VIJANA WA KANISA LA LIVING WATER-KITUNDA WAFANYA SHANGWE KWA PAMOJA.




Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Kati ya jambo ambalo kanisa la leo hulikosa ni jambo la KUKAA KWA PAMOJA HUKU WAKIMEGA MKATE.

Vijana wa kanisa la Living water center;kitunda,waligundua siri hiyo. Kwamba kwa kushiriki chakula kwa pamoja huleta upendo.

Pichani hapa chini ni baadhi ya vijana walio na ufahamu wa namna ya kumega mkate kwa pamoja.

Hii ni karamu iliyopendeza sana iliyofanyika jana tar.20/10/2013.nyumbani kwa mtumishi Itatilo,maeneo ya Banana sitaki shari.

Karamu hiyo ilianzia kanisani kwa shangwe za kueleweka zikiongozwa na Mch. Devota Gwau kama aonekanavyo akiimba hapo pichani.

" Ninamshukuru Mungu ambaye aliweka msukumo wa kuwakutanisha vijana kwa pamoja tukishiriki chakula kwa pamoja. " hayo aliyasema mtumishi Itatilo (pichani aliyesimama mlefu) ambaye ndiye mbeba maono hayo.

Alikadhalika kulikuwa na mafundisho ya ukweli kutoka kwa Wachungaji,pamoja na mwinjilisti Musa.(kama waonekanavyo wakifundisha)

Mimi binafsi nilikuwepo pia nikishuhudia namna vijana wakiwajibika.

" imependeza sana kuona umoja huu wa vijana wakishiriki chakula pamoja na mafundisho,hakika wewe uliokuwepo hapa hujapoteza..." Niliweza kuwaambia hayo.

Zaidi ya yote vijana walichinja mbuzi na kuandaa chakula kizuri sana

Comments