UMPOKEAPO VIZURI MTUMISHI WA MUNGU,UMEPOKEA MBARAKA WAKO.

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya....
Jina lake liinuliwe milele na milele...

Ipo siri ya kupokea muujiza wako pindi umpokeapo vizuri mtumishi wa Mungu.

Yapo mambo ambayo yamefichwa ndani ya mtumishi wa Mungu. Nasema mambo YAMEFICHWA kwamba hayako wazi,ambayo yapo ndani ya mtumishi wa Mungu.

Sasa ili mpaka aweze kuyaachilia kwako,inakubidi ufanye kazi ya ziada ya kuugusa moyo wa mtumishi wa Mungu.

Maana moyo wake yeye ambaye ni mtumishi ni sehemu ya uwakili wa siri za mbinguni.

Hivyo basi,
Ukimpokea mtumishi wa Mungu kwa uzuri kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akafurahia hayo mapokezi yako,ujue kwamba hukumpokea yeye kama yeye bali umempokea Mungu.

Maana yeye mtumishi ni muwakilishi wa Mungu. Hivyo umuonapo ni sawa sawa na kumuona Mungu.

Naye mtimishi huwa kama mungu mdogo tu kwako wewe uliyefungua moyo kwa kumpokea vizuri.

Mfano;

Chukulia waziri mkuu wa Tanzania aendapo katika nchi ya ugeni,atakapo kuwa huko huwakilisha serikali ya Tanzania na wala si yeye ajiwakilishie

Hivyo ikiwa watu wa ugenini hapo wakimpokea vizuri,watakuwa wameipokea vizuri serikali ya Tanzania na wala si waziri kama waziri bali wameipokea Serikali.

Alikadhalika yeye anayempokea vizuri mtumishi wa Mungu,hakumpokea mtumishi kama mtumishi tu bali amepokea serikali ya Mbinguni,amempokea Mungu.

Na hapo sasa tegemea kupokea mbaraka toka kwa mtumishi huyo. Maana si yeye bali ni Mungu ndie atakaye kubariki kwa maana ndio uliyempokea.

Tunasoma:

2 Wafalme 4 :8

" Hata ikawa siku moja,Elisha alikwenda Shunemu;na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo;

Naye akamshurutisha aje ale chakula
Ikawa kila alipoingia njia ile,huingia kula chakula"

Tazama kwa makini hilo andiko kisha utagundua kwamba mbaraka wa huyu mwanamke mshunami ulikuwa UMEFICHWA
Ndani ya ya Elisha.

Maana baada tu ya Elisha mtumishi wa Mungu kuguswa moyo na mwanamke kwa mapokezi mazuri ,
Basi tunaona sasa akibarikiwa mpaka kupitiliza.

Angalia mstari wa 16 wa andiko hili hili.
"Akasema ,panapo wakati huu mwakani UTAMKUMBATIA MWANA"

Ooh...
Haleluya...

Kumbe mtoto alikuwa amefichwa kwa Elisha. Kwamba ilibidi huyu mwanamke mshunami afanye kitu kwanza ndipo apokee muujiza wake.

Ambao huo muujiza ulikuwa tayari umeshaandaliwa kwa ajili yake.

Sasa emu jihoji kidogo....
Kwamba je umeshawahi kumpokea mtumishi wa Mungu vizuri?

La ikiwa bado ujue hupo muujiza wako katika mapokezi mazuri kwa mtumishi wa Mungu. Maana ukimpokea vyema,wampokea Mungu

Mimi pia nimepokelewa vizuri kabisa na wapendwa watenda kazi familia ya Mbwana Luhui.
Wao wamegundua siri hii ya pekee,maana katika kupokea baraka zao wamepokea.

UBARIKIWE.

Comments