BWANA NDIE JIBU,MTATUAJI WA KILA AINA YA TATIZO. *sehemu ya pili *

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla
Bwana Yesu asifiwe...
Hakika mwenye nguvu ni Yeye mmoja tu.
Haleluya...

Tunasoma,
"Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi." Zab 118:5

Anasema,pale alipokuwa na shida hakumuangalia mwanadamu yeyote yule bali alimuangalia BWANA tu,

Kisha BWANA akamjibu.
Neno ‘‘BWANA akanijibu’’Hii ina maana kuwa, jibu haliji mpaka swali liwepo.
Nasema;
Ugonjwa ni swali,
Shida nayo ni swali,
Mateso ni maswali,
Dhiki kubwa ni miongoni mwa swali,

Ukiwa na maswali ya namna hiyo,ujue hakuna wa kukusaidia isipokuwa ni BWANA tu mwenye kuweza kukusaidia.
Yeye Mungu ndie mwenye majibu,tena Yeye mwenyewe ni JIBU TOSHA juu ya maswali yote yaliyokuwako,yaliyopo, hata yatakayokuwepo milele na milele.

Kumbuka,
Daudi alipokuwa na shida (Zab.118:5) hakunyamaza kimya,Bali aliliitia jina la BWANA naye BWANA akamjibu.
Kama ang’enyamaza kimya,basi yamkini asing’epata ufumbuzi wa shida aliyokuwa nayo.
Hivyo basi, Yeye mwenye shida yoyote ile ,iwe ni ugonjwa au ukame wa njaa kali,Basi yampasa KULIITIA JINA LA BWAANA. Naye Bwana atakusikia na kukujibu.

Ooh,..Mimi nampenda sana Daudi vile alivyopiga hesabu na kuona kwamba njia ni moja tu nayo ni ya kuliitia Jina la BWANA.Tazama mtunga Zaburi atuambiavyo leo katika Zaburi hii;

'' Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.’’ Zab.121 :1-2

Duniani ipo milima mbali mbali- yale magumu,shida,vita,N.K hayo na mengineyo yenye kufanana na hayo ni milima,Sasa swali ambalo linaulizwa hapo katika hiyo zaburi kwamba;
*Msaada juu ya hiyo milima utatoka wapi?

Oooh..Tazama jibu lake lilivyozuri,
Anasema ;
'' msaada wangu U katika Bwana,’’

Jambo moja la leo tunalojifunza mahali hapa ni kwamba,
• Ili upate msaada juu ya tatizo ulilokuwa nalo ni lazima ukaze kuliitia jina la Bwana.

Ni kweli,Bwana anafahamu shida uliyokuwa nayo,Lakini anakusubiri wewe utende, kisha naye atende.
Na hiyo ndio principal Yake.
Na ndio maana hata Yesu alipokutana na Bartimayo yule aliyekuwa ni kipofu,alimuuliza

'' Wataka nikufanyie nini?’’ Marko 10 :51.

Si kama BWANA YESU alikuwa hamuoni Bartimayo kwamba ni kipofu,bali alihitaji kujua nini haswa ambacho Bartimayo anachokitaka kutoka kwake?
Alikadhalika katika milima uliyonayo leo hii,
-BWANA anakuuliza wataka nikufanyie nini?

*Sasa imebaki kwako kujibu,kwamba watakaje?

Katika mstari wetu wa kusimamia fundisho hili,tumeona kwamba ilimbidi Daudi apaze sauti kwa BWANA akihitaji msaada,ndipo baadaye Bwana akamjibu.
Hii ni safi sana,naipenda staili hii.

WAWEZAJE KUPOKEA MUUJIZA WAKO ?
Zipo njia kuu za msingi,
Njia mojawapo,nayo ni ya kwanza ,ndio hii;

01.KUJISALIMISHA KWA BWANA.
Hakuna njia mbadala wa kupona kwa hilo tatizo lako ulilonalo pasipo KUJISALIMISHA mbele za Bwana.
Nasema ni KUJISALIMISHA,ikiwa na maana kwamba;
• Kujifichua pale ulipojificha,
• Kujidhili mbele za uso wa Bwana
• Ku-Salenda mikono juu mbele za Bwana.

Mimi binafsi nimeshajisalimisha mbele za Bwana,nami nipo huru,huru kweli kweli….

Katika kujisalimisha mbele za Bwana,ipo gharama ikupasayo uilipe.
Gharama hiyo ni kudharau AIBU. Kujikataa wewe mwenyewe kwamba huwezi,na kuhitaji msaada utokao juu kwa BWANA…

ITAENDELEA…
• Kwa maombezi,
• 0655 111149
• 0783 327375

Usikose muendelezo wa fundisho hili la msingi mahali hapa,

UBARIKIWE.

Comments