NATAKA KUONA * sehemu ya tatu * Marko 10:51

Na mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Haleluya…
Nasema,
Haleluyaa…

Karibu tuendelee kujifunza katika fundisho letu.
Kupitia fundisho hili ,
tunajifunza jambo moja kwamba yatupasa tupate KUONA KIROHO katika huduma zetu na maisha ya kila siku ambayo yamejaa kila aina ya vita.
Tulisoma andiko letu la msingi kupitia kitabu cha Marko 10:46-52.

Kupitia Marko 10 :46-52.
Tumeona jinsi Bartimayo mwana wa Timayo,alivyokuwa na shauku ya kutaka kupata KUONA.
Biblia inatuambia kwamba Bartimayo alikuwa ni kipofu mtu mwombaji.

Lakini mtu huyu alikuwa na akili nyingi sana kwa maana alichokijiua yeye ni kwamba uponyaji wake upo kwa Bwana Yesu tu na sio kwa mwingine awaye yote.

Hapo hata mimi akanishangaza mno,tena akanishangaza zaidi pale alipopiga hesabu kali,kisha akajua jambo moja kwamba, endapo ataendelea KUKAZA KULIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA sawa sawa na neno la Mungu lilivyoandikwa katika kitabu cha Warumi 10 :13,tunasoma hapa;

“ kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.”

Hivyo Bartimayo alipaza sauti yake,ingawa wengi walimkemea anyamaze,Lakini alingangana kumpazia sauti Bwana,Jambo moja la msingi tunalojifunza katika eneo hili ni kwamba,
Mazingira kawaida hayataki wewe upokee muujiza wako,

Hivyo wengi watakukemea unyamaze. Lakini ukiendelea Kuliitia jina la Bwana hakika utapokea muujiza wako.

Bartimayo alikuwa omba omba kila siku.
Lakini pale aliporehemiwa na Bwana Yesu tunaona Bartimayo anaomba sasa kwa mara ya kwanza jambo moja zito,
Anapeleke sasa hoja kamili kwa Bwana.

Kwa maana nyingine ni kwamba,Bartimayo hakuwahi Kuomba hata siku moja bali alikuwa akiomba omba kila siku.

• Ipo tofauti kubwa sana kati ya OMBA OMBA na KUOMBA.
Omba omba ni kule kupeleka hoja isiyo kamili mbele za Bwana au kwa mtu yeyote yule.

Mfano wa omba omba ni huu hapa ;

“ Baba wa mbinguni naomba unipe mke,naomba unipe chakula nile,naomba unipe watoto,naomba unipe gari,naomba Baba unipe kiwanja,naomba uwafanye wanaonidai wasahau madeni yao kwangu,naomba nipandishwe cheo,naomba familia nzuri,N.K”

Ukichunguza vizuri maombi hayo,utagundua mtu huyo alikuwa akiomba omba maana yake hakuwa na hoja kamili mbele za Bwana.
Sababu pale alipoanza kuliombea jambo moja gafla hajalimaliza jambo hilo,kisha akaanza kuliombea jambo jingine,tena gafla kaweka na jingine,
Mtu wa namna hiyo ni OMBA OMBA.

Bartimayo naye hapo awali kabla ya kupokea muujiza wake kwa njia ya REHEMA alikuwa ni mtu omba omba sadaka,hakuwahi KUOMBA.
Simply,Omba omba ni BEGGING

Lakini tunapozungumzia KUOMBA ambako sio kuomba omba kwenyewe KUOMBA kunatokana na neno PRAISING/KUSIFU UUMBAJI WA MUNGU.

Sasa yeye ANAYEOMBA huwa ni Yule kwanza huanza na kusifu jina la Bwana maana Bwana huketi katika sifa.

Hivyo OMBA OMBA huwa hajibiwi hata aombe vipi mbele za Bwana maana hana hoja kamili maandiko yanatuambia tupeleke hoja kamili,yenye nguvu mbele za Bwana.

Sasa angalia kwa habari yetu ya Bartimayo aliyekuwa kipofu;
Alipokuwa omba omba hakuwai kupata KUONA hata mara moja,wala sadaka alizokuwa akiomba hazikumsaidi kuona!

Bali alipopata Rehema kutoka kwa Bwana,tunaona kwa mara ya kwanza AKIOMBA/PRAISING kisha Bwana Yesu akamwambia “ Wataka nikufanyie nini ?” Marko 10 :51

Ooh, kumbe!
Nimegundua kitu hapo,maandiko yanatuambia;

“Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.” Yoh.9:31

Tazama Bartimayo hapo mwazo alipokuwa omba omba hakuweza kusikiwa na Bwana maana yamkini alikuwa na dhambi,Hivyo Mungu hakuweza kumsikia wakati akiomba omba. Bali aliposamehewa dhambi zake,
Mungu akamsikia kwa mara ya kwanza naye Yesu akamuuliza wataka nikufanyie nini ? Maana Yesu hasing’eweza kumuuliza hivyo kama asing’emsikia,alimsikia kwanza pale alipokuwa safi baada ya rehema,
ndipo akampa kuona kadri atakavyo yeye.

Leo wapo wengi wanafanana na Bartimayo pale alipokuwa kipofu mwenye dhambi,Nao watu hao huomba omba mbele za Bwana. Mungu hawasikii wao,
sababu ya uwepo wa dhambi ndani yao.
Kumbe sisi sote tunaweza kujifunza kitu kwa Bartimayo ambaye alimuendea Bwana kwanza kwa kuomba TOBA/KUOMBA REHEMA
kisha ndio tupeleke hitaji letu,
sio mahitaji no! nasema no!
hitaji letu liwe moja tu lenye nguvu…

ITAENDELEA…

• Usikose muendelezo wa fundisho hili mahali hapa,
• Kwa huduma ya maombezi,
0655 111149
0783 327375

UBARIKIWE.

Comments