BWANA NDIE JIBU,MTATUAJI WA KILA AINA YA TATIZO * sehemu ya mwisho *


Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...

Siku ya leo,Bwana Mungu akuhudumie kwa namna ya tofauti tunapomalizia hii tafakari.

Kumbuka, tulikuwa tumekwamia kuchimba kiundani katika tafakari,

Tukijifunza juu ya njia moja ya kwanza ya kupokea muujiza/jibu lako kutoka kwa mwenye majibu ambaye ndie wa milele,

Ni Bwana wa mabwana,
Mfalme wa wafalme,
Mungu mwenyezi,
JEHOVA aliyekuwepo,aliyepo na atakayekuwapo milele na milele.

Tulijifunza njia moja ya kupokea jibu lako nayo hiyo njia nilikuamba ni kujisalimisha kwake BWANA.

Leo tunajifunza njia nyingine ya kupokea jibu lako.
Kumbuka kwamba,
Kila jibu juu ya swali ulilonalo lipo kwa BWANA.

Labda kabla hatujaangalia njia nyingine itupasayo kupokea majibu kutoka kwa Bwana,
Niseme hivi;

Katika njia hiyo ya kujisalimisha kwa Bwana,ipo gharama ikupasayo kuilipa.

Gharama yenyewe ni ya kuidharau aibu.

Aibu ni gharama,
Aibu hutesa maisha yetu,
Wengi,hatupokei kwa sababu ya kuwa na AIBU.

Mungu leo atusaidie sana tuweze kuidharau aibu.

Ili ujifichue na umfuate Bwana Yesu,lazima ukubali kuacha yote.

Tazama sasa;
jamii inayokuzunguka itakusema vibaya,kwa sababu ya kumfuata Bwana Yesu.

Kujisalimisha kwa Bwana Yesu ni kuokoka.

*kuokoka ni kukutana na Yesu.

Yeye aliyejifichua na kumfuata Bwana Yesu, usamehewa dhambi katika sala ya toba,
Pale atakapoongozwa na mtumishi wa Mungu.

Bwana anatutaka leo twende mbele zake tukaoshwe dhambi zetu zote ;
tuwe wake kweli kweli.

Ndugu usomaye,
Bado hujachelewa,
kumbuka Bwana ndie jibu lako,naye Yupo akikungoja ujifichue kwanza,
ukamuendee uokoke kwa faida yako mwenyewe.

Tazama akituambia leo maneno haya;

Mathayo 11:28-29

" Njooni kwangu,ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo,nami nitawapumzisha.

Jitieni nira yangu,mjifunze kwangu;kwa kuwa Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo;
nanyi mtapata raha nafsini mwenu; "

Leo Bwana anatualika twende kwake sisi tusumbukao na wenye kuelemewa na mizigo.

Anakualika wewe pia,tena no buuree!
umuendee Yeye Mungu wa kweli,maana Yeye haitaji pesa yako,

Wala haitaji Mali zako,
Wala haitaji umuonge,
Bali anahitaji leo ufungue MOYO wako,ukajisalimishe kwake,uokoke kwa toba ya kweli.

Mateso uliyokuwa nayo ni mzigo wenye kukuelemea,
Lakini;
Yupo Bwana Yesu wa Nazareti atakaye kukutua.

Bwana ndie jibu lako,
Yupo hai halisi kukuokoa.

Mimi sijui unateseke na nini?
Sijui nini kinakutesa?

Lakini Bwana Yesu leo yupo,Yeye anajua unachoteseka nacho ,mkimbilie upokee jibu lako.

Nalikupa mifano michache ya watu waliokuwa wameifuata njia hii tujifunzayo mahali hapa,
Njia
Ya kumuendea Bwana juu ya shida walizokuwa nazo,

Nao wote walipokea saa ile ile kile walichokihitaji.
Ikiwa wote hawa waliponywa,
Basi hata wewe waweza kuponywa.

Haleluya...

Nasema na mtu mmoja mahali hapa,
Nikikutia moyo kwamba jambo lolote lile ambalo ni msiba kwako,
Kwa BWANA MUNGU sio msiba.

*Yeye MUNGU,anao uwezo wa kutatua yote yaliyokushinda.

Nasema, njia ya kwanza ni kujisalimisha kwa BWANA.
Hakuna njia nyingine iwayo tote,

Isipokuwa ndio hiyo tu ya kwanza,
Njia nyingine zitafuta baada ya njia hiyo kufanyika.

Tazama,mgonjwa mmoja wa kifafa aliyeponywa na Bwana Yesu.
(Soma Mathayo 17:14-21)

Mgonjwa huyu asing'eponywa kama asing'efichuliwa kwa kupelekwa mbele za Bwana Yesu.

Watu waliompeleka kwa BWANA waligundua kwamba,
Njia ya uponyaji wa mgonjwa wao ni BWANA tu.

Na tunaona wakimpeleka kwa Bwana Yesu pekee.

*Wewe je,wangoja nini?

Wapo watu leo hii wakiteseka Sana kwa hospitali,
Wakiwaendea hata waganga wa kienyeji,wakitaraji kupata majibu.

Lakini ukweli ni kwamba hawapati chochote,maana hao wote ni wanadamu tu.

Mimi nakutangazia kuachiliwa kwako juu ya tatizo ulilokuwa nalo kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti,POKEA SASA UWE MZIMA.

Tuangalie tena njia pili ya kupokea jibu lako kutoka kwa Yeye BWANA mwenye majibu, nayo ni;

02.KULIFUATA NEN0 LA KRISTO.

Haleluya...

Nimekuambia kwamba,
Bwana anayo majibu yako yote.
Ili upokee yakupasa uwe mtu aliyejaa NENO LA MUNGU pia uwe mtendaji wa NENO.

Mtu wa namna hii ambaye amelihifadhi neno la Bwana huwa haitajiki kuombewa ombewa;
Sababu neno la Bwana lenyewe ni dawa tosha kwa yeye alijazaye.

Njia hii ya kulijaza NENO la Bwana pamoja na kulifuata ni njia ngumu sana maana hakuna waezaye kulijaza neno la Bwana kwa akili zake mwenyewe,
Isipokuwa kwa msaada wa Roho mtakatifu.

Hapa sasa ndipo Roho mtakatifu anahitajika sana,
Maana tunapozungumzia neno la Mungu, tunazungumzia pia habari za Roho mtakakatifu.

Tumuombe Mungu leo atujaze Roho wake katika kulijaza neno lake.

Yanawezekana haya yote kwa msaada wa Roho mtakatifu.

Ikiwa lipo jambo lenye kukutesa,
Ikiwa upo ugonjwa kwako,na umeuchoka kabisa,
Ikiwa yapo mateso kwako,
Ikiwa yapo mambo ambayo kiukweli kabisa ni mambo magumu kwako kimaisha,

Basi nataka niombe na wewe siku ya leo.

Mawasiliano yangu ni;
0655 111149,
0783 327375.

MWISHO.

UBARIKIWE.

Comments