VITA VYA KUMILIKI * sehemu ya mwisho *

Mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla 


Bwana Yesu asiwe...
Jina la Bwana lipewe sifa...

Karibu katika sehemu ya mwisho ya fundisho hili, likujialo mahali hapa kwa muda na wakati sahihi kabisa.

Lipo KUSUDI la msingi la fundisho hili kwako,mimi ninachokifahamu ni kitu kimoja tu,kwamba,lipo jambo moja kati ya mambo mengi kupitia somo hili ambalo litakusaidia katika vita ya kumiliki mali zako.

Kumiliki ni haki yako,
Kumiliki kumeumbwa kwa ajili yako,
Kumiliki kuna kutambulisha uwepo wako katika dunia hii.

Sasa huwezi ukamiliki chochote kile chini ya jua hili kiurahisi rahisi pasipo kuwapo na VITA.

Hapo ndipo kuna KUSHINDA au KUSHINDWA katika vita hivyo,kutegemea na upiganavyo.

Leo nataka nikutangazie kwamba ushindi wa vita hivi ni kukutana na Yesu. Kuji-position vizuri kwake,huku ukiongozwa na Roho mtakatifu.

Kuwa mkristo maana yake ni kuwa mmiliki,

Ukiona humiliki,ujue lipo tatizo kwako.
Yaani umepigwa katika vita hivi.

Bwana yupo hapa kukueleza kwamba UTASHINDA TU wala usiwaogope hao waliokushinda.

Kumbuka nilikupa hatua takribani tatu za ushindi dhidi ya adui yako.(pitia sehemu zote zilizopita)

Kumiliki sio tu kuwa na magari,
Kumiliki sio tu kuwa na majumba,
Kumiliki sio tu kuwa na viwanja,
Kumiliki sio tu kuwa na pesa nyingi.

Bali kumiliki ni zaidi ya mambo hayo yote.
Maana waweza kuwa na hayo yote na ukawa bado hujawahi kumiliki.

Usishangae nikikuambia hivyo,
Maana KUMILIKI ni utiisho wa ki-Ungu.
Ni hali ya kuwa na sauti ya utiisho,kwamba vyote kuwa chini yako.

Kumiliki ni kutotawaliwa,ni kutoka kabisa MISRI.

Wapo wengi leo hii wenye mali na wakidhani wamemiliki tayari,kumbe hawajawahi hata kumiliki.
Maana yule mwenye mali kisha ile mali ikiwa si yake bali huitumia tu,mtu huyo bado hajamiliki.
Au
Yule ambaye yupo Misri naye hajamiliki kabisa hata kama anaonekana na mali nyingi bali hizo mali zote ni za wamisri tu wala sio zake.

Misri ya leo ni utumwa chini ya ibilisi,
Ibilisi ndio mwenye mali zake kwa yule aliyekuwa Misri. Kwa maana mtu awapo na mali kisha yu chini ya ibilisi,
Hizo mali ni si zake bali ni za ibilisi.

*Maana mmiliki ni yule mwenye sauti juu ya kile anachokimiliki.

Jambo moja analoanza kumiliki mtu wa Mungu ni ARDHI.

Kumiliki ardhi ni vita. Sio rahisi rahisi kama wengine wadhaniavyo.
Na ndio maana ninakuambia habari hii mapema kabisa kwamba ipo VITA VYA KUMILIKI.

Wakristo wengi si wamiliki hata leo,hii inatupa picha kwamba wameshindwa kupigana vita.

Nami nakuambia kwamba umepewa kumiliki.
Maana Yeye Bwana Yesu alifanyika maskini ili tuwe matajiri.

Mungu yuko upande wako,tatizo liko kwako mwenyewe.

Hiyo hali uliyonayo sio maisha halisi aliyokupangia Bwana kuishi. Bali umeshindwa kujua haki yako.

Nilikuambia ili umiliki mali zako zote ni lazima ;
* uhakikishe mausiano yako na Mungu yako sawa.
* usikubali dhambi ikae katika kituo chako
* udumu katika maombi

Hayo mambo matatu sio mambo ya kawaida kawaida bali ni principles ambazo wana wa Mungu walizitumia na wakafanikiwa.

Mfano mdogo tu,
Mtazame maisha ya IBRAHIMU.

Tazama pia Mfalme SULEIMANI.
tazama maisha ya DAUDI. NK

wote hao utagundua waliishi ndani ya mambo hayo matatu.

Hivyo,mtu wa Mungu jaribu hayo kisha uone kama hujashinda vita vya kumiliki.

MWISHO.
* Mawasiliano yangu ni ;
0655 111149
0783 327375.

UBARIKIWE.

Comments