Mwimbaji wa gospel nchini Steven Mwikwabe anatarajia kuzindua album yake
ya tatu iitwayo "Wewe wajua" jumapili hii katika kituo cha ushauri wa
kibiblia na maombezi (BCIC) Mbagala maji matitu akisindikizwa na
waimbaji kama Beatrice Mwaipaja, Lembo Emmanuel Junior, Tina Marego,
Atosha Kisava pamoja na waimbaji wengine wakiwemo wenyeji.
Comments