VITA VYA KUMILIKI * sehemu ya tano *



Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya...

Karibu tena katika muendelezo wa fundisho hili mahali hapa. Kwa maana fundisho hili limekuwa baraka sana kwa watu wengi.

Sababu linatufundisha njia sahihi za kumiliki mali zetu ambazo zilichukuliwa na adui yetu.

Leo nazungumza na mtu mmoja mahili hapa ambaye ameibiwa umiliki wake pasipo kujijua au hata kujijua.


Awali ya yote
Kumbuka mahali tulipokuwa tumeishia. Tulikuwa tukijifunza njia ya pili ya kupigana vita hivi vya ushindi,nayo hiyo njia ilikuwa ni:

*usikubali dhambi ikae katika kituo chako.
(Pitia fundisho lililopita kwa notes zaidi)

Leo tuangalie njia au mbinu ya tatu tuitumiayo kushinda vita vya kumiliki,nayo ni:

03.KUDUMU KATIKA MAOMBI.

Njia hii ni njia nzuri sana kwa yule mwenye kupigania umiliki wake.
Maombi ni silaha nzuri sana imuwezeshayo mtu mmoja kushinda maadui hata elfu moja kwa wakati mmoja.

Kuomba kunaendana na kushukuru,kusifu na kuabudu.

Sasa tuangalie Biblia inasemaje katika njia hii.
Tunasoma ,

2 Nyakati 20:21-22

" Naye alipokwisha kufanya shauri na watu,akaweka wale watakao mwimbia Bwana na kumsifu katika uzuri wa utakatifu,wakitoka mbele ya jeshi,na kusema

Mshukuruni BWANA ;kwa maana fadhili zake ni za milele.

Nao walipoanza kuimba na kusifu,BWANA akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu,na wa mlima Seiri,

Waliokuja juu ya Yuda nao wakapigwa "

Hiyo ni habari ya wana wa Yuda. Ambao waliinukiwa na mataifa matatu yaani hayo mataifa yalikuwa ni ;

*Wana wa Moabu.
*Wana wa Amoni,pamoja na baadhi ya Wameuni.

Biblia inatuambia kwamba,hawa wana wa Israeli/Yuda waliposikia habiri ya vita hivyo,wakamtafuta Bwana kabla ya chochote kile.

Maana walijua siri kwamba mwenye vita ni Bwana wao na kwa huyo ndipo ushindi hupo hapo.

Njia mojawapo ya ushindi juu ya mataifa yale yaliyoinuka juu yao ilikuwa ni MAOMBI YENYE KUSIFU NA KUSHUKURU KATIKA BWANA.

Tazama huo mstari wa 21( 2 Nyakati 20: 21)
Biblia yangu inasema kwamba hao wana wa Mungu wakawatanguliza mbele wana wa sifa na kumuinua Bwana kumsifu.

Hivyo kazi yao ilikuwa ni moja tu,ya kumuinua Bwana hata pale katika hali ngumu ya namna hiyo ya vita.

Sasa sijui kwako unapitia hali ya namna gani,iwe ni magumu ya namna yoyote,
Iwe ni milima yoyote ile,
Iwe ni shida yoyote ile au hata vita upitiayo,

Lakini kwa magumu hayo yote ili upate mpenyo wako,basi huna budi kumuinua Bwana kwanza kwa kumuabudu. Maana ni Yeye Mungu ndiye atakushindia pindi umuinuapo.

Katika akili ya kawaida unaweza usielewe au unaweza kutokubaliana na akili yako,kwamba wapo watu waliopanga kukupiga katika vita waliyopanga wao wenyewe.

Kisha wewe ndio unaanza kumuimbia Mungu na kumsifu Mungu.kama hali ilivyo kwa wana wa Israeli pale walipoinukiwa na mataifa hayo kwa vita.

Lakini wao wakawatanguliza watu wa KUOMBA tu kwa kumuinua Bwana hali maadui zao wanakuja na silaha mikononi mwao.

Na ndio maana ninakuambia hili ni jambo ambalo huwezi kulielewa kwa akili za kawaida.

Tazama namna maombi yalivyojibu hata wana wa Yuda wakapata mpenyo na kushinda kumiliki mali zao na hata mali za maadui zao baada ya Mungu kuwashindia.

Kudumu katika maombi ni jambo liletalo ushindi tupiganapo vita hii ya kumiliki.

Wana wa Yuda walidumu katika kuomba kwa sababu tunaona pale vita ilipotokea wao wakazidi kumuinua Bwana kwa kumshukuru kwa kusema ;

" Mshukuruni Bwana kwa maana fadhili zake ni za milele."

Ilikuwa sio jambo jepesi kwamba adui yako anakujia na panga mbele yako akuangamize kisha wewe uanze kumuimbia Bwana Mungu pasipo kuwepo na silaha yoyote ile ya kibinadamu.

Lakini kumbe vita ijapo kwako . Wewe endelea kudumu katika maombi na Bwana Yeye atakushindia vita hiyo nawe utaweza kumiliki.

Sababu Biblia inatuambia kwamba vita si vya kwetu bali ni vya Bwana.

Kudumu katika maombi kunakuwezesha kupiganiwa na Bwana kwamba wale adui zako wajapokujia basi Bwana atakushindia.

ITAENDELEA...
Kwa maombezi ;
0655 111149
0783 327375.

*Usikose muendelezo wa fundisho hili.

UBARIKIWE.

Comments