Tunaomba kwa sababu mwili ni dhaifu


Dhiki na taabu zinatufundasha kumwomba Mungu, na kama ilivyo katika maandiko matakatifu  Mathayo  26:41 Neno linasema "Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni roho i radhi lakini mwili ni dhaifu." Na katika  Zab;50:15 imeandikwa "Ukaniite siku ya mateso nitakuokoa na wewe utanitukuza."
Tunapoomba  tunatambua dhiki na taabu tulizonazo na mara nyingi tunatambua kwamba hatuwezi. Na Mungu anaweza kuruhusu tupate  dhiki ili atuonyeshe udhaifu wetu na kutukumbusha kwamba msaada wa kweli unapatikana kwake  kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi katika dhiki. Hakuna vipingamizi vitakavyoweza kututisha, kwa maana matumaini yetu hayapo katika nguvu zetu, bali yote tunayaweka mbele zake Mungu kwa njia ya  maombi. Neno la Mungu linasema hivi. Ayubu 33:29-30 "Tazama haya yote ni Mungu anayeyafanya mara mbili naam hata mara tatu kwa mtu ili kurudisha roho yake itoke shimoni."

Lk:21:36 "Basi kesheni ninyi kila wakati mkiomba ili mpate kuokoka na hayo yatakayotokea na kusimama mbele za Mwana wa Adamu."
 
Bwana wetu Yesu yeye mwenyewe alikuwa kielelezo katika kuomba, aliomba maombi ya dua pamoja na kulia sana. Yeye alilia machozi ingawa alikuwa ni mwana wa Mungu. Sisi ni zaidi tunahitaji na kutegemea maombi, tuziangalie nafsi zetu sisi wenyewe kisha tujiulize: "Mimi ni nani? Kama Yesu aliomba kwa nini mimi na wewe tusiombe?" Waebrania 5:7 "Yeye,siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu."
MUNGU awabariki sana

Comments