![]() |
Don moen |
Don
moen ni muimbaji na mtunzi wa mashairi ya injili aliezaliwa tarehe 29
june 1950 huko Minneapolis Minnesota nchini Marekani. Don alifahamika
baada ya kutoa album aliyoipa jina lake la Worship with Don Moen mwaka
1992. Album hiyo iliuza zaidi ya nakala milioni tano na kumfanya Don
kuwa kwenye orodha ya waimbaji waliouza zaidi nchini Marekani.
Alifanya
kazi na Integrity records kwa miaka 20 akiwa kama mbunifu mkuu wa
integrity music na rais wa integrity lebel. Aliachana na integrity
records mwaka jana(2008) na kuanzisha kampuni yake ya The Don Moen
Company. Kampuni hiyo imempatia Don tuzo ya Dove mwaka huu huku akiwa na
tuzo zingine tisa alizozipata kwa kazi ya muziki. Akiwa kama mtunzi wa
mashairi amewatungia waimbaji wengi kama; Claire Cloninger, Paul
Overstreet, Martin J. Nystrom, Randy Rothwell, Ron Kenoly, Bob Fitts,
Debbye Graafsma, Paul Baloche na Tom Brooks.
Album
ya Hossana give thanks ilikuwa album bora ya label ya intergrity, album
hiyo ilifuatiwa na album nyingine mbili zilizozofanya vizuri, En tu
Presencia and Trono de Gracia ambazo alizitua kwa lugha ya kispaniola.
Akiwa kwenye ziara barani Asia mwaka 1999 alirekodi singo ya The Mercy
seat kwenye uwanja wa michezo wa Singapore nchini Malaysia na Heal our
land akiwa Yodo park nchini Korea Kusini mwaka 2000.

God
will give way(the best of don moen) ilitolewa mwaka 2003, wimbo
uliobeba album hiyo wa God will give Way aliutoa maalum kwa ajili ya
dada yake na mumewe ambao walimpoteza mtoto wao wa kwanza kwenye ajali
mbaya ya gari huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya. Don anatarijiwa
kutoa album ya I belive there is Way ambayo itakuwa ya mwisho kufanywa
na Integrity records. Don ametoa Album zaidi ya album 20 baadhi ya album
hizo ni;
.†Give Thanks
. .†Steadfast Love
.†Bless the Lord
.†Christmas
.†Eternal God
.†Worship with Don Moen
.†God with Us
.†Trust in the Lord – Live Worship with Don Moen
.†Rivers of Joy
.†Emmanuel Has Come
.†Praise with Don Moen
TUZO
Baadhi ya tuzo alizoshinda nipamoja na hizi zifuatazo
Ameshinda tuzo za Dove mara tisa
1994-Album bora ya mwaka “God with Us”
Dove Awards
1992-Wimbo bora wa mwaka “God Will Make A Way”
1993-Album bora ya mwaka “Worship with Don Moen”
1995-Wimbo bora wa mwaka “Mighty Cross”
1998-Wimbo bora wa mwaka “Emmanuel Has Come”
1999 -Album bora ya mwaka “God for Us“
2001-Album bora ya kispaniola ya mwaka “En Tú Presencia”
2003-Record bora ya country ya mwaka “God Is Good All The Time”
2004-Album bora ya kispaniola ya mwaka “Trono de Gracia”
Don kwa sasa anaishi Alabama nchini Maekani pamoja na mkewe Laura na watoto wao watano.

Comments