MIAKA KUMI NA TANO YA MATESO NA MAGONJWA YAKOMA BAADA YA MAOMBI

Mama Anna (kushoto) akiwa na Anna mwanaye ambaye alimleta mkutanoni

Mama Anna ambaye ameletwa na mtoto wake kutoka Babati  ili apate kuombewa na kupona tatizo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda wa miaka 15; mtoto wake anasimulia kuwa mama yao huyo aliumwa sana kwa kipindi cha miaka kumi na mitano na hospitali zote wameshindwa kumtibu, ikefikia kipindi inambidi awekewe mtungi wa oxygen kwa ajili ya kupumua.




Lakini siku ya jumapili wakasikia kuwa kuna mkutano mkubwa wa injili unafanyika jijini arusha ukiongozwa na mpakwa mafuta wa Bwana Yesu Kristo, Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima pamoja na watendakazi wake, na wakawa pia, wamesikia kupitia watu mbalimbali, matendo makuu ambayo Mungu anayatenda kupitia mkono wa Mchungaji huyu.



Ndipo wakafunga safari yakuja na kumkuta Ministry Pastor aitwaye Peter na akamuombewa na kukemea magonjwa yote amabayo yalimsibu mama huyo na huyo akohoa kwa sauti kubwa sana kwa mara saba na baada ya hapo akawa na uwezo wakutabasamu na ndipo kila mtu pamoja na watoto wake walio mleta walipomsifu Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea.

MUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE!!!

Comments