Maadhimisho ya Miaka 20 ya Dayosisi ya AICT Shinyanga.


Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga linakukaribisha kwenye Maadhimisho ya Miaka 20 ya Dayosisi hiyo. Ratiba Nzima ya Maadhimisho hayo ni Kama Ifuatayo: Kuanzia 18.10.2013 mpaka 20.10.2013 kutakuwa na Tamasha la Uimbaji.

Kuanzia 21.10.2013 Asubuhi na Jioni mpaka 26.10.2013 kutakuwa na Mkutano wa Injili. Na Siku ya Hitimisho yaani Octoba 27, shughuli nzima itakuwa ikifanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage. Wageni watakaokuwepo ni Maaskofu wote wakiongozwa na Askofu Mkuu wa CCT Dr. Alex Malasusa.
Kitenge Maalum cha Kuvaa siku ya Kilele cha Maadhimisho haya
Siku ya hitimisho yaani October 27 Siku ya Jumapili, kutakuwa na Changizo kwa ajili ya kuchangia shule ya Kanisa inayoitwa Bishop Nkola Secondary School na Mgeni rasmi wa Changizo Hilo ni Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowasa na Mc wa Changizo hilo atakuwa ni Masanja Mkandamizaji.
Tshirt maalum kwa ajili ya Maadhimisho haya
Kwaya zote za Aict Shinyanga zitakuwepo na Kwaya ngeni ya CVC kutoka Dar es salaam pia watakuwepo. Kwaya za shinyanga zitakazo kuwepo ni Aic Shinyanga Choir, Aic Kambarage Choir, Mwadui Choir, Malampaka na nyingine nyingi.

Kwa Mawasilino Zaidi
0752 521 353

Wote Mnakaribishwa 

Gospel News Media

Comments