WATEULE WA MUNGU TUKO VITANI





Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula wa Maisha ya ushindi ministry

Vita  sio   lelemama.Ni kufa  na  kupona.Tena  vita  vyetu sisi “si juu  ya  damu na  nyama bali  ni  juu  ya  falme  na  mamlaka  juu  ya  wakuu wa  giza  hili, juu  ya  majeshi  ya  pepo  wabaya  katika ulimwengu wa  roho “{Wafeso 6:12}.Vita  kali
Kuna  watu  wengi  wanaokata  shauri  kumpokea  YESU(wanaokoka).Kweli wanakuwa  wamepanga  hasa  kwenda  mbinguni.Wanaimba nyimbo  za  sifa zionyeshazo hamu  ya  kuwa YESU  arudi upesi.Huaanza kushuhudia kwa  nguvu zote,hata kwa  kufunga  na  kuomba na  machozi.Wanakuwa wameanza Vita wanakutana  na  vikwazo na  shida  njiani wanapigana  sana.Wengi wanashinda lakini wengine  wengi wanachoka  polepole  na  wanaachwa  na  wenzao  wanapobaki nyuma  peke,  yao adui anakuja  na  kuwazunguka  na  kuwateka  mateka
Pengine umekwisha waona  hawa  waliorudi nyuma  wakaanguka.Usidhani kuwa  mtu anayekata shaurikumwacha YESU huwa wanajishtukia wameanguka kushindwa huku ni  sawa na  usingizi.ukilala kitandani unakuwa ukiwaza mambo  mengi  au  unazungumza na mwenzako. La ajabu ni kwamba hujui unasinzia saa ngapi na  dakika ngapi na ukaacha kusikia hata  kama  utalala ukiangalia saa unayezungumza naye anakuja  kugundua kuwa anazungumza peke yake tu wewe unatambua kuwa ulikuwaumesinzia wakati unapoamka, 
ndivyo ilivyo kwa  maisha ya kiroho. Mtu hawezi  kujua lini hasa alipoanguka
Anakwenda  taratibu hatua  kwa  hatua akisogea  nyuma na baadaye anajikuta ameanguka amekwishatekwa na maadui

Maadui wetu wana  nguvu sana .Maadui hasa ni watatu

-Adui wa kwanza ni  shetani: ni kawaida watu wa MUNGU kusema shetani ameshindwa Haleluya’’.Ni kweli Lakini hakufa ili kwa vile ameshindwa na YESU amri jeshi mkuu amekimbia na kuzungukazunguka akikuta mtu amebaki  nyuma na amechoka basi anamteka tu Yeye shetani kama simba angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ammeze {1 petro 5:8}
Shetani siyo mvivu anashughulika  usiku na  mchana akiwatafuta watu wa MUNGU ili aende nao jehanamu Tusije tukasahau hili,
 Biblia anasema kwamba tukeshe {tukae macho } ili tumpinge atakapokuja kutushambulia .Tuwe tumevaa silaha zote za MUNGU ili tupate kujikinga na kuzipinga hila zake {Wafeso 6:11}

-Adui  wa pili ni mwili: Biblia inasema “mwili”, ina maana ya ule utu wa kale, ile hali ya dhambi tuliyonayo kwa asili.mwili hupambana na roho zetu Tena mwili huu {flesh} ni wa mauti.Paulo anaeleza vizuri jambo hili katika {Warumi 7:15-24}
Upo uwezekano wa kuishi kufuatana na mapenzi ya mwili k.m kutamani kuona wivu kudanganya ili kukwepa hatari kutotii,n.k mwili upo karibu sana nasi tena ni sehemu yetu.Ni adui wa hatari sana tumchunge

-Adui wa tatu ni ulimwengu
Ulimwengu  ni mambo yote yaliyo kinyume na MUNGU mambo ya dunia k.m miundo ya jamii,siasa,mazingira,watu n.k
Ulimwengu  una  dhiki BWANA hakutoa ahadi kwamba hatutapata dhiki {1thes.3:3,4} Dhiki ni sehemu ya ukristo wetu Lakini ni vigumu kuvumilia dhiki kama njaa,uchi,ugongwa na uchungu wa kifo.Hata hivyo ugumu huu siyo  kisingizio cha kushindwa kwetu.
Ulimwengu hauna dhiki tu.Una raha pia.Raha nayo inaweza kabisa kutufanya tumwache BWANA kwa mfano Dema, ambaye Paulo alimwita mtendakazi pamoja nami alikaa  na  Paulo muda mrefu akihubiri .Lakini Paulo alipo fungwa gerezani tunashangaa tukiona anamwandikia mpendwa wake timotheo kwa masikitiko akisema “DEMA aliniacha ,akiupenda ulimwengu huu wa sasa {2timotheo 4:10}
Alikwepa dhiki akakimbia raha wenzetu wengi wameangushwa na raha hizi kama mali,wapenzi, vyeo n.k wanasahau kabisa wito waliloitwa na BWANA
Hata hivyo maadui hawa wasitutishe.tunaye YESU,BWANA wa MAJESHI yule mwanamke aliyeitwa Hana, alishuhudia akisema “Wala hakuna mwamba kama MUNGU wetu “{1samweli 2:22} tunaweza  kujiunga naye tukiimba
Moyo wangu wamshangilia BWANA
Pembe  yangu imetukuka katika BWANA
Kinywa  changu kimepanuka juu  ya adui zangu
Kwa kuwa naufurahia wokovo wako {1samweli 2:1}
Tujue tuko. vitani vita vya kiroho, vya imani. tusiwe kama wajinga tukajisahau
Ndiyo maana Paulo ,akijaa ROHO MTAKATIFU anatwambia ,”kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU mpate kuweza kushindana siku ya uovu ,mkiisha kuyatimiza yote ,kusimama “{efeso 6:13}
Katika sehemu inayifuata, tujaribu kuona silaha hizi za MUNGU zitakazotuwezesha kumshinda  shetani, mwili na ulimwengu, na kukua kiroho.
MUNGU awabariki sana ndugu wote.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
         Maisha ya ushindi ministry.
               

Comments