MATENDO MAKUU AMBAYO MUNGU AMEYATENDA KUPITIA KWA MCHUNGAJI KIONGOZI, JOSEPHAT GWAJIMA WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA, MJINI MOSHI



USHUHUDA WA MAGRETH
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, akimuombea Magreth afunguliwe dhidi ya vifungo vya shetani vya magonjwa.



Magreth akiuelezea umati wa watu katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi kuhusiana na tatizo alilokuwa anasumbuliwa nalo na akielezea kupona kwake.




    Magreth aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo na pia kutokwa na damu (bleeding) kwa muda mrefu sana. Anaitwa MAGRETH, aliyeshuhudia kuwa baada ya kuhudhuria mkutano katika viwanja vya mashujaa amepona kabisa baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima, amepokea uponyaji wake wa tumbo na damu zime acha kabisa kumtoka kwa jina la yesu. Anamshukuru Yesu kwa kumponya.


USHUHUDA WA SARAH




         Binti huyu hapa juu anaitwa SARAH, mkazi wa Moshi mjini, alichukuliwa msukuleni na baba mkwe wake na kumpeleka Singida kulima mashamba ya mahindi na alizeti. Binti huyu alionekana kuchoka sana mara baada ya kurudishwa toka  msukuleni,jambo lililosababishwa na ugomvi uliotokea kati yake na babamkwe wake. Sarah aliendelea kushuhudia kuwa mara baada ya kuanza kuita watu wote waliochukuliwa misukule NJOOO KWA JINA LA YESU, gafla kulitokea ugomvi huko alikokuwa amefungiwa  hadi kujeruhiwa katika mkono wake wa kulia. Binti huyu  alionekana mwenye kuvimba sana mkono wake wa kulia, alipoulizwa kuhusu gomvi wake na babamkwe wake umesababishwa na nini, alieleza kuwa  ilisikika sauti kubwa ya kushtua na kutisha ikimuita ‘Sarah njooo kwa jian la yesu”jambo lililimfanya babamkwe kumpiga na mpini wa jembe mkwe wake na kumfukuzia mbali. Jambo la kushangaza, binti alizidi kueleza kuwa  mipini ya jembe waliokuwa wanatumia kulimia huko msukuleni ni mikono ya wanadamu!! Hakika hakuna lililositirika ambalo halitajulikana. Sarah amefunguliwa na yuko huru kwa jina la yesu.

 USHUHUDA WA RATIFA SIRAJI
    HAKUNA jambo gumu la kumshinda MUNGU! Hata hili ni jepesi machoni pa bwana! RATIFA SIRAJI ni binti aliyekuwa wakala wa shetani  aliyechukuliwa kwa njia ya kichawi na kuwekwa chini ya mto Wami huku kazi yake ikiwa ni kusababisha ajali na kuchukua matumbo ya uzazi ya wanawake kwa njia za kichawi na baada ya hapo alidai wanawake huenda hospitali na kupimwa na kukutwa na matatizo ya kizazi na huishia kukatwa. Jambo la kushangaza binti huyu aliyeonekana mwenye umri mdogo aliezeza kuwa hata alipokuwa anarudishwa alikuwa anatoka matekani alikuwa ametumwa  kusababisha ajari ya gari la MASAMA-SERENGETI ili kuchukuwa vizazi vya akina mama watakao kuwa katika gari hiyo. 
.
Ratifa akikana kumfahamu rafiki yake ambaye wanafahamiana vizuri
Jambo la kushangaza   mara baada ya kurudishwa binti  alikuwa hamtambui mtu yeyote hata yule aliyekuwa naishi nae nyumbani kwao. Hakika yake tunaokolewa kwa neema, hata leo neema ya Mungu ya ukombozi kwa walioibiwa na kutekwa imemfikia mtoto huyu na kumuokoa. Kwa kushuhudia zaidi alieleza kuwa mara baad ya kusikia sauti yenye mungurumo ikimuita “NJOOO” bibi aliyefahamika kwa jina la AMINA ambaye anadaiwa kumchukua na kumuweka mateka aliamua kumtupa katiaka viwanja vya mashujaa. Binti alipata kuombewa na mchungaji kiongozi JOSEPHAT GWAJIMA mpaka ufahamu wake na kumbukumbu zikarejea akawatambua ndugu zake. Yesu ni Yule yule jana leo na hata milele.
Ratifa Siraji akiwa amepona na ameshammpokea Yesu, na kuwekwa huru kutoka katika vifugo vya kumtumikia shetani


Binti aliyekuwa amechukuliwa msukule na hapa pichani akiwa amerudi anamshkuru Bwana Yesu na  Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.

HAPPY MANDALI

       HAPPY MANDALI ni  binti mwenye umri wa miaka 16, anaishi mjini Moshi, amepata kurudishwa toka msukuleni alikochukuliwa na rafiki wa mama yake, ambaye ni mfanya kazi mwenzake.
  Dada huyu anayeitwa happy alionekana mwenye huzuni kubwa iliyoambatana na kilio kikubwa! Jambolilimfanya kuendelea kumsihi mchungaji kiongozi Josephat Gwajima aendelee kumuita mama yake maana binti alidai kuwa amemuacha pia mama yake kule msukuleni ARUSHA. Binti alizidi kusisitiza kuomba mama yake aitwe kwa kuwa aliona mateso na taabu alizokuwa akizipata kule msukuleni.Maandiko lazima yatimie kuwa mwana wa adamu alikuja kutafuta kila kilichopotea hata leo walokuwa wamepote wanaonekana na kurudishwa kwa jina la YESU






USHUHUDA WA AISHA MOHAMED
ASHA MOHAMED ana umri wa miaka 19, amekuwa mjumbe wa shetani kwa kufanyishwa mambo mazito na ya kutisha tangu akiwa na umri wa miaka 8. Asha ameweza kueleza mambo aliyoyatenda japo ilikuwa ni ngumu sana kuongea kutokan na ukweli kwamba alikuwa anasikia uchungu sana kwa kuwa alijiona kuwa mambo hayo yote hakuna wa kumsamehe makosa yake na watu wange mtenga.Lakini Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima alimshauri kuwa Mungu anasamehe kila dhambi hata iwe na ukubwa kiasi gani, cha msingi ni ukiri kuwa umekosa ujinyenyekeshe mbele zake na usiyarudie tena.

Hatimaye Asha akaelewa na akaanza kueleza, kuwa wakati anasoma darasa la nane nchini Kenya, ulikuwa usiku wa manane walimjia kundi la watu wengi wakamzunguka alikokuwa amelala na kumwambia unahitajika kijijini kwenu. Kulipokucha mchana wa saa sita, walikuja wasichana 3, wakiwa uchi walimfunika machoni na gafla alijikuta yuko kijijini kwao katikati ya kundi la wachawi wa kijijini.


Baada ya kuchukuliwa, alianza kufunzwa jinsi ya kuroga, na mwalimu wake alimtaja kwa jina la Hamis. Asha liendelea kupewa kazi na majukumu  kama kubadilishwa maumbile na kuwa mwanaume nakuanza kuwaingiia wanawake usiku jambo lililokuwa likisababisha wanawake kuvunja ndoa zao. Na wakati mwingine alikuwa akiwaingilia wanawake kwa kugeuzwa maumbile alikuwa nasababisha saratani na kupooza. Jambo la kusikitisha sana Asha amekuwa mateka kwa muda wa miaka 11 huku chakula chake kikiwa ni kunywa maji ya chooni!

 Aisha akionesha mkono ambao kulikuwa na kidole cha kichawi ambacho kilikuwa kimeoteshwa kichawi kwa ajili ya kuwanyonya watu damu na kuwasababishia kupooza.

Asha aliendelea kueleza kuwa alikuwa anatumia kucha yake ndogo ya mwisho kuchoma watu shingoni na kunyonya damu mpaka  kumsababishia mauti. Aliendelea kulia sana akidai kuwa amemnyonya damu mdogo wake mwenye umri wa miaka miwili, na pia alisema magonjwa kama ya saratani, na kupooza ni magonjwa ambayo yeye alikuwa anatumwa awasabishiye watu wengi sana.




Aisha Mohamed akiwa anakiri kuwa amechoshwa sana na kazi za ushirikina, akasema anataka kummpokea Yesu, akamkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Muokozi wa maisha yake, na akaokoka.

Comments