COSMAS CHIDUMLE AFANYA MKUTANO: NGUVU YA MUNGU YASHUKA NA WATU WAOKOLEWA



Mkutano wa Injili unaoendelea katika eneo la Vijibweni Soweto kata ya Kigamboni, Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. Bwana ameendelea kujidhihilisha kwa namna ya ajabu huku Mtumishi wa Mungu Cosmas Chidumle akiendelea kuwa chombo kinachotumika kuwaleta watu kwa Bwana Yesu.

Kati ya vivutio katika mkutano huo ni uwepo wa Mtumishi wa Mungu Betrice William aliyekuwa mshiriki wa Bongo star search akijulikana kwa wimbo wa KUSAKA MAHELA baada ya kuokoka amejikita katika uinjilisti kwa njia ya uimbaji sasa anakuambia SIO KAWAIDA WATAHEMEA JUU JUU, Wimbo ambao ukiimbwa uwanja wote unaitika kwa shangwe kama ilivyo kawaida kwa Betrice William kulitawala jukwaa.




Beatrice William(Beatrice wa BSS) akiimba Watahemea Juu juu


NEEMA JECKONIA
Kivutio kingine katika mkutano huo ni Muimbaji anae jua kulitumia vyema jukwaa kiasi kwamba halimtoshi inabidi ashuke chini ni Mrs Chavala au Neema Jeckonia ambaye hakufanya makosa alipo karibishwa aimbe wimbo wa MWENYE UWEZA ulio katika mahadhi ya Segele. Hakika Yesu anasifiwa kwa namna tofauti.
Frola Fabian kama kawaida akimtukuza MUNGU

Muimbaji Frola Fabian akiimba huku akisindikizwa na Bloggers, Robert Maziku(Admin wa Injili Forever mwenye shati jeusi) na Peter Michael(Admin wa Maisha ya Ushindi) wakicheza kwaito la Yesu.
Segele sio muondoko pekee adimu ulio jitokeza katika Mkutano huo unao endelea mpaka jumapili ya Tarehe 17/11/2013 bali uimbaji wa nyimbo zenye mahadhi ya kwaito uliimbwa pia.
Mtumishi Cosmas Chidumle akihubiri
Kama ilivyo katika mkutano mwisho alisimama Gwiji la Mziki(Mwana Mziki halisi) ambae kwa sasa anamtangaza Yesu kwa Nguvu zake Mwinjilisti Cosmas Chidumle. Aliwaambia wakazi wa Vijibweni kuwa Kama ni Uhuni yeye alikuwa Mhuni zaidi, kama ni usharobaro basi alikuwa hivyo ila wa enzi hizo. Pamoja na maisha ya kujulikana aliyoyaishi kipindi hicho hakuwa na furaha kwani alikuwa amepungukiwa kitu. Yesu alipoingia katika maisha yake maisha yake yamekuwa ya tofauti sana. Mwinjilisti huyo aliutumia dakika kumi kuhubiri kutokana na kuchelewa kufika lakini hio ilikuwa Ijumaa lakini Jumamos Mungu anaenda kutembea kwa njia ya ajabu ambapo Mtumishi atasimama mapema na watu kwenda kufunguliwa.
Katika mkutano huo watu walimkubali Bwana Yesu na kuongozwa sala ya toba.
MKUTANO HUU UNALETWA NA KANISA LA P.A.G.

Comments