Maombi ya kushughulikia Kinywa, kisilete madhara kwa wengine,


NGUVU YA KINYWA,
Mtu wa Mungu Nabii: Samson
Utangulizi: kila kinywa  kina nguvu sana nguvu ya kujenga au kuharibu kinywa kina nguvu ya kuuwa au kufufua kinywa kina nguvu ya maamuzi kukusanya au kutawanya kupendezesha au kuchafua kinywa kina nguvu ya kulaani na kubariki kinywa kina nguvu ya kukupeleka Mbele au kukurudisha nyuma, kinywa kina nguvu ya kuokoa na kina nguvu ya kupoteza, inatengemea jinsi utakavyo kitumia kinywa chako, sasa katika somo Mungu atatufundisha namna ya kutumia hii nguvu iliyoko katika kinywa, nguvu nini?
         
NGUVU:
Nguvu ni  uwezo wakusababisha jambo unalolitaka litokee  likatokea kwa muda ule unaohitaji litokee, sasa nguvu isiyo na uwezo wakusababisha jambo likatokea mimi siongelei ya namna hiyo bali mimi naongelea ile nguvu yenye uwezo wa kusababisha jambo likatokea, haswa nguvu iliyo katika kinywa, kwa mfano tuangalie maandiko matakatifu hapa,
Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.
Mhubiri 9 : 16
Kwanini hekima iwe na ubora kuliko nguvu alafu hapo hapo hekima hiyo inapokuwa kwa masikini inadharauliwa na maneno yake hayasikilizwi hii inamaanisha kumbe ili masikini asikilizwe kunahitajika nguvu ya kusababisha  yeye asikilizwe,asababishe jambo litokee lionekene,
hekima inapokuwa kwako usipoitumia inahama kabisa inaenda kwa mwingine  anayeihitaji wewe unabaki na kunywa kilicho na mizaha, hapo ndipo unamkuta mtu wakati wote amebakiza mizahaa tu,
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
 Naye atakuwa Kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake Kwa majira yake, Wala jani Lake Halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. Zaburi 1:1-3
Kumbe unaweza kuwa Na kinywa lakini ukawa hauna nguvu  nao  ukiongea usisikilizwi, kinywa chako kitakuwa na Nguvu pale Mungu atapokuwezesha vinginevyo nisawa na kuwa na mali ambazo hazitumiki,
         
Luka 21:15
kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.
Nanyi mtasalitiwa Na wazazi wenu, Na ndugu zenu, Na jamaa zenu, Na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.
Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.
Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.
Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.
Kusudi kuu la Mungu kukupatia Kinywa ni kwaajili ya wewe kutabiri juu ya maisha yako kwanza angalia maandiko Matakatifu usisubiri utabir aza kutamka yale unayosukumwa ndani ya Moyo wako tabiri sasa usingoje kutabiriwa, onyesha kuwa umekubali mbele za bwana
Ezekieli 37:11 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.
Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
Ukiendelea kufuatilia kwa karibu kwa habari ya Ezekieli utagundua sababu ya Mungu kumleta katika bonde lile lililojaa mifupa. Kwanza, Imani ya Ezekieli ilikuwa imani yenye matumaini. Ingawa hali halisi ya mifupa ilikuwa imekwisha kauka, yeye alibaki na tumaini kuwa mifupa ile yaweza kuishi.kwakuwa aliamini Mungu hashindwi na jambo,
Sasa hatua kubwa sana ya Mtu ni ile kudhihirisha kuwa mtu anamjua Mungu na kumtumaini kwa kila jambo na popote  hata  katikati ya vita, au hali za kukatisha tamaa, au hana analolitegemea katika maisha yake lakini bado anataja mambo yajayo, anataja matendo makuu ya Mungu.na kuamini Mungu atatenda,
Mungu hataki  ukate tamaa, wala umkufuru yeye katikati ya magumu au matatizo  ukifuatilia kwa umakini mkubwa katika maandiko matakatifu watu wakubwa katika biblia hata walioitwa na Mungu, walipitia magumu lakini katikati ya magumu hayo walitamka maneno ya ushindi.
Pia, kutamka maneno ya matumaini katikati ya magumu kunakufanya utoke mapema kwenye hali mtu aliyoko ila ukionyesha kushindwa unaruhusu uvamizi
Inawezekana unapitia katika hali ngumu kwa sasa, lakini utakalolinena ukiwa katika dhiki hiyo itakufanya utoke ukiwa shujaa au aliyeshindwa.  Maamuzi unayo wewe mwenyewe Na ndio maana hata Ezekieli alipowekwa mbele ya mifupa mikavu na kuulizwa 'je mifupa hiyo nyaweza kuishi?' Naye alijibu kuwa 'wewe Bwana wajua’ akionyesha kuwa hakuna jambo la kumshinda Bwana. Na ndio maana hata alipopewa nafasi ya kutamka neno alitamka uzima. Ni muhimu kujua maneno ya kutamka pindi unapopitia katika hali ngumu au matatizo, unaweza ukaharibu au ukajenga
Ni muhimu kujua unachokiongea leo ndicho utakachokiishi kesho wewe na kizazi chako na jamii iliyokuzunguka wengine hujikuta wanaongea maneno mabaya juu yao wenyewe, huku wakisahau kuwa ni shetani ambaye anawafanya waongee maneno hayo ili apate nafasi ya kuharibu maisha yao baadaye.
Isaya 57:10 "ulikuwa umechoka kwaajili ya urefu wa njia yako, lakini hukusema hapana matumaini, ulipata kuuhishwa nguvu zako, kwasababu hiyo hukuugua" kumbe watu hawa, hali yao halisi iliwafanya wakate tamaa ya kufika wanapokwenda lakini pamoja na urefu wa njia bado walichukua hatua walikiri kuwa matumaini yapo. Na kwasababu ya ukiri huo walipewa nguvu mpya. Usikiri udhaifu, Mungu anayetenda miujiza yupo na ukimkimbilia yeye, ataiondoa aibu yako na kukuvika heshima.
Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.
Ayubu 18:7
Kumbe katika hatua kuna hatuwa  zanguvu na hatuwa lege lege sawa sawa na Neno la Mungu hatuwa za mtu zinasongwa na shahuri lake mwenyewe, shahuri unalo wewe mwenyewe juu ya wewe kuchukuwa hatua au kubaki kama ulivyo,
Kwa mfano: Ukifuatilia habari ya Yusufu ambaye maisha yake yalianza kwa kuuzwa na ndugu zake kwa wamisri. Na alipouzwa waliigawa kanzu yake maana yake aliuzwa bila mavazi yaani uchi,
Lakini akiwa Misri na matumaini yakaanza kuja likatokea jambo jingine la kukatisha tamaa. Mke wa potifa akamsingizia kuwa anataka kumbaka, hivyo akatupwa gerezani maisha nikukumbushe na hapa tukio linalofanana na la mwanzo likamtokea baada ya Yusufu kusingiziwa na kukimbia Vazi lake lilibaki mikononi mwa mke Potifa Hivyo anaondoka bila nguo tena nguo alipatia Gerezani tena za wafungwa,
 Katiaka hali hiyo ni dhahiri kuwa Yusufu alikata tamaa kabisa. Lakini alipotoka gerezani Yusufu akawa waziri mkuu, jiulize, Mungu aliyemfanya kuwa waziri mkuu alikuwa wapi kipindi anauzwa? Au jiulize alikuwa wapi kipindi anawekwa gerezani? 
Ni muhimu kujua kuwa kupitia hali ngumu,au katika tatizo flani  ukahisi Mungu amekuacha, si kweli; Mungu bado yupo pamoja na wewe na matumaini bado yapo. Yesu Kristo ni tumaini la kutosha kwenye maisha yako. Leo sikia sauti yake hii ikisema Usiogope hali unayopitia . Pata muda kuingia kwenye maombi na Mungu atakupa tumaini jipya leo. Inawezekana unapitia shida za ndoa, matatizo kazini,katika biashara, vita shuleni, roho ya kukataliwa mpaka umejihisi hakuna kesho ile uliyoiwaza.
 Leo tambua kuwa hata Ayubu katikati ya dhiki kuu hakuwahi kumkufuru Mungu aliyemtumikia  bali aliweka tumaini lake kwake na kwa saa sahihi matumaini makuu yalionekana.leo kwetu ni somo,
Kuna mtu anasubiri somo kutoka kwako juu ya hali yako unayopitia sasa usiposhinda utasababisha na wengine watapopitia hali kama yako washindwe kama wewe unavyotaka kushindwa usikubali kushindwa Mwamini Mungu Mtumaini kama walivyokusha kushinda wanavyotufundisha,
Hata kama ndoto yako inaonekana inataka kuzimika,Huduma kisimati, inawezekana ulikuwa na ndoto za kusoma katika maisha yako lakini sasa unaona muda umeenda nakwambia bado lipo tumaini.ulikuwa na ndoto ya kuoa au kuolewa ukahisi muda umeenda bado ushindi upo tena  Inawezekana madktari walikwambia kuwa mwisho wa kuzaa ni miaka 45 na wewe sasa unajiona unaelekea huo umri ukiwa hauna mtoto lakini nakwambia neno ambalo Yesu amenituma kwako nikuambie sema neno juu ya maisha yako chukuwa hatua ya kufanya hivyo na subiri Mungu atende ukishatamka acha kumsaidia Mungu kwakuharakisha, Mwache Mungu atende kwa majira yake, usije juta,!!
Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.
Zaburi 18 : 36
Ndani ya nafsi ya kila mwanadamu kuna hatua ndiyo maana kunawatu kimawazo wako mbali sana hatakama hana kipato kibwa lakini anahatuwa kubwa sana ndani ya moyo wake,  jambo lolote linalotokea halitikei hivi hivi bila nguvu ya hatua kufanyika nayo inaanzia ndani ya moyo wa mwanadamu,
Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki.
Zaburi 119 : 133
Mungu anaelekeza je  hatua zao ni ndani ya moyo wako sasa kama Mungu hayumo ndani yako ninani atakayezielekeza hatua zako, ezekieli mkono wa Mungu ulikuwa juu yake akaweza Kutabiri juu ya mifupa mkavu, je swali langu wewe unatabiri wakati gani mkono wa Mungu ukiwa juu yako au ukiwa peke yako,
Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.
Mithali 16 : 9
Omba maombi maalumu juu ya Hatua zako zote kwa kila jambo unalolifanya,
Mungu akubariki kwakufuatilia somo hili naamini Mungu ninayemtumaini ahatoyaacha maisha yako yabaki kama yalivyokuwa mwanzo,
Kwa msaada  wa ushahuri na maombi na maombezi wasiliana na yule Mtu wa Mungu Nabii samson, kwa namba 0756 809 209 0653 22 42 19 ni Bure huduma hii,
DVD VCD Za Masomo ya Mtu waMungu Samson  zinapatikana,wakati wote, umbali Usiwe kikwazo,Nabii Samson, piga simu 0756 809 209

Comments