![]() |
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ (T) Church - ufufuo na uzima, , akiwaombea maelfu ya watu katika mkutano wa Injili uliofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi. |
Kijana huyu anaitwa CHARLES, anaumri
wa miaka 11, alichukuliwa na bibi mmoja, akampeleka shimoni. huko shimoni
alikuwa anafanyinywa kazi ngumu za kulima mtama, huku akinyweshwa damu na
kulishwa nyama za wanadamu anaema kulikuwa na wachawi wengi wafupi. Mtoto huyu anasema alichukuliwa mwaka 2012 mwezi wa
sita. mama yake mzazi hakujua hayo yote ila alituelezea kuwa alichoshangaa ni
mtoto wake kubadilika tabia ghafla na kuwa mkorofi kupita kiasi, hata kufikia
hatua ya kuwa anacharuka ghafla katika vipindi tofautitofauti, bila sababu na
kuanza kummpiga mama yake, Anamshukuru Yesu kwa kumtoa mautini na kumpeleka
uzimani na pia akaongeze kusema kuwa huko shimoni huyo bibi ameshafariki baada ya maombi ya Mchungaji.
![]() |
Kijana charles baada ya kufunguliwa aliweza kumsifu Mungu kwa nyimbo,akiwa na mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Florah Mbasha. |
Saumu ni msichana aliyekuwa anaishi Mjini Moshi, lakini kumbe alikuwa amechukuliwa kwa njia za kishirikina na kuwa msukule na kufanyishwa kazi ngumu, na alikuwa amewekwa kwenye Giza na aliyemmpeleka ni kaka yake kabisa anayeitwa matei.
Alisikia sauti kubwa ya watu wengi ikimwita njoo na akatoka na kukimbia, na akajikuta yuko uwanjani.
![]() |
Msichana Saumu aliyerudishwa toka msukuleni na Bwana Yesu kuptia mchungaji kiongozi Josephat Gwajima. |
Huyu ni msichana anayeitwa Matronia ambaye anashuhudia kuwa alikuwa amechukuliwa na mama yake mdogo huko marangu na kuwekwa nyuma ya mlango, na chakula alichokuwa anakula ni pumba na damu za watu.
Lakini ghafla akaanza kuskia sauti inamuita njoo na akakimbia, Matronia alikiri kummpenda Yesu na Kuwa Yesu ni Mungu na akaahidi kumkabidhi Yesu maisha yake, na kumtumikia.
Huyu alikuwa amechukuliwa na jirani yake aitwaye patricia na kuwekwa kwenye mtii uitwao Mruka |
Msichana Beatrice wa Moshi ambaye anaombewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima. |

Beatrice ambye
alielezea kuwa mashangazi zake walimchukua na wakamfungia katika msitu
wa kilema, na wakawa wanamdai mbuzi, huku wakimmpa mateso na kumkataza
na kumfunga asiolewe, lakini alifunguliwa kwa Jina la Yesu na Mchungaji
Kiongozi.
![]() |
Bibi ambaye alisumbuliwa na shetani kwa kufanywa chuma ulete na kuletewa matatizo ya miguu hadi kufukia kutumia magongo lakini baada ya maombezi Yesu alimmponya na kumuweka huru na akayaacha magongo. |
Comments
Mwalimu, Cyril Kibali
MWANZA.