BARAKA NI NINI?

Na Mtumishi-GERALD ROBERT
BARAKA NI NINI? =Baraka ni nguvu ya Mungu inayofanikisha ambayo Mungu huiachilia nguvu hiyo kwa watu wanao mtii yeye.

 KUMBU KUMBU LA TORATI 28:2- , Na Baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana Mungu wako, utabarikiwa mjini, utabarikiwa mashambani......

 LAANA = Ni nguvu ya Mungu inayokufanya ushindwe, au usifanikiwe Kiuchumi, Ki Afya, Kazini, nk. Nguvu hii nayo hutokana na kutokumtii Mungu, au kutokufanya vile Mungu alivyokuagiza ufanye. KUMBU KUMBU LA TORATI 28:15- .......ndipo zitakuja Laana hizi zote na kukupata, utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani...... Pesa, Nyumba, Magari, Viwanda, Kuwa na Kampuni, Nk. Hayo yote ni matokeo ya Baraka, na sio Baraka halisi. Kwamaana Mungu huanza kuleta Baraka kwanza, ndipo yale Matokeo ya hufuata, mali zinazo onekana kwamacho ni matokeo ya Baraka, lakini Baraka yenyewe huwa haionekani kwa macho. Katika utangulizi wangu pale juu, nilisema kwamba, Baraka ni nguvu itokayo kwa Mungu, na nguvu hiyo ikisha kujilia ndani yako ndipo kila jambo utakalolifanya litafanikiwa. Mfano= Baada ya Mungu kuachilia Baraka ndani yako, Ukifanya biashara, itafanikiwa, utapata pesa, (Kwamaana hakutakuwa na hasara katika biashara yako) 

 Neno lasema hivi, /MITHALI 10:22, Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni nayo/ hivyo basi, Baraka ya Mungu ikikujilia, tegemea mafanikio katika kila jambo ulifanyalo. ..Tuludi kwenye mfano wetu.. Kwahiyo, ikiwa faida iliyopatikana kwenye hiyo biashara yako ukaitumia kwa kujenga Nyumba, au Kununua Gari, nk. Hayo tunayaita ni Matokeo ya Baraka, na sio Baraka yenyewe. Kwamaana, Baraka ni Nguvu, au Uweza wa Mungu uliyoifanya biashara yako ifanikiwe, na hatimaye wewe kununua au kupata kitu au vitu kutokana na Uweza, au Nguvu hiyo ambayo huitwa Baraka, na hapo ndipo watu watakaposema ,, Furani amebarikiwa kupata Gari, Nyumba. Nk. MITHALI 10:6= Baraka humkaria mwenye haki kichwani, bali jeuri hufunika kichwa chake. Je, Baraka ingekuwa ni vitu kama watu wanavyodhani, mfano= Gari, Nyumba, Viwanda, nk. Je,vingewezaje kumkalia mwenye haki kichwani pake ? MALAKI 3:10, Leteni zaka kamili ghalani , ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo (njia ya utoaji) asema Bwana wa Majeshi, mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni Baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Ukisoma vizuri sula hii utagundua kwamba Baraka siyo Vitu, ila vitu ni matokeo ya Baraka, kwamaana Mungu amesema, Nitakumwagieni Baraka (yaani ile Nguv u ya kukufanikisha) hata isiwepo nafasi ya kutosha. Mungu hakusema kwamba , Nitakumwagieni vitu, mfano, Nyumba, magari, nk. Ila amesema atamwaga Baraka, kwamaana Baraka ndiyo itakuwezesha wewe kupata vitu, hata isiwepo nafasi ya kutosha kwa wewe kuweka vitu hivyo. Kama ukiendelea kusoma MALAKI 3:11, Mungu ameahidi kuvilinda vitu vyote vitakavyo patikana kutokana na Baraka zake. Mungu akipendezwa na wewe, na akaamua kuachilia Baraka juu yako, basi ile Baraka itakuletea mafanikio, au kwa lugha nyingine Utakuwa Tajiri, kwasababu ndani ya Baraka kuna Utajiri, Ndio maana Neno la Mungu linasema, MITHALI 10:22 Baraka ya Bwana hutajirisha.  

#MWISHO Mpendwa, Somo la Baraka ni somo lenye malefu na mapana yake , nikipata nafasi nitalimalizia. Kwaana hapa nimezungumzia Baraka za Mungu, pia zipo Baraka zitokanazo na Ibilisi, ambazo mwisho wake ni Uangamivu, na ukibarikiwa na ibilisi utajiri huo huwa haudumu. Tena ni lazima utoe kafara kila baada ya muda furani. Lakini utajiri wa MUNGU ni wa kudumu. MITHALI 8:18, Utajiri na heshima ziko kwangu, naam, utajiri udumuo, na haki pia. =Pia kuna makundi ya Baraka. 1, Baraka za rohoni, 2, Baraka za mwilini =Baraka za rohoni za KiMUNGU, na Baraka za mwilini za KiMUNGU. =Baraka za rohoni za shetani, na Baraka za mwilini za shetani. Nikipata nafasi nitalimalizia somo hili. MUNGU AKUBARIKi

Comments

Unknown said…
Asante mtu wa Mungu Bwana Yesu azidi kukuwezesha katika mema.