MAISHA NA UJUMBE WA YESU HUSABABISHA MABADILIKO





Tazama maisha na mvuto wa Yesu wa Nazareti, Mesiya, katika historia yote na utaona kwamba yeye na ujumbe wake huleta mabadiliko makubwa katika mataifa na maisha ya wanaume na wanawake. Popote mafunzo yake yalipoenea, utakatifu wa ndoa, haki na sauti ya wanawake imetiliwa maanani; shule na vyuo vikuu vimeanzishwa; sheria za kulinda watoto zimeandikwa; utumwa umeachishwa; na mabadiliko mengine mengi yamefanywa kwa manufaa ya wanadamu. Maisha ya watu binafsi yamebadilishwa kiajabu. Kwa mfano, Lew Wallace, jemedari aliyejulikana na mwandishi shupavu, alikana Mungu yupo. Kwa miaka miwili, Bw. Wallace alisoma kwenye maktaba zilizo bora sana kule Ulaya na Merikani, akitafuta habari ambazo zingeangamiza kabisa dini ya Kikristo. Alipokuwa akiandika sura ya pili ya kitabu hicho, alijikuta ghafla ameanguka magotini na kulia kwa Yesu akisema, "Bwana na Mungu wangu."
Kwa sababu ya ushuhuda usioweza kukanwa, hakuweza kuendelea kukana kwamba Yesu Kristo alikuwa mwana wa Mungu. Baadaye, Lew Wallace aliandika kitabu kilichoitwa "Ben Hur", moja wapo ya vitabu shwari vilivyo andikwa katika lugha ya Kiingereza kuhusu nyakati za Kristo.

Vile vile, marehemu C. S. Lewis, profesa wa chuo kikuu cha Oxford, alikana kwamba Kristo alikuwa pia Mungu kwa miaka mingi. Lakini, yeye pia, kwa hekima za ukarimu, alijinyenyekeza mbele za Yesu kama Mungu na Mwokozi baada ya kusoma ushahidi usio na pingamizi kwamba Yesu pia alikuwa Mungu .

Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako ya hapa duniani na pia ya uzima wa milele yatategemea jibu lako kwa swali hili.

Dini zote zingine zilianzishwa na wanadamu na zinategemea falsafa za kibinadamu, kanuni na pendekezo za tabia. Ondoa waanzilishi wa dini hizi kutoka idhini na tabaka za kuabudu, na machache sana yatabadilika. Lakini ondoa Yesu Kristo kutoka Ukristo na hakuna chochote kitakachobaki. Ukristo uliopendekezwa kwenye Biblia siyo falsafa ya maisha peke yake, wala siyo tabaka na njia za kimila za kuabudu. Msingi wa Ukristo wa kweli ni uhusiano wa kibinafsi na Mwokozi na Bwana aliyefufuka na anayeishi.
MWANZILISHI ALIYEFUFUKA
Yesu wa Nazareti alisulubiwa, akazikwa kwenye kaburi lililokopwa, na siku ya tatu alifufuka kutoka wafu; Ukristo niwa kipekee kwa ajili ya jambo hili. Ubishi wowote juu ya ukweli wa Ukristo utategemea uthibitisho wa kufufuka kwa Yesu wa Nazareti.

Katika enzi zote, waliohitimu katika masomo na kuchunguza sana mathibitisho ya ufufuo wameamini, na wangali wanaamini kuwa Yesu yuhai. Baada ya kuchunguza mathibitisho ya ufufuo kama yalivyoandikwa na waandishi wa Injili, marehemu Simon Greeleaf, aliyehitimu kwa mambo ya kisheria katika Harvard Law School, alisema; "Haingewezekana kamwe kwao kuendelea kusisitiza ukweli wa mambo walionena, kama Yesu kweli hakufufuka kutoka wafu, na kama hawakujua jambo hili kama walivyojua ukweli wowote mwingine walioujua kwa uhakika.
John Singleton Copley ambaye ni mwanasheria aliyetambulikana sana, alisema: "Najua kiasi kwamba ushahidi ni kitu gani; nakwambia, ushahidi kama ule uliotolewa kuthibitisha ufufuo bado haujawahi kuvunjwa."
MUNGU awabariki sana
ITAENDELEA..........

Comments