Mateso ni nini?

 Na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira

Mateso ni nini?
- Mateso ni hali yoyote ambayo inakunyima wewe kuchangamka.
- Mateso ni kitu chochote kinachoweza kukukandamiza mwili ukasikia maumivu, inaweza ikawa ajali, ugonjwa n.k.
- Hali ya kushindwa kufanya kile kitu ambacho unatakiwa au unatarajia kufanya. Mfano, Unatamani kujenga nyumba lakini huna hela.

Wengine huko nyumba walikopanga hawezi kuweka kanda ya nyimbo za YESU; mwenye nyumba atasema Unawasumbua; au ukinunua kanda ya Neno la MUNGU ukaweka na kuisikiliza, mumeo akaikuta Anakugombeza…! Ni maumivu.

- Aina nyingine ya mateso ni ile hali inayokuzuia kwenda mbele, aidha Kusoma, unataka kufanya Biashara Pesa huna, inakunyima maendeleo yako. Kila ukitamani kufanya jambo linashindikana. Zaburi 107: 13 “Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, BWANA Akawaponya na shida zao zote”.
- Mateso ni ile hali unayosikia ya kuugulia ndani ya moyo na huna njia ya kutatua hilo jambo.

DHIKI
Dhiki ni nini?

Dhiki ni ile hali ya Uhitaji. Unatamani uvae nguo nzuri lakini huna pesa hivyo inakusababishia kuvaa nguo zilizochanika au kuzeeka ambayo ndani mwako hupendi.

Unatamani ule chakula kizuri huna uwezo huo. Ziko jamii hazielewi leo watalala wapi, wengine ni watumishi wa MUNGU!

Wengine wamepanga chumba kimoja na wana watoto wanne; jiko ni hapo hapo, kukaribisha wageni hapo hapo kitandani.

Dhiki ni ile hali ya kutoelewa mtu ale nini, avae nini, asafiri vipi. Mfano mwingine Baba yake mzazi kafa huko Arusha, halii kwa sababu ya msiba umemfika lakini ni namna gani atafika kwenye msiba Arusha. Hana nauli ya kufika huko, hata chakula cha siku hiyo hana!.

Fikiri mtu amefiwa na mume wake na huyo mumewe ndiye aliyekuwa anafanyakazi, kusomesha watoto na kuleta chakula nyumbani. Ana dhiki huyu! Analia ili apate msaada na MUNGU Anajua kuna watu watakaofikiwa na dhiki hiyo ndiyo maana akasema hao wajane YEYE ndiye MUME WAO na ATAWATEGEMEZA. Hivyo Wajane WASIANGALIE shangazi au mjomba, Wanatakiwa KUMWANGALIA MUNGU Tu!

TAABU
Taabu ni nini...?

(Maneno haya Matakatifu, Makuu Yenye HEKIMA na UFAHAMU Yataendelea)
Mwana wa MUNGU huu ni wakati wako wa KUTOKA, USIKUBALI Tena, Ni wakati wako Mwana wa MUNGU KUTOKA, ni wakati WAKO.
BWANA Akakuridhie.”

Comments