Taabu na shida

Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira


''TAABU
Taabu ni nini?
Taabu –hali ya kutotulia ili jambo Fulani lifanikiwe. Ni hali ya kujitaabisha ili kitu kingine kitokee yaani unajitaabisha ili kupata maisha.

Usipotaabika kutafuta chakula ili upate chakula; watoto hawali au usipofanya kazi hupati mshahara na ada za shule za wanao. Usipojitaabisha hakuna maisha; hata usingizi wako ni wa shida na maisha yako mengi na taabu yako nyingi ni kutafuta ili upate angalau mahitaji yako ya kila siku.

Lakini MUNGU AKISHAKUOKOA na hiyo taabu; Biblia inasema ANAMPA mpenzi wake usingizi; ANAAMURU Mashariki na Magharibi TOA; Kusini na Kaskazini PELEKA. Halafu Anaendelea kusema Yeye kila Alifanyalo huyo mpenzi wake LITAKUBALIWA na LITAFANIKIWA.

MUNGU Anafika mahali ANAKUINULIA WATU Wanafanya badala yako; unaletewa Vyakula, Mavazi, Pesa, Kiwanja, n.k

UTAJUAJE KWAMBA BWANA AMEONA TAABU YAKO; DHIKI YAKO?
Utaona vitu KUBADILIKA, badala ya kupata dhiki na taabu; na mateso; unafanya kwa KUMPENDA MUNGU; Kila unalolifanya kwa UTUKUFU WA MUNGU. Hufanyi ili upate Chakula, unafanya ili MUNGU ATUKUZWE.

Wengi wanafanya kazi ili wapate chakula; lakini Biblia inasema, tufanye kazi kwa sababu MUNGU Ameagiza tufanye kazi. Biblia inasema asiyefanya kazi na asile, ina maana kuna kikundi cha kufanya kazi ili wale; hiyo taabu. Biblia husema AKATUOKOA NA TAABU ZETU ZOTE.


SHIDA
Shida ni nini?

Shida ni kitu kilichokushika na unatamani kutoka; NEEMA ipo lakini umeshikiliwa.

Mtu mwenye shida ANAHITAJI MSAADA au USAIDIZI na AKISAIDIWA hutoka katika hali hii; HAHITAJI Uponyaji. Ili uweze KUSAIDIWA Unahitaji KUFAHAMU Unahitaji Msaada wa aina gani, ni NENO LA MUNGU au UPONYAJI, KUOKOLEWA.

Mtu amepata kazi; na amesaini mkataba na atafanya kwa miaka 20 lakini hapo katikati anagundua anapunjwa na anaweza kufanya kazi mahali pengine pa mshahara mkubwa zaidi. Hata akipata kazi yenye kumpa mshahara mkubwa, hawezi kutoka kwa sababu amesaini mkataba ambao mpaka amalize kipindi chake ndipo anaweza kutoka. Akitoka atashtakiwa hivyo inabidi akae hapo huku akiugulia kwa sababu kuna kitu kimemshikilia na kumzuia asiondoke hapo.

Siku zote shida HUJA kutokana na maamuzi ya Ujinga alioufanya mtu kutokana na Uhitaji wa wakati ule au kwa tatizo la muda.

Mfano.
Binti anapewa lifti na kijana mwenye gari, baadae anakubaliana naye kutokana na Uhitaji alionao kwa wakati huo na anapewa mimba; baadaye anagundua Yule kijana hawezi kumwoa kwa sababu ana mke.
(Kuna watu wanapita kwenye Matatizo ya muda MFUPI lakini anaweka MAAMUZI ya muda mrefu, matokeo yake anateseka kwa Muda mrefu).

MSIBA
Msiba ni ile hali inayokupata inayokuondolea Tumaini. Msiba ni kuondokewa na Tumaini lako, mfano Kufukuzwa kazi, kufiwa na mzazi au mumeo au kuondokewa na kile ukipendacho; kuunguliwa na nyumba; kudhulumiwa biashara, kuibiwa gari au chochote; kuna jambo linalokusibu au linalokufika ambalo linakusababishia kurudi nyuma badala ya kusonga mbele.

Mwenye msiba anahitaji FARAJA. Faraja ni MATUMAINI; Matumaini ni nguvu ya kumtoa hapo alipo na kumwongoza kuendelea mbele. Mtu mwenye msiba anahitaji UPENDO.

Tunasoma Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii MUNGU Aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee ili kila mtu Amwaminie asipotee bali awe na Uzima wa Milele”.

Msiba unasababisha wewe kupoteza mwelekeo; Tumaini lako likipotea unapoteza mwelekeo, hivyo unahitaji UPENDO wa MUNGU KUKUSHUKIA kupitia Wanadamu WALIOUMBWA kwa MFANO na SURA YAKE ili KUKUONYESHA UPENDO.

Utaangalia kama shughuli zako zimeharibika; Unahitaji MTU mwenye UPENDO wa kukuelekeza kwamba Ulikosea pale na Pale ndipo unaweza kusimama tena na kusonga mbele.

Kama umefiwa na mume wanatokea WATU wanakutia Moyo na kukupa Faraja ya kusonga mbele.

(Maneno haya Matakatifu, Makuu Yenye HEKIMA na UFAHAMU Yataendelea)
Mwana wa MUNGU huu ni wakati wako wa KUTOKA, USIKUBALI Tena, Ni wakati wako Mwana wa MUNGU KUTOKA, ni wakati WAKO.
BWANA Akakuridhie.”

Comments