somo: IKIMBIENI ZINAA






Bwana Yesu asifiwe...

Tunasoma ;
1 Wakorintho 6: 18
" Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake;ila yeye afanyaye ZINAA hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."

Nami leo hii nisipokuambia hili,nitahukumiwa ni bora nami niseme kwako mpendwa;
IKIMBIE ZINAA.

Dhambi zote ziko sawa lakini sio dhambi zote zinamatokeo sawa.
Dhambi ya wizi au dhambi ya uuaji au dhambi ya kutukana,dhambi hizo zote zinampeleka mtu motoni. Dhambi hizo zote zina uzito sawa lakini matokeo yake ni tofauti.

Neno linasema tuikimbie zinaa. Na wala neno halikusema tukimbie dhambi ya wizi,unyanganyi,uongo N.K
Neno limesema juu ya KUKIMBIA ZINAA PEKEE likijua kabisa matokeo ya zinaa ni mabaya kuliko dhambi nyingine iwayo yote hapa chini ya jua.

Nasema MATOKEO ya zinaa huaribu sana kuliko chochote kile. Ukweli ni kwamba dhambi zote ni sawa lakini zinazidiana katika matokeo yake.

Zinaa ndio dhambi ya pekee ya kuikimbia.
Sio kuikemea tu. No!
Kuikemea peke yake haitoshi Bali yeye aikemeaye anapaswa kuikimbia kabisa.

Kwa nini zinaa kuikimbia?

Jibu:
*Zinaa ni agano kati ya wawili wazinio.

Nasema ni agano kwa sababu mtu yeyote anayezini huungamana na huyo wa pili ambaye anazini naye.

Nao wote huwa mwili mmoja.
Kwa zinaa tu.

Mtu akiiba, hawezi kuungamana na yule aliyemuibia
Mtu akiua,hawezi kuungamana na yule aliyemuua.
Lakini ZINAA huunganisha wawili kuwa mwili mmoja.

Hali halisi ya leo inatisha sana!
Watu wengi wameungana na kuwa mwili mmoja kwa kutojijua.

Mungu akusaidie mpendwa kuikimbia kabisa hiyo zinaa. Uwezo wa kuikimbia upo ndani yako.
Kuikimbia sio kuishinda,
Kuishinda ni kitu kingine kabisa ambacho huwezi kuishinda wewe kwa akili zako. Bali hutaishinda kwa msaada wa Roho mtakatifu tu.

Lakini KUIKIMBIA waweza;ndio maana unaambiwa uikimbie.

Leo watu wengi wameshindwa kuikimbia tena wengine kwa kukosa maarifa utakuta wakiikemea tu .

My freind,
Zinaa haikemewi tu,
Bali zinaa ni KUIKIMBIA .

Tazama vijana wa leo walivyounganishwa na kuwa mwili mmoja.
Wakina dada wasioolewa wengine utakuta wameunganishwa na wanaume wengi.

Mfano;
Mwanamke aliyezini na wanaume labda watano hivi,katika ulimwengu wa roho,
Hao wanaume wote ni waume wa huyo mwanamke,sababu ameungamana naye.

Au,Mwanaume aliyezini na wanawake labda watano hivi,naye huyo anakuwa amewaoa hao wanawake wote nao wamekuwa mwili mmoja.

Sasa angalia hatari iliyopo;

Mabinti hutakuta hawaolewi hata kama ni wazuri vipi.
Vijana wakiume hutakuta nao hawaoi hata wawe wazuri vipi.

Kumbe !
Ukichunguza vizuri utagundua kwamba;
Hao wote wameshaoa na kuolewa kiroho na wale ambao wamezini nao.

Huo ndio ukweli uliopo sasa.

Kama mtu mmoja ataelewa ninachokifundisha hapa ,basi atakimbia zinaa.

Kuikimbia ZINAA sio kwa wasiooa au kuolewa tu , Bali ni kwa kila mtu yampasa kuikimbia.

Maandiko matakatifu leo hii yanatuambia KUIKIMBIA ZINAA. Kwa faida yetu wenyewe.

Kuikimbia zinaa maana yake nini?

Jibu;
Ni kutokuwa na mausiano ya kimapenzi na yule ambaye si mke au mume wako.
Ni kukaa mbali na mtu ambaye mwenye vishawishi vya uzinzi awe ni mchumba au mke/mume ambaye si wako.

Kuikimbia zinaa ni kujitenga na kila kishawishi kinachokufanya uzini.

Hayo yote ni namna ya kuikimbia zinaa.

Kanisa la leo lipo katika hatari hii ya kushindwa kuikimbia zinaa wakidhani kwamba Roho mtakatifu atawasaidia huku wakiwa wameikumbatia zinaa.

Yeye Roho mtakatifu ameshakusaidia kwa kukufundisha KUIKIMBIA sasa imebaki wewe kuchukua hatua ya kuanza kukimbia kweli kweli.

Dawa ya wale wote walioungamana kwa habari ya zinaa ni hii hapa;

Ukweli ni kwamba wengi tuliunganishwa na makahaba na tukawa ni mwili mmoja,wengine tukapata neema ya wokovu lakini bado wengi wakakosa wenzi wao wa kuoa au kuolea mpaka sasa.

Wengine waliounganishwa na makahaba/wauni wameoa/wameolewa lakini bado tatizo lipo pale pale katika ndoa kwamba bado nao wamefanyika kuwa makahaba na wauni katika ndoa zao,

Yaani wamekuwa hawatulii na ndoa zao kwa sababu walishaunganishwa na kahaba hapo awali kabla ya kuoa/kuolewa.

Dawa sio kuokoka pekee ingawa kuokoka ni njia ya kwanza ya kila kitu katika utakatifu.

Njia ni kufanyiwa ibada kamili ya kuvunja maagano yote uliyoyaingia katika uzinzi hapo mwanzo kwa kutokujua.

Waweza kwenda kanisani kwako na kuomba kwa mchungaji ibada ya namna hiyo,nawe utapata.

MWISHO.

UBARIKIWE.
na mtumishi Gasper madumla

Comments