CHRISTINA SHUSHO AZUNGUMZA NA WANAHABARI

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Christina Shusho amefanya mazungumzo na wanahabari katika hoteli ya Keby's maeneo ya Bamaga kuhusu tamasha lake kubwa la uimbaji alilolipa jina la "Nataka nimjue" lililobeba jina la video yake mpya litakalofanyika katika ukumbi wa kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga jijini Dar es salaam tarehe 24 mwezi huu kuanzia majira ya saa 9 mchana. Katika uzinduzi huo atasindikizwa na The Voice, John Lisu, Bahati Bukuku, Kinondoni Revival Choir, Joshua Mlelwa, Upendo Kilahiro, Amani Kapama, Paul Clement na waimbaji wengine.
chanzo: Gospel kitaa

                              

Bwana Prosper Mwakitalima ambaye ndie mratibu wa tamasha hilo akizungumza na wanahabari ambao hawapo pichani.
Christina Shusho muhusika mkuu wa tamasha akizungumza.

Wanahabari wakisikiliza kwa makini.







Christina Shusho akiwa na wawakilishi wa kundi la The Voice ambao watashiriki katika tamasha hilo.
Blogger Unclejimmy Temu akiweka mambo sawa na Fred.
Ritha Chuwalo na King Chavala nao walikuwepooo.   

Comments