BWANA NDIE JIBU,MTATUAJI WA KILA AINA YA TATIZO.* sehemu ya tatu *

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Tunasoma,;

"Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi." Zab 118:5
Andiko hilo ni andiko letu la kusimamia fundisho hili.

Haleluya…
Nasema Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana libarikiwe.

Bwana ana majibu yako juu ya tatizo ulilonalo.Shida haiko kwa Bwana bali shida iko kwako wewe mwenyewe jinsi umuendeavyo Bwana.
Majibu yapo tayari kwa ajili yako,
Nafasi ipo tayari kwa ajili yako,Ila ni wewe mwenyewe unajichelewesha kupokea,sababu ya njia unayoitumia.

Lakini ipo NEEMA mahali hapa kwa fundisho hili kwamba tujifunze kwa usahihi kabisa njia sahihi za kupokea miujiza yako.

Kumbuka nilikuambia kwamba zipo hatua za kutufanya tuweze kupokea muujiza yetu ,
Nami nalikuambia njia mojawapo ya kwanza ya kupokea muujiza wako,sababu Bwana yupo hai kukujibu.
Njia hiyo tuliyojifunza ni;

*KUJISALIMISHA KWA BWANA YESU.

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu,Biblia,wale wote waliopokea miujiza yao ni wale ambao walimuendea Bwana Yesu.
Yaani wale wote walioponywa walibidi wakutane na Bwana Yesu ndipo wapokee uponyaji wao.

Ila imeandikwa mara moja katika Biblia ikishuhudia mtu mmoja tu, aliyepokea uponyaji wake akiwa mbali na Bwana Yesu.
Huyu mgonjwa alikuwa ndio wa pekee katika Israeli kuponywa akiwa mbali na Bwana Yesu.
Kwa habari yake mgonjwa huyu,tunajifunza fundisho kubwa sana.

Tunasoma;
‘’ Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.’’Mathayo 8:5-6

Haleluya…

Labda nikujuze kidogo juu ya Kapernaumu,
Kapernaumu ilikuwa ni moja ya sehemu ambayo Bwana Yesu Kristo aliitumia katika huduma yake.

Zipo sehemu nyingine zilizokuwa zikiendana na sehemu hiyo.
Sehemu hizo ambazo kiukweli zilifanyika Baraka kwa huduma ya Bwana Yesu,Nazo ni
*Korazini
*Bethsaida.

Hizi sehemu tatu (Kapernaumu,Korazini,&Bethsaida) zipo mfano wa umbo la pembe tatu,triangle.Zote zipo ndani ya Galilaya.

Sasa tazama Yesu anaingia Kapernaumu,na huko anakutana na Akida mmoja ambaye alimuendea Yesu akiwa yeye kama yeye hakumuendea na mgojwa.Akida alimuacha mgonjwa wake nyumbani,
mgonjwa aliyekuwa anaumwa sana,naye Akida akamuacha kisha akamuendea Bwana kwa ajili ya uponyaji wa Yule mgonjwa.

• Hii sio hali ya kawaida,kwa sababu ilizoeleka kwamba uendapo kwa daktari basi ni lazima uende na mgojwa.

Tazama Yesu alipotaka kwenda kwa Akida ,huyo akida akamwambia haina haja ya kwenda bali Yesu atamke neno tu na mtumishi wake atapona.

Yesu Kristo Yeye mwenyewe akakiri ya kwamba hajawahi ona IMANI KUBWA namna hii.(Mathayo 8:10)

Mgonjwa akaponywa tangu saa ile ile.
Kile kilichosababisha aponyaji ni IMANI KUBWA aliyokuwa nayo yule akida.

Nasema IMANI ile aliyokuwa nayo Akida ni imani iliyomshangaza Bwana Yesu. Kwa sababu hajawahi kuonekana katika Israeli IMANI ya namna ile.Maana wale wote walioponywa walibidi wapelekwe kwa Bwana Yesu,Lakini hii ya Akida ni ya tofauti kabisa.

Leo ili uweze upokee muujiza wako wa uponyaji ni lazima umuendee Bwana Yesu kwa IMANI,kama vile alivyofanya Akida.

Akida alikuwa na tegemeo la kuponywa kwa mgonjwa wake na ndio maana alimuendea Bwana Yesu pekee na hakumuendea mwingine yeyote yule, bali Bwana tu,Kwa mfano huo anatufundisha kwamba Bwana ndie mwenye majibu,naye Bwana ndiye jibu.

Haleluya…

Tuangalie tena watu wengine wenye akili,ambao walitumia njia hii ya kwanza ya kumuendea Bwana kwa ajili ya uponyaji wao.Watu wa namna hii hawakumuendea hivi hivi tu bali walipiga hesabu kwanza,Nami nazipenda hesabu zao,

Tunasoma;

'' Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.
Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.''
Mathayo 9:32-33

Tazama hesabu iliyopigwa hapo,
Hawa ndugu waligundua kwamba bubu waliyekuwa naye kamwe hawezi kumuendea BWANA yeye kama yeye bali walipoona hivyo wakaamua KUMPELEKA kwa BWANA.

Nimeipenda hii habari sana,
Inatufundisha hata sisi wa leo,kwamba wapo watu katika jamii tuishizo ambao hawawezi kumuendea Bwana pasipo kupelekwa….

ITAENDELEA…
• Usikose fundisho lijalo mahali hapa,ambapo tutachimba zaidi.
Kwa maombezi;

• 0655 111149
• 0783 327375

UBARIKIWE.

Comments