KUZIJUA NA KUWEZA KUZIPINGA HILA ZA SHETANI (sehemu ya kwanza)

Mtumishi wa MUNGU Nickson Mabena akifundisha neno la MUNGU

Waefeso 6:11

"Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kuweza kuzipinga hila za shetani"

Hila maana yake ni udanganyifu, uongo au ulaghai; au ninaweza kusema ni kitendo cha kutanguliza ukweli ili ukubalike ila ukitafuta namna ya kuachilia uongo utakaoleta uharibifu.

Muasisi mkuu wa hila ni Shetani mwenyewe, ingawaje kwa sasa anawatumia watumishi wake kutekeleza hayo kwa lengo la kuleta uharibifu kwa kanisa na kwa watu wa Mungu kwa ujumla.

Tunaona kwenye bustaniya Edeni alipomdanganya Hawa, alimletea maneno matam sana na mazuri pia yanayovutia kumbe alikuwa anatafuta namna ya kukubalika kwao, Hawa bila ya kutambua kwamba ilikuwa ni hila tu akampa nafasi, na ndipo kilipozaliwa kifo cha kiroho.
ona; Mwanzo 3:4
"Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa".

Nyoka alimhakikishia kabisa mwanamke, akampa usalama wote juu ya kuyasikiliza maagizo yake!!

NDIVYO AFANYAVYO SHETANI KATIKA KANISA HATA LEO.

2Kor 11:3
"Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake asije akawaribu fikra zenu, mkauacha unyoofu na usafi wa Kristo"
Paulo analiandikia kanisa ya kwamba, anahofia (anachelea) kama vile nyoka alivyofanya kwa Hawa ndivyo anavyofanya pia kwetu, yaani mbinu zilezile alizozitumia kwa Hawa ndizo hizo hizo anazotumia katika kanisa la leo ili tuuache usafi na unyoofu katika kumfuata Yesu Kristo.

Kama ukichunguza kwa makini hali ya kanisa ilivyo; utagundua kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu umepungua katika maisha ya mwamini kwa asilimia kubwa sana, sababu kuu ikiwa ni Hila ziletwazo na Shetani kwa kanisa.

Roho Mtakatifu kwa kinywa cha Paulo analitahadharisha Kanisa ya kwamba shetani asije akaziharibu fikra zetu!!

Kumbuka kwenye somo letu tunazungumzia HILA ZA SHETANI, sasa usitegemee shetani akaja mzimamzima kuja kukudanganya, bali huwatumia watu wako wa karibu kabisa, kwenye familia, Kanisani, au kazini,shuleni n.k

Nimekutana na watu wengi sana ambao maisha yao yamepoteza muelekeo kwa sababu tu, walidanganywa na wakajikuta future zao zimepotea;
Kuna Mabinti kadhaa ambao niliwafahamu kama watumishi wazuri wa Mungu, lakini utumishi wao umepotea kwa sababu tu ya kudanganywa na maajenti wa shetani, wengine wamezaa watoto lakini ni nje kabisa ya mpango wa Mungu!!
Wengine wamebaki wanalia tu hata Moyo wa Ibada haupo tena kwa sababu walitendewa vitu vibaya na watu waliowaamini ya Kwamba wameokoka vizuri.

Wengine walipodanganywa ya kwamba wataolewa, waliposadiki tu maneno hayo wamejikuta kwenye wakati mgumu sana;

Kumbe wasijue ya kwamba wamebeba HILA ndani yao, bali walichanganyikiwa na maneno matamu waliyoambiwa na wao.

Yesu aliwajua wenye roho za nyoka ndani yao;
"Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake." MATH 12:34

Kumbe wapo watu wanayanena mema ingawa wamejaza ubaya ndani yao (HILA), Yesu aliwaita wazao wa nyoka.

Ndugu yangu si kila maneno ni ya kuyasadiki, mengine ni sumu kwako wewe uliyeokoka,yanawinda kiroho chako tu!

Maneno ya kuyasadiki ni habari njema tu za Ufalme wa Mungu......


Kwa Maoni na Ushauri wasiliana nami kupitia; phn no. 0769323490, 0712265856


Nickson Mabena
  email adress: mabenanickson@gmail.com

<<<<SOMO LITAENDELEA>>>>>>

Comments