VITA VYA KUMILIKI * sehemu ya tatu *

Na mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Nakusalimu katika jina la Bwana,ndugu mpendwa…
Haleluya…

Karibu tuendelee na fundisho hili zuri mahali hapa,
likiwa na lengo kubwa la kukuonesha ya kwamba kuwa mkristo pekee haitoshi bali yakupasa umiliki,maana yeye ambaye ni mkristo ni mrithi sawa sawa na ahadi;

" Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. " Wagaratia 4 : 29

Tulikuwa tumejifunza juu ya hatua moja ya kupigana vita ikupayo ushindi wa kumiliki mali zako,njia hiyo ya kwanza tuliojifunza ilikuwa ni ;
01.Hakikisha mahusiano yako na Mungu wako sawa.

Leo tunajifunza njia ya pili ya ushindi pindi upiganapo vita vya kumiliki,nayo ni;

02.USIKUBALI DHAMBI IKAYE KATIKA KITUO CHAKO.

Kati ya njia au mbinu ya msingi ya kushinda vita ya kumiliki ni kuhakikisha hautawaliwi na dhambi,kwa sababu pindi dhambi iwapo inazuia mawasiliano yako na Mungu,Biblia inasema;

'' lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. '' Isaya 59:2

Hii ni sawa na mfano wa mwanajeshi aliyekuwepo vitani pasipo mawasiliano na mkuu wake ambaye kwa huyo ndiko silaha zinatoka,
Dhambi huficha mawasiliano,

Mbinu moja ya ushindi pindi mwanajeshi awapo vitani ni mawasiliano mazuri na wakuu wake,lakini pasipo kuwepo mawasiliano mazuri basi tegemea kushindwa kwa anguko kubwa sana.

Ninanapokuambia kuwa USIKUBALI DHAMBI IKAYE KATIKA KITUO CHAKO nina maanisha kuwa,kituo chako kiwe safi muda wote.
Tazama andiko hili ;

'' kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha. '' Kumbukumbu la torati 23 :14

Mungu hatakuacha katika vita ya kumiliki mali zako,lakini hapa tunatahadharishwa kwamba Yeye Bwana Mungu akiona kitu kisichokuwa kisafi katika kituo chako,atageuka na kukuacha upigwe na adui zako,

Wayahudi kipindi kile walikuwa wakijitahidi sana kusafisha vituo vyao vya vita ili Mungu akiwatembelea akute ni visafi kiasi kwamba anaweza sasa kuongea nao na kuwashindia vita.

KITUO chako cha leo ni moyo wako,
Kwa huo moyo unapaswa kuwa safi,pindi unapodai haki yako ya kumiliki iliyoibiwa,tegemea Bwana atakujia katika kituo chako/Moyo wako yaani si moyo tu kama moyo bali ni roho yako iwe safi.

Biblia inatuambia ipo sehemu moja tu ya mwanadamu ambayo inampasa kuilinda sana kuliko vitu vyoote alivyo navyo,sehemu hiyo ni MOYO (Mithali 4 :23)

Ili uwe na mahusiano mazuri na Bwana Mungu basi hauna budi kufuta na kusafisha dhambi zote katika kituo chako kwa jina la Yesu Kristo,ili ajapo akute kisafi ,ukaishinde vita,na ukawe mmiliki halali wa mali zako.

Ukweli ni kwamba sisi sio maskini hata kidogo,bali dhambi zetu zimeuficha uso wa Mungu hata sasa tukawa maskini kwa sababu ya dhambi zetu.
maana ;

*Umaskini ni dalili ya dhambi.

tazama akina Adamu na Hawa,
Walikuwa na kila kitu katika bustani ya EDENI.Lakini dhambi ilipoingia tu wakawa mbali na uso wa Mungu na kuanza kuwa wahitaji wa kila kitu,wakati kila kiltu kilikuwa bustanini kabla ya dhambi kuingia.

Ili ushindi uje kwako,basi jitahidi sana kuwa mtu wa toba kila dakika,saa,siku na kila muda pasipo kujihesabia haki,nawe utamiliki mali zako zilizoibiwa na watu/ufamle wa giza....

ITAENDELEA....
Usikose muendelezo wa fundisho hili mahali hapa,
*Kwa maombezi na kusalimiana,mawasiliano yangu;
0655-111149
0783-327375

UBARIKIWE.

Comments