VHM YAZIDI KUPASUA MAWIMBI KWA INJILI, WATU WA DINI TOFAUTI WAMPOKEA YESU KILWA

Baadhi ya wanakijiji ambao walimpa Kristo maisha yao katika huduma ya VHM.

Huduma ya The Voice of Hope ministry (VHM) yenye makao makuu yake Mwenge jijini Dar es salaam chini ya mkurugenzi wake mchungaji Peter Mitimingi wameendelea kuwasha moto wa injili vijijini na kuleta matumaini kwa watu ambao walikuwa wakiteswa chini ya vifungo vya shetani kwa kipindi kirefu.

Ambapo hivi karibuni walikuwa katika vijiji vya Kilwa mkoani Lindi ambako kama picha zinavyojionyesha watu wengi wakiwemo kutoka dini nyingine wamempa Kristo maisha yao na kufunguliwa kutoka katika matatizo mbalimbali yaliyokuwa yamewafunga.

Huduma hiyo ambayo kwakawaida haifanyi kazi mijini au sehemu zinazofikika kwa urahisi, wamekuwa wakipiga kambi katika vijiji vilivyoshindikana kwa ushirikina na mateso mbalimbali ikiwa pamoja na sehemu ambazo hazijawahi kufikiwa na injili, mpaka sasa wametembelea mikoa ya Kigoma,Mbeya, Tanga ambako walivunja makao makuu ya wachawi, Pwani kama Mkuranga, Kilwa, Msanga na sehemu nyingine nyingi.

Pia huduma hii hurusha vipindi vyake kupitia radio mbalimbali za Kikristo nchini ikiwemo WAPO RADIO 98.1 FM au kwa njia ya mtandao popote ulipo duniani, kila siku za ijumaa na jumapili kuanzia saa 3:30 usiku ambapo unaweza kusikia mambo yanayoendelea vijijini na namna huduma hiyo inavyofanya kazi zake.


Neno likasomwa.
Maombi yakafanywa.
Na sifa zikapazwa kwa aliye juu.

Ili kuvifikia vijiji vingi zaidi nchini na sehemu zote zinazoaminika kushindikana kwa ushirikina basi kwa pamoja tuwatie moyo wainjilisti hawa wa VHM kwa kuwachangia michango mbalimbali, pesa taslimu, nguo, mafuta ya taa, ya kupikia na chochote kile ambacho Mungu amekugusa ili kuwapeleka watumishi hawa.

Wanapatikana Mwenge karibu na stendi ya mabasi, ulizia hospitali ya mama Ngoma, wanatazamana na hospitali hiyo, fika hapo kwa maelezo ya kina kuhusu huduma yao, lakini pia waweza kutumia namba hii kuwasiliana nao na kufikisha mchango wako +255 713 183 939. Barikiwa
Chanzo ni blog bora ya Gospel kitaa


Comments