Skip to main content
MAUAJI YA MASHEIKH MOMBASA!!! GHASIA ZAZUKA... VIJANA WA KIISLAM WACHOMA KANISA MOTO
 |
|
Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema kuwa vijana
wameteketeza kanisa katika ghasia ambazo zimezuka kufutia kuuwa kwa
mhuburi wa kiisilamu.
Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa kwenye ghasia hizo.
 |
Salvation Army Church |
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake watatu.
Polisi
ya Kenya imetangaza kuwa, watu wanne akiwemo Sheikh Ibrahim Ismail Rogo
wameuawa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana ndani ya gari
dogo jana usiku huko mjini Mombasa.
Taarifa ya Polisi ya Kenya
imeeleza, Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa mrithi wa Sheikh Aboud Rogo
ambaye naye aliuawa na familia yake kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana mwezi Agosti 2012.
Mauaji ya Sheikh Ibrahim Rogo
ambayo yameutikisa mji wa Mombasa, yametokea baada ya kupita takriban
wiki mbili tokea kundi la al Shabab lilipovamia na kuua watu
wasiopungua 63 na kujeruhi mamia ya wengine kwenye jengo la maduka ya
biashara la Westgate jijini Nairobi.
Baadhi ya wananchi wa Mombasa wanakituhumu kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi kuwa ndicho kilichotekeleza mauaji hayo.
Sheikh
Ibrahim Rogo ambaye alikuwa akitoa mihadhara kwenye Msikiti wa Musa
mjini Mombasa alituhumiwa na jeshi la polisi kuwa anawachochea vijana wa
Kiislamu kujitumbukiza kwenye makundi ya kigaidi.
Polisi ya
Kenya imesema kuwa, Gaddafi Mohammad, Issa Abdallah na Omar Abu Rumeisa
ni miongoni mwa waliouawa, naye Salim Aboud alinusurika kwenye
shambulio hilo.
Comments