BWANA NDIE JIBU,MTATUAJI WA KILA AINA YA TATIZO.* sehemu ya tano *

Na mtumishi Gasper Madumla


Haleluya...
BWANA YESU asifiwe...

Dhima kuu ya fundisho hili mahali hapa ni kuonesha kwamba upo msaada wakati wa shida,
Msaada utokao kwa Bwana.

Yamkini wewe unayeteseka na magonjwa,mateso ya pepo na kila aina ya udhaifu,BWANA MUNGU yupo pamoja na wewe,kamwe hajakuacha.

*Mungu yupo hapa kukuponya.

Katika fundisho lilopita tulijifunza njia moja ya kupokea muujiza wako,
Njia hiyo ni:
Kujisalimisha kwa BWANA.

Na tulisoma habari ya mwanamke aliyekuwa na MSIBA wa kutokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili.
Uponyaji wake ulitegemea, kwanza akutane na Bwana Yesu ndipo aponywe.

Labda tuendelee tena na tena kujifunza kwa habari hii.
Kwa kifupi,
Soma,
Marko 5 : 25-34.

Tuangalie sasa mstari mmoja tu au miwili,kwa siku ya leo.

Haleluya...

Tunasoma;
"Aliposikia habari za Yesu,..."Marko 5:27a

Huyu mwanamke kwanza alihitaji ASIKIE habari za Yesu.Na wala hakuhitaji kupona kwanza ingawa dhumuni lake ni kuponywa.

Ni watu wachache sana wanaweza kuelewa hilo,na ni wachache pia wenye kuweza kufanya hivi,Bali wengi hatuwezi.
Nami naomba nawe uwe miongoni mwa hao wachache wenye kutaka kwanza kusikia NENO LA BWANA MUNGU.

Aliposikia habari za Yesu ndipo alipokuwa na ujasiri wa kuchukua hatua ya kwenda nyuma ya mkutano na kuligusa pindo la vazi la Bwana Yesu.

Kwa lugha nyingine ni kwamba,
Asing'eweza kwenda kuligusa vazi la Bwana kama asing'esikia habari za Bwana Yesu.

KUSIKIA ni chanzo cha IMANI,au
Niseme hivi,
IMANI chanzo chake ni kusikia neno la Kristo. (Warumi 10:17)

Baada ya kusikia hufuata matendo kwa kile ulichokisikia.
*Na ndio maana IMANI sio IMANI bila matendo.

Haleluya...
ooh !
nampenda huyu mwanamke,alijua siri ya imani kwamba ni kusikia Habari za Yesu.

Anatufundisha kitu kizuri sana siku ya leo,
Kwamba Bwana yupo na majibu yetu yapo mikononi mwake Bwana.

Lakini Bwana anahitaji kutuona Kuwa ni watu wasikivu juu ya neno lake.

Maana mtu msikivu wa NENO ni mtendaji wa NENO.

Mara nyingi hatuponywi kwa sababu sio watu wasikiaji wa neno la BWANA. Leo tupone jamani!

Aliposikia habari za Yesu,tunaona huyu mwanamke anajihimalisha kusimama katikati ya kusanyiko,na kumuendea Bwana kwa ujasiri ambao hata wale waliokuwa wakimsikiliza Bwana Yesu ,hawakuwa na ujasiri huu.

Kumbe,
Mtu aliyelijaza neno la Kristo huwa ni jasiri,
Haijalishi mazingira yanasemaje,lakini ni lazima awe jasiri na ashinde zaidi ya kushinda.

Bwana Yesu, anamwambia huyu mwanamke kwamba,

"Binti imani yako imekuponya,enenda zako kwa amani,usiwe msiba wako tena. " Marko 5:34

Bwana Yesu alichungulia kiwango cha imani ya huyu binti,akagundua kwamba Imani yake ni kubwa.

Hivyo hapo tunafundishwa kwamba ili tupokee miujiza yetu ni lazima tuwe watu wa imani kubwa.

Hiyo ni njia moja tu ya kujisalimisha kwa BWANA,
Maana haya yote yametokea mbele za BWANA.

Haleluya..
Nasema Haleluya...

Watu wote waliomuendea Bwana Yesu kwa habari ya uponyaji wao,
Hawakumuendea wakiwa na mikono mitupu,Bali walimuende wakiwa na IMANI ya kuponywa.

*Imani ya kuponywa ni chombo cha kupokelea miujiza itokayo kwa Bwana

Ipo imani kama imani, na pia ipo imani ya kuponywa.

Tunasoma;
" Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena ;ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana IMANI YA KUPONYWA ''Matendo 14:9

Ukiendelea kusoma utaona yule kiwete akaponywa kwa kuambiwa asimame na aende,wala hakuwekewa mikono ili kuponywa.

Kilichohitajika kwake ni kuwa na imani ya kuponywa,na kusikia habari za Yesu kwa usahihi wake.

Leo yawezekana ni mgonjwa,
Yawezekana umekosa msaada juu ya tatizo ulilonalo muda wote huo,
Yawezekana yapo mateso.,
Yawezekana umekata tamaa
Juu ya hilo ulilonalo.

Nami nakutangazia uponyaji wako kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti.

Kwa maombezi ,
*0655 111149
*0783 327375

ITAENDELEA....

*Usikose fundisho hili mahali hapa.

UBARIKIWE.
Na mtumishi Gasper Madumla

Comments