Nifanye nini ili niwe Huru kutoka katika vifungo Vya Hofu katika maisha yangu

  • Uhuru kutoka katika Hofu; Freedom from Fear na mtumishi wa MUNGU Samson Oxpel
    Utangulizi
     Matatizo mengi wanayokumbana nayo watu wengi ni matokeo ya yalewaliyo yafanya hivyo kukwama au kusonga mbele ni matokeo mazuri ya bidii na ujuzi ulioutumia kufika katika hatima yako Unapoongelea Maisha ya kiumbe yeyote anayeishi katika hii Dunia nipamoja na uhuru wake, maana Hofu ni kifungo kikubwa sana cha maisha ya mtu tena ni roho, kamili inayotenda kazi ndani ya watu, ila uhuru unaambatana na maamuzi binafsi ya kilasiku ya kila kiumbe, na huu uhuru unaanzia katika ulimwengu wa kiroho, kwakuwa ndiko maisha yanakoanzia, 

    Biblia inatufundisha nini juu ya uhuru kutoka katika hofu, 

    Mithali 1:3,I saya 35:4,Isaya 41:10,warumi 8:15 anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya. kinachowatisha watu kila inapoitwa leo ni matuko wanayoyaona au kusikia na ki-baya zaidi anaposhindwa kupambanua hayo matukio yametokea serekali gani ndipo uoga unachukuwa nafasi yake maana uwoga unaukaribisha wewe mwenyewe moyoni mwako kunapokuwa na nafasi iliyo wazi,

     Hofu ni nini?
     Ni ile hali inayomtokea mtu/kiumbe kwa ghafla baada ya kuona au kusikia jambo Fulani linalomtatiza, na kukosa maamzi juu yake, Kiumbe au mtu anapokumbana na hali tata katika maisha yake ya kila siku na akashindwa kupata mhafaka mara nyingi hofu inamjia kwakuwa hili ni tendo amalolimewekwa na Mungu ndani ya mwili kwa kusudi Fulani, ndani ya mwili kinacho ongoza hali hii ya hofu kwa watalamu wanasema ni adrenaline and the stress hormone nyongo/chungu /hakina lugha moja kila taifa au kabila lina luha yake wanavyo weza kikiita,

     Madhara ya hofu kimwili 
    Hofu inaweza kukusababishia magonywa yafuatayo Katika mwili

    1:Ugonjwa wa moyo BP(ile hali ya kusababisha moyo kufanya kazi ya zihada,


    2: Hofu inaweza kukusababisia ngozi kuwa na vichunusi/au makujanzi ya uwoga(huwezi kupata muda wa Furaha)

    3: Hofu inaweza kukusababishia kushindwa kushika mimba au kuharibu Mimba(mwili unakuwa hauko katika mood nzuri) 

    4:Hofu inaweza kukusababishia vidonda vya tumbo(huwezi kukumbuka kula) 

    5:Hofu inaweza kukusababishia kufa gazi, kwa mwili mara kwa mara(kutulia sehemu moja muda mrefu) 

    6:Hofu inaweza kukusababishia ugonjwa wa kuweweseka(kuongea mwenyewe) 

    7:Hofu inaweza kukukaushia maji mwilini ,(kutokwa na jasho sana) yapo magonjwa mengi ila haya nimachache ya mifano,

    Madhara yanayoweza kutokea katika ulimwengu wa kiroho juu ya maisha yako, Kama utaruhusu Hofu,


    A:Maisha yako yatakuwa kwa sababu Gizani- huwezi kuwa na mahusino mazuri na Mungu 


    B: Utakuwa Mtumwa- kwa sababu kila atendaye Dhambi ni mtumwa wa Dhambi Kwa kuwa hofu ni dhambi, 

    C:Utakuwa kipofu, kwa sababu macho yako ya rohoni hayatakuwa na Nuru ya kuona jambo lolote jema lililokusudiwa na Mungu, kwakuwa umekosana na Mungu 

    D:Utakuwa kilema kwa sababu huoweza kusogea hatua yeyote katika ulimwengu wa ki-roho maana Yesu ni njia na wewe njia umeshaipoteza kwa hofu

     E:Utakuwa bubu kwa sababu hutokuwa na ujasiri wowote wa kuongea katika jamii maana huyaamini hata maneno yako kama yako sawa, 

    F: Utakuwa kiziwi kwa sabubu hutoweza kusikiliza ushahuri wowote mzuri kutoka kwa mjumbe au kusikia kutoka kwa Mungu, 
    G:Utakuwa mpweke kwa sababu Mungu hakai katika hofu kwakuwa hofu Ni dhambi, na utaona kila aliyembele yako ni adui kwako kwasababu mwenye hofu anakimbia hata pasipokimbizwa,

    Hivyo hofu inaweza kuharibu mipangilio ya maisha yako yote, kwakuwa huwezi kupata uwezo wa kufikiria na kupanga lile unalolitaka katika maisha yako Muovu shetani anatumia sana Mlango wa Hofu kuwafarakanisha Watu na Mungu kuwa makini sana juu ya hofu isikubali hofu ikatawala au ikafanya makao, 

    Nini kinacho sababisha Hofu Kila mmoja wetu katika hii Dunia anamatakwa yake na anavitu anavyovitaka au kuviitaji awe navyo katika maisha, sasa yote anayoyataka mwanadamu katika hii Dunia yapo mikononi mwa watu, unaposhindwa jambo Fulani, hofu inasababishwa na kihatarishi chochote kilicho mbele yako, Ufahamu umetengeneza nafasi au mandalizi ya Hofu na unapoanza kutafakari kihatarishi kilicho mbele yako na ndiko kushindwa kwako, fahamu kuwa kihatarishi kinaumba hofu ndani yako itakayo bebea mimba ya wasiwasi ambayo matokeo yake yatazaa mtoto anayeitwa Uwoga, ambao uoga ukizidi unaweza kusababisha mauti ya kiroho na kimwili, ikikubali kubeba mimba ya wasiwasi ikisha zaliwa huyu kumtupa huwezi tena unabaki unalelea mtoto wako ambaye yeye atasababisha maisha ya wasiwasi siku zote za maisha yako, Kazi ya wasi wasi ni kukuza tatizo dogo kuwa kubwa sana, Jitahidi kufuatilia somo hili hadi mwisho utasaidika sana namna ya kuishinda Hofu na utakuwa Huru, nah ii ndiyo sababu ya mimi kuwa mbele yako na somo hili ili ni kusaidie wewe Mungu aliyekuandaa, Maandiko yanasema nini juu ya maisha yetu, Isaya 35:4 Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. Msaada pekee ili kishinda hofu Zaburi 27:1-5 Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote
    Isaya 41:10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
    warumi 8:15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba · Hii inatujulisha wazi hatutakiwi kuogopa kwa namna ya aina yeyote ile kwa namna yeyote ile hofu hatutakiwi kuipatia nafasi na siyo sehemu ya maisha yetu, Namna ya kuishinda Hofu, Hatua ya kwanza ni kukubali wewe mwenyewe kwa ihari yako kumkaribisha Mungu maishani mwako yaani kumpokea Yesu maishani, au ukubali kuzaliwa kwa mara yapili kwakuwa mwili wa asili ni wa dhambi na kila mtenda dhambi ni wa ibilisi, sasa huwezi ukasaidiwa na Mungu na Ibilisi kwakuwa hawachangamani
    Wasiyo haki wanahofu kubwa sana wanakimbia hata pasipo kukimbizwa toka huko kwa baba wa uwoga yaani ibilisi,
    Unapo kubali kuzaliwa mara ya pili yaani kuokoka Unaruhusu Mungu kukusaidia, kwa kila jambo unalolifanya, Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. 11-Timotheo 1:7 Mateso mengi wanayoyapitia watu wengi bila ya kuangalia rangi ukabila uo elimu mojawapo nihayo niliyoyataja hapa, Hapo juu ya somo, Walioishinda hofu walifanya nini
    · Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe; Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini? –zaburi 56:3-4 njia moja wapo nay a kukusaidia sana ni kumshirikisha Mungu mabo yako yote, hata ukiwa ndani ya tatizo tafuta kuwa na Mungu ndani ya Tatizo,
    Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.Mithali 3:24 hofu aichaguwi wakati wa kukutesa iwe usiku au mcha kosa ni wewe ukiruhusu ikutawale, Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. –Yeremia 1:8 kubali msaada wa Mungu Mungu wako unaye mtumaini anafahamu shida yako hitaji lako na hata sasa wewe kupata bahati hii ya kupitia hapa ni Mungu amepaandaa kwaajili yako, Kwa gharama ya bure kabisa, ili usiendelee na mateso yako, yanayosababishwa na hofu
    Mtu wa Mungu amekuwa akipokea mamia ya simu za watu wengi sana waliokuwa wanasumbuliwa na tatizo kama la kwako lakini hadi sasa wengine wengi wameshasaidiwa bure na wameifahamu kweli nayo kweli ya kristo imewaweka huru, Mungu ni Pendo,
    Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo. -1yohana 4:18 ukilinganisha gharama ya kumtumaini Mungu Na kuishi na hofu mimi ninakushahuri kubali kubadilia utakuwa mtu mwingine kabisa na utajishangaa wewe na kushangaza wengine,
    Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? –waibrania 13:5-6 vipo vishawishi vingi vinavyo weza kutusababisha kujikwaa katika tatizo au kutumbukia katika shimo kubwa la hofu, pesa,familia,ndugu,jamii, mazingira, vitu, nikuwa makini navyo kabila havijatuongoza katika hayomatatizo,
    Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. –Yohana 14:27 penye hofu hapana Amani mara nyingi wa ndoa wengi wanateseka sana katika shimo hili bila wao kujuwa duwa yangu kama wanandoa wote wangepata nafasi ya kupitia sehemu hii wangefaidika sana ninaamini hivyo,
    Ufanye nini baada ya kujifunza kata shahuri kuendelea kukosa Amani au kukubali kuipokea Amani ya kristo Yesu Mwana wa Mungu aliye hai hata sasa,
    Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. - waibrania 2:14-15
    Masomo haya yote yaliyopo hapa ni bure Yesu amesha yalipia kwaajili yako unaruhusiwa kuyatumia vile utakavyo kasoro kuyabadilishia maana, au kuongezea kisicho hitajika, Ukihitaji somo hili lote lipo pia katika mfumo wa DVD,CV,VCD CASTE Kuzipata ni rahisi kabisa wasiliana na Mtu wa Mungu Moja kwa moja kwa simu namba 0756 809209/0653 294219 Masomo mengine
    Uhuru wa kutoka katika hofu Upenyo wa kumili Siri kuu tatu za kutunza siri zako zote Nguvu ya kinywa Mauti ndani ya tumbo Nguvu ya hatua, yapo masomo mengi sana haya ni machache yale mapya mapya,

Comments