BWANA NDIE JIBU,MTATUAJI WA KILA AINA YA TATIZO.*sehemu ya nne *


Na mtumishi Gasper Madumla

Tunasoma;
"Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi."
Zab 118:5,
(Andiko la kusimamia fundisho hili)

Mtunga Zaburi anajaribu kuelezea pale alipopata shida,alimuita Bwana,Bwana akamjibu.
Ikiwa Bwana alimjibu basi Yeye BWANA ndie JIBU wa tatizo lake.Sikia hapo,
alipokuwa na shida -hakuwa katika nafasi ya ki-ungu,yaani ile nafasi ambayo anastahili kuwapo,
ndio maana BWANA alipomjibu kitu cha kwanza AKAMWEKA PANAPO NAFASI.

Mtu mwenye shida hana nafasi,
ili awe na nafasi yambidi aliitie jina la BWANA ili BWANA mwenye kutoa nafasi ampatie nafasi.
Nafasi katika ulimwengu wa roho ni KIBALI.

Oooh kumbe !;
Kibali chatoka kwa BWANA,na kumbe kibali kipo tayari kwa ajili yetu, pale tutakapomuita BWANA,BWANA atatujibu na kukiachilia kibali mbele zetu.
Basi Ikiwa ndio hivyo BWANA ndie JIBU na mtatuaji wa kila aina ya shida.

Nakusalimu mpendwa,
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya…

Nasema Haleluya….
Jina la BWANA lisifiwe…

Tulikuwa tunaangalia njia ya kwanza ya kupokea majibu yako kutoka kwa Yeye Mungu mwenye majibu.
Na nilikuambia njia ya kwanza ni ;
Kujisalimisha kwa Bwana Yesu.

Na hapo tuliona watu wachache wenye akili ambao walimfichua mtu bubu mwenye pepo kwa kumpeleka kwa BWANA,
BWANA akamponya,
naye huyo bubu akanena kwa mara ya kwanza ,kisha makutano wakastaajabu.
Maana haikuwahi kuonekana katika Israeli wakati wote
(Mathayo 9 :32-33)

Kumbuka;

Yule bubu asin’geponywa kama asing’epelekwa kwa BWANA.
Watu walipoona yafaa kumpeleka,Wakampeleka mbele za Bwana,Naye akapokea uponyaji saa ile ile.

Nasi yatupasa kuwaleta wenye mapepo,magonjwa,wadhaifu,N.K
Wote hawa hawawezi kumwendea BWANA wao kama wao,muda mwingine yatupasa KUWAPELEKA ndipo waponywe.

Ili umpeleke mgonjwa kwa Bwana,Hakikisha kwanza wewe mwenyewe sio mgonjwa. Yaani uwe safi,
safi katika kila eneo,
uwe safi hata katika kinywa,
maana mgonjwa anahitaji maneno ya faraja
Kwa kumuambia mfano;

'' Utapona tu,yupo Yesu wa Nazareti asiyeshindwa na ilo tatizo lako.,…Polee mpendwa,hayo ni ya kawaida kabisa,mpe maisha BWANA Yeye atakutua mzigo wako…N.K ''

-Lakini sio uwe na maneno ya kumvunja moyo.

Haleluya…

Tuwapeleke wagonjwa kwa BWANA ambaye Yeye ni JIBU na mtatuaji wa kila aina ya shida.

Tuangalie mfano mwingine mmoja katika siku ya leo kwa habari ya KUJISALIMISHA KWA BWANA.
Nimekuambia kwamba,hiyo ndio njia ya kwanza ya kupokea uponyaji wako,
Na hapa tunasoma,

Marko 5:27-28,&34
'' aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.’’

Haleluya…

Huyu ni mwanamke aliyetokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, Alafu sio tu kutoka damu,sikia, Biblia inasema aliteswa sana kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.

*Oooh,Jesus,I’ve mercy on us…
Unajua watu wengi wakisoma maandiko kama haya yenye kuelezea shida za watu kama hizi,wanafikiri kwamba ilikuwa rahisi….

Mimi nasema hapana,
Haya mazingira tunayoyasoma katika maandiko matakatifu ni mazingira magumu sana,
Tazama habari hiyo hapo juu ya huyo mwanamke aliyetokwa na damu muda mlefu namna hiyo pasipo kupona na pia alipoteza mali zake zote,nasema alipoteza mali zake zotee,sio mali kidogo bali ni mali zake zote zilipotea,
na hata hapo bado hakukumfaa kitu.

Sasa utaona ni jinsi gani alivyokuwa akiteseka huyu mwanamke.
Lakini leo anatuambia habari njema maana haumwi tena,
Hateseki tena,
Hana msiba tena,
Maana amemwendea mmoja mwenye majibu juu ya tatizo lake la kutokwa damu.
Ni Yesu pekee ambaye ndie daktari wa kweli,
Yeye ni bingwa wa mabingwa.

Nalikuambia tunajifunza njia moja tu ya kupokea muujiza/uponyaji wako na ni
KUJISALIMISHA KWA BWANA.

Mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu muda mlefu huo,Yeye alipoijua siri hii ya uponyaji,
kwamba uponyaji halisi upo mbele za BWANA,alifunga safari na kumuendea mahali alipo BWANA.
Biblia inasema
'' aliposikia habari za Yesu,
alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;’’ Marko 5 :27

Sikia sasa,
Huyu mwanamke alikuwa ana akili nyingi sana,
Maana yeye alihitaji kwanza KUSIKIA HABARI ZA YESU.Kisha aliposikia AKACHUKUA HATUA kwa kupita kwa nyuma ya mkutano na kuligusa vazi lake.

Tazama hapo kwa makini Biblia inasema '' Aliposikia…'' IMANI ya mwanamke huyu ilianzia hapo kwa kusikia habari za Yesu Kristo.
Na mara tu baada ya kusikia AKAPIGA HATUA,
Hii ikimaanisha kwamba ALIPOKUWA NA IMANI AKAJUMLISHA NA MATENDO ya kugusa pindo la vazi la BWANA. Naye akapona na ule msiba saa ile ile.

Hizo hatua alizozichukua mwanamke huyu,ndizo hatua tutakazojifunza katika fundisho lijalo…

ITAENDELEA…
• Usikose fundisho lijalo mahali hapa,ambapo tutachimba zaidi.
Kwa maombezi;

• 0655 111149
• 0783 327375
UBARIKIWE.

Comments