YESU KRISTO ni nani? (sehemu ya 2)





inaendelea...........

SABABU ZA KUAMINI
Ufufuo ni msingi katika imani ya Mkristo. Kuna sababu kadha wa kadha ambazo wale wanaosoma kuhusu ufufuo wanaamini kuwa ufufuo ulitendeka:
KUTABIRIWA: Kwanza, Yesu alitabiri habari za kifo chake na ufufuo na zikatendeka kadri na jinsi alivyotabiri (
Luka 18:31-33).

KABURI LILIYO WAZI: La pili, ufufuo ni kielelezo cha pekee cha kaburi lililo wazi. Ukisoma Biblia kwa makini, utaona kwamba kaburi ambalo walilolaza mwili wa Yesu lililindwa barabara na wanajeshi wa Kirumi na pia lilizibwa na jiwe. Kama Yesu hakuwa amekufa, bali alikuwa amedhoofika - kama wengine walivyosema, walinzi na jiwe pia lingezuia juhudi za kuhepa au kusaidiwa na wafuasi wake. Maadui wa Yesu hawangechukua mwili kwa sababu kukosekana kwa mwili huo pale kaburini ingalitia nguvu imani juu ya kufufuka kwake.
KUONANA KIBINAFSI: La tatu, ufufuo ni kielelezo cha kipekee cha kuonekana kwa Yesu na wafuasi wake. Baada ya kufufuka kwake, Yesu alionekana mara zisizopungua 10 na wale waliomjua na pia kwa watu 500 waliokusanyika pamoja. Bwana aliwathibitishia kwamba kuonekana kwake mara tatu hizikuwa ndoto. Alikula na kuongea nao na walimgusa (
1 Yohana 1 :1).

KUZALIWA KWA KANISA: La nne, ufufuo ni sababu ya pekee ya kueleza sababu ya kanisa kuanzwa. Kanisa la Kristo ni chama kikubwa kuliko vingine vilivyoko sasa pia vilivyowahi kuwepo katika historia ya ulimwengu. Zaidi ya nusu ya mahubiri ya kwanza yaliyohubiriwa yalikuwa kuhusu ufufuo (
Matendo 2:14-36). Hakika kanisa la kwanza lilijua kwamba jambo hili litakuwa msingi wa ujumbe wake. Maadui wa Yesu wangelikomesha wakati wowote kwa kuutoa mwili wa Kristo.

MAISHA YALIYOBADILISHWA:
La tano, ufufuo ni kielelezo cha kipekee cha maisha yaliyobadilishwa ya wafuasi wake. Walimwacha kabla ya kufufuka kwake; baada ya kifo chake walikufa moyo na kuogopa. Hawakutarajia kwamba Yesu atafufuka kutoka wafu (
Luka 24 :1-11).

Lakini baada ya kufufuka kwake na mambo waliyopata wakati wa Pentekote, hawa waliokufa moyo, waliopoteza hamu, wanaume kwa wanawake, walibadilishwa na nguvu za Kristo aliyefufuka. Katika jina lake, walifanya kishindo kikubwa duniani. Wengi walipoteza maisha yao kwa ajili ya imani yao; wengine waliudhiwa vibaya. Matendo yao ya ujasiri hayana kielelezo kamili isipokuwa kwamba waliamini Yesu Kristo kweli alifufuka kutoka wafu - jambo lililowatosha hata kukubali kufa kwa ajili yake.

Katika miaka 40 ya kufanya kazi na wataalamu wa vyuo vikuu ulimwenguni, sijawahi kukutana na mmoja ambaye ameyasoma mathibitisho ya dhati kuonyesha uungu wa Yesu wa Nazareti na pia kufufuka kwake, ambaye hakukubali kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, Mesiya aliyeahidiwa. Ijapokuwa wachache hawaamini, wanasema kwa moyo wa kweli, "Sijachukua muda wowote kusoma Biblia au kuangalia mambo katika kihistoria yalitotendeka katika maisha ya Kristo."
BWANA ANAYEISHI:  Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, wanafuasi wake wa kweli hawafuati tu orodha za mwanzilishi aliyekufa, bali wanauhusiano wa karibu na wakibinafsi na bwana aliyehai. Yesu Kristo yuhai leo na anabariki na kuimarisha maisha ya wote wanaomwamini na kumtii. Katika enzi zote, wengi wamedhihirisha kufa kwake Yesu Kristo, kati yao wakiwa watu waliotenda makuu ulimwenguni.

Mwanafizikia na mwanafalsafa wa Kifaransa Blaise Pascal alisema jinsi mwanadamu anavyomhitaji Yesu aliposema, "Kuna pengo katika Luka 18:31-33
Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyanyiwa dhihaka; atatendewa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.

 
1 Yohana 1 :1
Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno ya uzima.

Matendo 2:14-36
Lakini Petro akasimama pamoja na wale kmi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. Sivyo mnavyodhank; watu hawa hawakuelewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli. Itakuwa siku ya mwisho, asema Mungu, nitamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake. Roho yangu, nao watatabiri. Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.
Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikiwe nao. Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wangu wa mkono wa kuume, nisitikisike. Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. Umenijulisha njia za uzima. Utanijaza furaha kwa uso wako. Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi. Yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu. Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. Basi yeye, akiishi kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa kuume. Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yaho. Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amefanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo.


Luka 24 :1-11
Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta; nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Wakayakumbuka maneno yake. Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote. Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao; hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo.
MUNGU akubariki sana  na kama hujaokoka muda wa kufanya hivyo ni leo. mpokee BWANA YESU naye atakuokoa, utakuwa huru tena utakuwa na ulinzi wa MUNGU mbali na wachawi na majini.


Comments