, na ATUKUZWE DAIMA.
                           - Efatha-


 

Comments