YESU KRISTO ni nani?



Watu wake YESU wakimwomba MUNGU


YESU KRISTO wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako hapa duniani na ya milele yanaguswa na jibu lako kwa swali hili?


Ni...
  • Mtu wa ajabu kupita watu wote katika nyakati zote?
  • Nani aliyejitokeza kuwa mtu mashuhuri kwa vipindi vyote?
  • Kiongozi mkuu?
  • Mwalimu mkuu?
  • Mtu aliyefanya matendo mema kwa wanadamu kupita mwingine?
  • Mtu aliyeishi maisha matakatifu kuliko yeyote aliyewahi kuishi?

Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia tabaka za dini zao, kama wanajua chochote kuhusu historia, watakubali kwamba hakujawahi kuwa na mtu kama YESU wa Nazareti. Yeye ni mtu wa ajabu mno kuliko watu wote wa enzi zote.

YESU KRISTO alibadilisha mwenendo wa historia. Hata tarehe kwenye gazeti lako la leo inathibitisha kwamba YESU wa Nazareti aliishi ulimwenguni karibu miaka 2,000 iliyopita. Maandishi kwa Kiingereza "B.C." yanasimamia nyakati kabla ya kuzaliwa kwa YESU KRISTO; vilevile maandishi "A.D." yanasimamia nyakati baada ya kuzaliwa kwa Kristo.

KUJA KWAKE KULITABIRIWA

Mamia ya miaka hata kabla ya YESU KRISTO kuzaliwa, maandiko yaonyesha wanabii wa Israeli wakitabiri kuja kwake. Agano la kale, lililoandikwa na watu wengi katika muda wa miaka 1,500, lina unabii zaidi ya 300 kuhusu kuja kwa YESU. Yote yaliyotabiriwa yalitendeka, pamoja na kuzaliwa kwake kimiujiza, maisha yake matakatifu, kufa na kufufuka kwake.

Maisha aliyoishi YESU, miujiza aliyotenda, maneno aliyosema, kufa kwake msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake mbinguni - yote yathibitisha kwamba yeye hakuwa mwanadamu peke yake bali alikuwa zaidi ya mwanadamu. YESU alisema, "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30), "Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:9) na, "Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana 14:6).

MAISHA  NA UJUMBE WAKE HUSABABISHA MABADILIKO

Tazama maisha na mvuto wa YESU wa Nazareti, Mesiya, katika historia yote na utaona kwamba yeye na ujumbe wake huleta mabadiliko makubwa katika mataifa na maisha ya wanaume na wanawake. Popote mafunzo yake yalipoenea, utakatifu wa ndoa, haki na sauti ya wanawake imetiliwa maanani; shule na vyuo vikuu vimeanzishwa; sheria za kulinda watoto zimeandikwa; utumwa umeachishwa; na mabadiliko mengine mengi yamefanywa kwa manufaa ya wanadamu. Maisha ya watu binafsi yamebadilishwa kiajabu. Kwa mfano, Lew Wallace, jemedari aliyejulikana na mwandishi shupavu, alikana Mungu yupo. Kwa miaka miwili, Bw. Wallace alisoma kwenye maktaba zilizo bora sana kule Ulaya na Merikani, akitafuta habari ambazo zingeangamiza kabisa dini ya Kikristo. Alipokuwa akiandika sura ya pili ya kitabu hicho, alijikuta ghafla ameanguka magotini na kulia kwa YESU akisema, "BWANA na MUNGU wangu."

Kwa sababu ya ushuhuda usioweza kukanwa, hakuweza kuendelea kukana kwamba YESU KRISTO alikuwa mwana wa MUNGU. Baadaye, Lew Wallace aliandika kitabu kilichoitwa "Ben Hur", moja wapo ya vitabu shwari vilivyo andikwa katika lugha ya Kiingereza kuhusu nyakati za Kristo.

Vile vile, marehemu C. S. Lewis, profesa wa chuo kikuu cha Oxford, alikana kwamba Kristo alikuwa pia Mungu kwa miaka mingi. Lakini, yeye pia, kwa hekima za ukarimu, alijinyenyekeza mbele za YESU kama MUNGU na Mwokozi baada ya kusoma ushahidi usio na pingamizi kwamba YESU pia alikuwa MUNGU .
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka ni nafasi yako leo kumpa BWANA YESU maisha yako maana hakuna uzima kwingine ila kwa YESU KRISTO. (Yohana 14:6)
ITAENDELEA................

Comments