Rose Muhando asababisha patashika Mkoani Arusha.


Jeshi la polisi wilayani Karatu mkoani Arusha jana lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakidai kurudishiwa fedha zao baada ya tamasha lililoandaliwa na wachungaji wa kanisa la TAG kushidwa kufanyia baada ya mwimbaji Rose Muhando kuingia mitini.

Tamasha hilo ambalo lingefanyike jumapili iliyopita, katika uwanja wa mazingira bora, baada ya wakazi wa Karatu kutangaziwa siku mbili kabla kwa kujiandaa kutoa kiingilio kwa watu wakubwa shilingi 2500, watoto shilingi 1000 na kuna baadhi walipatiwa kadi maalum.

Baada ya mwimbaji huyo kuingia mitini wananchi waliokuwa uwanja hapo walisikika wakisema kuwa wachungaji wamewatapeli kwa kuchukua fedha zao huku mwimbaji kutoanoekana katika eneo hilo.

Wakati wananchi hao wakitaka kuwapiga wachungaji kwa madai ya kuwatapeli polisi waliigilia kati na kuanza kuwaomba wananchi kutawanyika katika eneo hilo kwani waliyekuwa wakimtarajia kufika kuonyesha tamasha hilo aonekani.

Akizungumza na wananchi mkuu wa polisi wilaya aliwataka wananchi kulinda amani kwani polisi watawafungulia jalada wachungaji na Rose Muhando aliyedaiwa kupewa shilingi milioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo.

Baada ya wananchi kutangaziwa na mkuu wa polisi walionyesha kutii kutoka nje ya uwanja lakini baada ya kufika mlango wa kuigilia walianza vurugu huku wakizuia magari ya wachungaji kutoka na pia wakirusha mawe hovyo.

Vurugu hiyo iliendelea kwa muda ambapo jeshi la polisi lilianza kutumia nguvu ya ziada kwa kutumia mabomu ya machozi kwa kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa walizigira maeneo ya uwanja huo .

Akizungumza kabla ya vurugu hizo mchungaji Joseph Msengi wa kanisa la TAG Karatu aliwatangazi wananchi waliokuwa wamekusanyika uwanjani ka ajili ya kumsubiri mwimbaji huyo alisema kuwa wachungaji walioandaa tamasha hilo na kamati hawakuwa na lengo la kuwatapeli wananchi bali walikwisha ongea na mimbaji huyo na kukubaliana.

Alisema kuwa pamoja na makubaliano yaliyofanyika baina ya Rose na wachungaji pia tayari walikwishamlipa fedha kwa ajili ya Tamasha lakini cha kushangaza mwimbaji huyo hakuwa hewani baada ya kutafutwa kwa simu yake ya hewani.

"Ndugu zangu wachungaji ni watu wa mungu hivyo hawakuwa na nia ya kuwatapeli watu na waliangdaa tamasha hilo kwa ajili ya uinjilishaji utakaofanyika Singida hivi karibuni hivyo tunaomba mtuelewe hivyo," alisema Mchungaji Msengi.

- Gazeti la Ohayoda -

Comments