NATAKA NIPATE KUONA * sehemu ya pili na ya pili *

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Nakusalimu mpendwa katika Jina kuu la uweza la Yesu Kristo,
Nikikuambia ;

Jina la BWANA lipewe sifa....

Dhima kubwa ya fundisho hili ni kupata kona kiroho.
Maana hakuna jambo lililo kubwa kama kuona kiroho. Yeye mwenye kuona kiroho ni mtu wapekee sana,maana hata maombi yake huwa ni yakipekee.

Leo tunajifunza kiundani kwa habari ya Bartimayo ambaye alifanikiwa kupata kuona. Nasi tunahitaji tupate kuona.

Nampenda sana huyu Bartmayo kipofu.
Yeye alijua jambo moja tu,;

Kwamba mwanadamu mwenzake hawezi kumsaidia apate kuona na ndio maana hajawahi kumuomba mwanadamu yeyote yule awenza kuona.

Yeye aligundua kwamba yupo mmoja tu mwenye kuweza kumpa KUONA ambaye ndiye BWANA YESU KRISTO PEKEE na ndio maana alimpazia sauti akiomba kuona.

Tazama katika habari hiyo vizuri kupitia kitabu cha Marko.

Marko 10:47
" Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti,alianza kupaza sauti yake,na kusema ,
Mwana wa Daudi,
Yesu,unirehemu. "

Bartimayo alishawahi kusikia habari za Yesu Kristo kabla hata ya siku hiyo. Hivyo kule kusikia habari za Yesu Kristo zilipata nafasi ndani ya Bartimayo;

Hata kutengeneza IMANI ndani ya Bartimayo. Maana kumbuka hili;

Imani chanzo chake ni kusikia,kusikia huja kwa neno la Kristo ( Warumi 10:17)

Hivyo basi IMANI ilitengenezeka kwa Bartimayo aliyekuwa ni kipofu. Imani ile ndio ilimpa ujasiri wa KUPAZA sauti yake katikati ya makutano mengi.

Uponyaji wa Bartimayo ulitegemea IMANI yake.
Na kile kilichomponya Bartimayo ni IMANI maana Bwana Yesu alipomkalibia aliiangalia IMANI wala hakumuangalia yeye alivyo.

Nasema Yesu aliiangalia IMANI ya Bartimayo,na ndio maana Yesu aliweza kumuambia kwamba ;
" Imani yako imekuponya.." Marko 10:51.

Haleluya...

Bwana Yesu akitaka kuachilia uponyaji wako,kitu cha kwanza kabisa ataangalua IMANI yako uliyonayo. Yeye hafanyi jambo nje ya kanuni yake ya IMANI.

*Bartimayo alijua siri hiyo,na ndio maana tunaona aliweza kuponywa.

Bartimayo alikuwa mjanja sana,tazama ;
Alikundua kwamba pesa zipo mifukoni mwa watu,hivyo akatega mtigo wake wa kuomba KANDO KANDO YA NJIA.

Hakuketi barabarani hovyo,bali alijua kwamba endapo ataketi kando kando ya njia itakuwa na urahisi wa kusaidiwa kuliko sehemu nyingine.

Mtu huyu alipopaza sauti yake ilikuwa sasa ni rahisi kusikiwa na Bwana Yesu,maana alikuwa kando kando ya njia mahali ambapo sauti hupaa kila kona,
Yaani sauti yake Bartimayo iliweza kumfikia Bwana Yesu kwa wepesi zaidi kuliko kama ang'eliketi barabarani.

Tunasoma
Luka 18:35
"Ikawa alipokaribia Yeriko,mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi KANDO KANDO YA NJIA,akiomba;sadaka "

Haleluya...
Jina la Bwana lisifiwe...

Walipomkataza Bartimayo kwamba anyamaze,bali yeye alizidi kupaza sauti yake akimuita Bwana.

Kama Bartimayo ang'enyamaza kwa kuwasikia wale waliomkataza,
Basi asing'epokea uponyaji wake.

Leo hii;
Wapo watu wenye kukwambia nyamaza,wakiwa na lengo baya la kuzuia uponyaji wako. Nawe usikubali kunyamaza maana hao wanaokunyamazisha kwanza hata hawana MBINGU. Si lolote si chochote hao !

Bali wewe jifunze jambo moja tu,kama lile la Bartimayo,
Jambo la KUKAZA KUMPAZIA BWANA SAUTI YAKO. Naye Bwana atakusikia maana hata katika Biblia yangu inaniambia;

"Kwa kuwa,Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka" Warumi 10:13

Sikia;
Wale waliomnyamazisha Bartimayo kwa kumkemea kwamba anyamaze,watu hao nao walikuwa ni VIPOFU.

Ni watu waliokuwa na Yesu kutokea hata huko Yeriko hali ni vipofu,hivyo hata wao hawakupata fursa/bahati ya kuona kama alivyopata Bartimayo.

Ni maombi yangu kwako;
Kwamba Mungu akupe Neema ya kumpazia sauti yako pasipo kuangalia jamii inakuonaje
Pasipo kujali maneno utakayosemewa,
Pasipo kujali matusi yoa.

*Bali wewe muite Bwana Upate kuona kiroho.

Hatuwezi kufanya huduma tukiwa vipofu,
Hatuwezi kufanya maombi tukiwa hatuoni kiroho.

Kumbe ili tuweze kumshinda shetani,kwanza ni lazima tuwe macho kiroho. Tusiwe vipofu.

Na ndio maana hata Paulo alipoijua siri hii aliwaambia;

" macho ya mioyo yenu yatiwe NURU,mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo;na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo." Waefeso 1:18.

Bartimayo anatufundisha jambo kubwa sana katika imani yetu,maana anatufundisha kuomba kwa habari ya kuona.

Bartimayo ang'eweza kumuomba Yesu,kwa habari ya umaskini wake,kwamba Mungu amuondolee umaskini,

Au ang'eweza kuomba apate pesa maana alikuwa ni maskini, mtu muhitaji,tena ni omba omba.

Lakini hayo yote hakuyaangalia,
Alichokiangalia yeye ni KUTAKA KUPATA KUONA TU.

Mungu akusaidie ili ubadilishe hata mkao wako wa maombi kwa kungangana kuomba mambo yasiyo na faida kubwa kwako.

Maana wengi huomba;
Kuolewa/Kuoa,
Kujenga au kupata kazi.N.K
Hali wao ni VIPOFU.

Maana kama mtu wa namna hii Bartimayo aliomba mbele za Bwana apate kuona tu,
Basi hata wewe waweza kumuomba Mungu akufungue macho ya rohoni upata kuona.

ITAENDELEA...

* Kwa maombezi
0655 111149,
0783 327375.

*Usikose muendelezo wa fundisho hili mahali hapa.

UBARIKIWE.

Comments