Yaliyotokea katika mkutano wa injili T AG Ndembela , Tukuyu

Ni katika kanisa la T.A.G Ndembela Kwa Mchungaji Kinene. Ambapo Mchungaji Thobias Tambikeni wa Kanisa la T.A.G forest alihudumu katika mkutano huo pamoja na hayo pia aliongoza ibaada ya kusifu na kuabudu ambapo roho mtakatifu alijidhirisha kwa watu. Katika ibaada ya asubuhi Mchungaji Thobias alifundisha somo lenye kichwa kinachosema "USHINDI ULIO MBELE YAKO KILA ATAKAYE ONA AU KUSIKIA ATAMTUKUZA MUNGU WA MBINGU NA NCHI" Ambapo maandiko ya somo yalitoka katika kitabu cha UFUNUO 3:7-13 Ambapo biblia inasema "Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadefia andika;Haya ndio anenayo yeye aliye mtakatifu wa kweli,aliye na ufunguo wa Daudi,Yeye mwenye kufungua ufunguo wala hapana afungaye.Nayajua matendo yako.Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako ambao hapana awezaye kuufunga,kwa kuwa unazo nguvu kidogo,nawe umelitunza neneo langu wala hukulikana jina langu.Tazama nakupa walio wasinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo.Tazama nitawatanya waje kukusujudu mbele ya miguu yako na kujua ya kuwa nimekupenda .kwa kuwa umelishika neneo la subira yangu ,mimi nami nitakulinda ,utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote.kuwajaribu wakaao juu ya nchi . Naja upesi shika sana ulicho nacho asije mtu akakitwaa taji yako .Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu ,wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wa Yerusalemu mpya,ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu na jina langu mwenyewe lile jipya. Yeye aliye na sikio na alisililize neno hilo ambalo roho ayaambia makanisa. i KWA MSAADA WA MAOMBI USHAURI WA KIROHO WASILINA NA MCHUNGAJI THOBIAS TAMBIKENI 0756-929510

Comments