BWANA NDIE JIBU,MTATUAJI WA KILA AINA YA TATIZO. *sehemu ya kwanza *

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe...
Hakika mwenye nguvu ni Yeye mmoja tu.
Haleluya...

Tunasoma,
"Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi." Zab 118:5

Mtunga zaburi anatufundisha jambo kubwa sana siku ya leo.
Anatuonesha njia sahihi itupasayo kuifuata pale tupatapo shida,
Njia hiyo ni BWANA tu.
Tazama anasema pale alipopata shida alimuita BWANA,BWANA akamjibu na kumuweka panapo nafasi.

Huyu ni Daudi,mtu aliyeupendeza moyo wa BWANA.
Yeye aliyeukamata moyo wa Bwana.Lakini leo anatuambia naye pia alikuwa na shida.

Kumbe shida zipo hata kwa watumishi wa Bwana.Tena sio watumishi wa Bwana wadogo tuwajuao leo hii,Bali pia hata watumishi kama akina Daudi.
Lakini jambo moja la msingi tunalojifunza hapa kwa habari ya Daudi ni kwamba
• Bwana ndie majibu ya kila aina ya tatizo tulilokuwa nalo.

Naipenda hesabu iliyoitumia Daudi,Kwamba hakuona mtu yeyote Yule ambaye atakayemsaidia juu ya shida aliyokuwa nayo,isipokuwa ni Bwana tu.
Ukweli ni kwamba;
Baba yako hawezi kukusaidia katika shida uliyokuwa nayo,
Mama yako hawezi kukusaidia katika shida yako,
Mchungaji wako hawezi kukusaidia katika shida yako,

Wala mtu yeyote Yule hawezi kukusaidia juu ya kumaliza msiba wako ulio nao,
Isipokuwa yupo mmoja tu,
Nasema yupo mmoja tu asiyeshindwa,
Asiyelala wala asiyechoka,
Naye ni BWANA tu
Yeye aliyekuwepo,
Yeye aliyeko,
Na atakuwapo milele hata milele,ni Bwana tu.

Haleluya…
Ooh! nampenda huyu Yesu wa Nazareti…
Ni Yeye tu aliyebaki…

Laiti kama Daudi asing’eliitia jina la Bwana,asing’elipona katika shida aliyekuwa nayo.
Lakini pale alipomuita Bwana,Bwana akamjibu,kisha akamuweka panapo nafasi.

Sasa angalia hapo;
Zipo hatua alizopiga Daudi katika kuliitia jina la Bwana mpaka akajibiwa,kisha akawekwa mahali panapo nafasi.
Wengi tunaliitia jiana la Bwana lakini hatujibiwi kabisa,
Na hali ikiwa ndio hivyo basi,ipo shida katika kuliitia Jina la Bwana.

Hatua hizo ambazo Daudi alizopitia kisha akajibiwa ndizo tunazotaka kujifunza kiundani ili nasi tupokee majibu yetu…
ITAENDELEA…
• Kwa maombezi,
*0655 111149
*0783 327375

*Usikose muendelezo wa fundisho hili la msingi mahali hapa,
UBARIKIWE.

Comments