KUSHINDA LAANA NA MAGONJWA YA KURITHI.


  LAANA:

Laana ni kile ambacho mtu anakirithi au kukipata kama amefanya makosa yeye au mtu mwingine kwa niaba yake,mfano sisi tumerithi laana ya Adamu.
Hivyo laana ni dhambi ya urithi kwa mtu kutoka kwa mwingine.
Tukosoma maandiko laana huende hadi kizazi cha nne lakini kimahesabu ya biblia laana haishi kwa maana namba nne ni namba mzunguko.
Ndio maana unaona hata leo sisi bado tuko katika laana za Adamu hivyo kwa ujazi nitakupatia mfano wa mambari zilivyo.
1babu/2baba/3mtoto/4mjukuu/5kitukuu
1babu kutoka 2/baba kutoka3/mtoto4/mjukuu
1 2 3 4
Kwa maana nyingine mjukuu atakuja kuwa babu hivyo huo ni mzunguko kamili hivyo ndivyo laana inavyofanya kazi.
Kwa hiyo unaposhughulikia laana hakikisha unashuhulikia mfumo mzima wa ukoo au familia maana mjomba wako pia ni mifupa yako na bibi mzaa mama yako ni mifupa yako na babu mzaa baba yako alivuka nawe katika laana akiwa katika viuno vya babu yako sasa hapo ndio utajua jinsi unavyozungukwa na laana.
Wazazi wetu walitoa kafara pamoja nasi tukiwa katika viuno vyao kabla hata ya kuzaliwa fanya maping za kujitoa kwani nawe ulishiriki naye naye alikukabidhi katika madhabahu hizo kwa hati maalum hivyo bila kufuta hizo hati ni kazi bure.
Hii inatenda kazi pasipo kujua au hata ukijua bila kushughulikia tatizo lilipoanzia ilanakuwa ni tabu kuachana nayo.
Watu wengi husubuliwa na laana nao kwa kuwa hawafahamu huona ni kama kitu cha kawaida tu.
Mfano mzuri wa hili ni kama magonjwa ya vipindi Fulani,Kukosa fedha kwa muda Fulani, Kuwa na matatizo kwa muda Fulani,Hata kuwa unazeeka hujao wala kuolewa,Elimu katika familia wote mwisho ni darasa la nne tu ,kfeli shule,kufa kabla ya umri wa uzee,kuwa wganga wa kienyeji nk.
Hivi vyote vina sababu zake na kuna jinsi ya kuvishinda Yesu kafa msalabani ni sawa lakini bila wewe mwenyewe kuchukua jukumu la kuona kuwa hiyo ni shida juu yako huwezi kukwepa kuhusika navyo.
Chora jedwari linaloonyeshwa familia yako kwa ujumla ilitoka wapi inaelekea wapi na anza kupitia baadhi ya mambo utagundua shida iko wapi na anza kushuhulikia hiyo shida hakuna sehemu ambapo umeandikiwa huta olewa wala kuoa au kufa kabla ya umri wako wa utoto maana ahadi za Mungu ni kweli na milele.
AMENI

By Salvation Choir Hebroni

Comments