VITA VYA KUMILIKI * sehemu ya nne*

na Mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Haleluya….
Mtu mmoja ampe utukufu Bwana….

Karibu katika mfululizo wa fundisho hili;
Kumbuka kwamba; nilikuambia sisi tu warithi wa mali zote tulizopewa na Bwana Mungu chini ya jua hili,

Lakini cha kushangaza tumeshindwa kabisa kuzimiliki mali zetu.Basi ikiwa ndio hivyo,ya kwamba tumeshindwa kumiliki UTAJIRI wa Baba yetu,inatuonesha kwamba tumeshindwa kupigana vita vya kumiliki,dhidi ya ufalme wa giza katika ulimwengu wa roho.

Kwamba kile ulichopewa ukimiliki kwa ajili ya kumuinulia sifa Mungu wetu,Adui huinuka na kuja na kuharibu,
ili usimiliki chochote kile na kwamba uwe mali yake shetani.

Hivyo jinsi ulivyo ni kwa sababu umeshindwa kupigana Vita vya kumiliki mali zako hata zimechukuliwa ungali U macho ukizitazama,na umebakia ni maskini kama vile sio mtoto wa Mungu.
Nami nasema;

Hiyo roho ya ibilisi ya iliyochukua mali zako,ishindwe kwa jina la Yesu,..
Nakutangazia urejesho wako,na huu ndio mwaka wako wa kumiliki yale yote yaliyoibiwa,

Haijalishi muda gani uliobakia katika kipindi hiki cha mwaka,maana Mungu wetu yupo kazini sasa kukurejeshea mali zako zote.
Amini nawe utapokea katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti…..(sema AMINA)

-Nilikuambia kwamba zipo mbinu kadhaa za ushindi kwa habari ya vita vya kumiliki.
Na tulifanikiwa kuangalia mbinu/njia mbili zikupasazo kushinda kumiliki mali zako,nazo ni;
01. 01.HAKIKISHA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU YAKO SAWA.
02. USIKUBALI DHAMBI IKAE KATIKA KITUO CHAKO.

Katika njia hiyo ya pili ambayo leo tunaendelea nayo kwa ufupi,
ni kwamba dhambi ndio kiini cha kushindwa kumiliki.

Na ndio maana ninasisitiza kwamba pindi ufanyapo dhambi basi tubu saa ile ile,wala usikubali dhambi izaye matunda yake maana matunda ya dhambi ni mauti.

Hapo utagundua kwamba Wakristo wengi wameziruhusu dhambi kukua hata kuzaa mauti,nao hapo hapo wanataka kumiliki mali zao hali ni wachafu mbele za Bwana.

Ngoja nikupe mfano kidogo,ili ujue jinsi mtu anavyoizoelea dhambi.Maana utakuta mtu afanyapo dhambi pasipo kuitubia kiukwelii,ujikuta ufanya tena nyingine,maana dhambi moja huzaa nyingine kisha mauti.

MFANO;
*Mtu mmoja mtafiti,alijaribu kuyapima matendo ya NURU na matendo ya GIZA,
kisha akajaribu kuona jinsi gani mtu afanyapo dhambi kwa mara ya kwanza kwamba hujutia sana,lakini akajaribu kuona tena kama mtu huyo asipoitubia dhambi hiyo hufuata nini.?

Mtafiti akakusanya watu mbali mbali wa kila lika,watoto,vijana hata wazee,na watu wa jinsia zote.
Akawaandalia karamu nzuri ya pamoja.Alihakikisha kila aina ya kinywaji na chakula kipo katika karamu hiyo.

Kisha watu wote walionekana wametulia katika meza zao za chakula na vinywaji wakizungumza kwa sauti ya upole huku kamziki kadogo kalikuwa kanaimba,
kwa ukweli kulikuwa na utulivu wa namna yake mzuri, maana hata watu wote walipendeza na kuketi kwa heshima ya namna yake.

Sasa mtafiti huyu akaanza kuwafanyia majaribio;
*Gafla akakata umeme,pakawa giza ukumbi wote kwa dakika tano.
Katika dakika tano zile,
hapakuwa na mtu aliyezungumza na mwenzake hata mmoja,maana GIZA liliingia kwa mara ya kwanza hivyo kila mmoja aliogopa giza,pakawa kimya kabisa.

*Zilipofika dakika nyingine tano(yaani dakika ya kumi ya uwepo wa giza)-Gafla watu wakaanza kuzungumza kwa upole,baadaye wakazungumza kama hapo awali.

*Zilipofika dakika tano nyingine(yaani dakika ya kumi na tano ya uwepo wa giza)-Watu wakazidi kuongea na wengine hata kuimba wao wenyewe kwa sauti kubwa tu.
Zikasikika sauti kama za watu walevi hivi wakiimba huku wakishangilia.

GAFLA AKAWASHA TAA.
“PAA!” TAA IKAWAKA

*Oooh !
akakuta mambo ya ajabu kwa wale watu waliokuwa wakionekana ni wastaharabu waliopendeza.
Maana kwanza alikuta watu wametawanyika wakiwa wengine wamekwenda kuketi katika meza ambazo sio za kwao walizopangiwa kuketi,

Wengine walikuwa wamesimama juu ya meza,
Wengine wamekumbatiana,
Wengine aliwakuta wamekunywa chakali! Tena hawa ndio waliokuwa hawatumii kilevi hapo mwanzo.

Jambo alilojifunza baada ya zoezi hilo ni hili;

*Palipokuwepo na NURU watu waliogopa kufanya maovu hivyo wakajizuia kwa kitambo tu kimwili lakini roho zao zilikuwa hazijajizuia,bali zilikuwa zikiwaka tamaa.

*GIZA lilipoingia mara ya kwanza watu waliogopa giza pakawa na ukimya kabisa,lakini lilipoendelea kuwatawala wakalizoea giza,wakaona ni kitu cha kawaida ni sawa sawa na dhambi mtu afanyapo mara ya kwanza huogopa,
tena hata kujutia lakini asipotubu kwa kung’oa mizizi ya dhambi hiyo,ujikuta kuizoea na kuona ni jambo la kawaida.

Sasa leo,
Ninakuambia usikubali dhambi ikuzoee,maana kamwe hutaweza kumiliki wala kamwe huwezi kuishi maisha ya ushindi.

*Tubu upesi,ili Bwana awe upande wako pindi upiganapo katika vita hivi vya kumiliki…

ITAENDELEA…

*Tafadhali ninakusihi USIKOSE KABISA muendelezo wa fundisho hili mahali hapa.
Kwa maombezi na kusalimiana mawasiliano yangu ni,
0655-111149,
0783-327375.

UBARIKIWE.

Comments