NINYI NI CHUMVI YA DUNIA * sehemu ya kwanza *

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


(Tafakari fupi)
Tunasoma hapa;

'' Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. '' Mathayo 5 : 13.

Bwana Yesu asifiwe...
Jina la Bwana liinuliwe...Oooh Haleluya...

Nami nasema na mtu mmoja mahali hapa,Ambaye ni CHUMVI ya dunia,na inawezekana kabisa ukawa ni wewe.

Siku ya leo,tunafananishwa na CHUMVI ya dunia,
Labda kabla sijaendelea mbele ni kuulize kwamba;

* Chumvi huwekwa wapi ?

Najua utakuwa na jibu lililosahihi,maana wengine hawana majibu sahihi mahali ambapo chumvi huwekwa,Wengine wasiokuwa na majibu sahhihi watanijibu hivi;

*Chumvi huwekwa katika magunia yaliyopo katika store ya chakula.
Au wengine waweza kujibu hivi;
*Chumvi huwekwa jikoni wanakoweka ghala ya chakula.

Majibu ya namna hiyo ni mazuri kabisa lakini sio majibu sahihi ya swali hilo,Maana ikiwa ning'euliza kwamba;

*Chumvi huifadhiwa wapi ?

Basi hayo yamkini yangekuwa ni majibu sahihi,bali nakuuliza kwamba chumvi huwekwa wapi?

JIBU SAHIHI.
*Chumvi huwekwa katika chakula.

Oooh!Kumbe !!

Okey;
Ikiwa chumvi huwekwa katika chakula,nasi tumefananishwa na chumvi hivyo basi nasi yatupasa kuwekwa katika chakula.
Na hapo hapo kumbuka kwamba nasi tunacho chakula,
Chakula chetu ni neno la Mungu.


Mahali hapo ndipo sisi yatupasa kuwekwa,kama vile chumvi iwekavyo katika chakula.

Sasa angalia hapa tena;

Sasa ,
Biblia inaposema sisi tu chumvi ya DUNIA inarejea kwamba sisi tu nuru ya ulimwengu uliojaa maovu.Maana neno DUNIA siyo sayari bali ni wana wote wa mataifa,sasa yatupasa tuwe NURU kwao kwa maana yule tuliyenaye ni NURU ya ulimwengu wote,yaani Bwana Yesu Kristo,Simba wa kabila la Yuda.

ITAENDELEA...

* Ni tafakari fupi ya muda huu,
lakini najua umebarikiwa kwa kiasi chake.

UBARIKIWE.

Comments