Beatrice akiimba baada ya kuokoka.
Ilikuwa Ijumaa ya Tarehe 15/11/2013 nikiwa Vijibweni
Soweto(Kigamboni) kwenye mkutano niliokuwa nimealikwa na rafiki yangu
Peter Michael ambae ni Blogger wa Maisha ya ushindi. Muhubiri katika
mkutano huo alikuwa ni Cosmas Chidumle. Akili yangu ilikuwa na shauku ya
kumuona Mtumishi wa Mungu Cosmas Chidumle hasa kutokana na historia
yake ya mziki hapa Tanzania.
Nilifika mapema kabla ya mkutano kuanza pia nilimuwahi mwenyeji
wangu Peter Michael, nikiwa nimekaa kwenye viti ghafla nikamuona binti
ambae akili yangu ilianza kumpambanua ni nani kwasababu ilikuwa kama
namfahamu vile ila ilinipa tabu kidogo kumkumbuka. Nilipo ona picha
haiji nikaamua kumpotezea, mpaka muongozaji wa ibada alipo simama
akasema "Namkaribisha dada Beatrice William aje aimbe nyimbo mbili" watu
wakaanza kushangilia bado nikapotezea. Nikasikia "naitwa Beatrice
William wengi wananijua kwa jina la Beatrice wa BSS, Sasa sisaki mahela
namsaka Yesu" Akili yangu ikafunguka na mdomo wangu ukasema ANHAAA.

Beatrice William akiwa na Robert Maziku(Mwandishi wa Makala hii).
Namshukuru Mungu nimefanikiwa kutimiza ahadi niliyowaahidi
wasomaji wetu wa Blog ya Injili Forever ambapo niliwaambia nitawaletea
mahojiano. Mahojiano haya yamefanywa Tar 20 na 21 mwezi wa kumi na moja
2013.
FATILIA HAPA SASA,
Robert Maziku(RM): Bwana yesu asifiwe dada.
Beatrice William(BW): Amen Habar yako?
RM: Nzuri unaongea na Robert wa Blog.
BW: Ok. Niambie,
RM: Samahani dada, Nataka kujua baadhi ya mambo ambayo watu wakiyafaham kuhusu wewe yataleta chachu nakuwa sehemu ya Injili.
Beatrice kabla hajaokoka

BW: Haina shida, (kwa sauti ya kukaribisha mazungumzo).
RM: Kwanza kabisa majina yako ninani na mwenyeji wa wapi?
BW: Majina yangu ni Beatrice William, ni Mhaya ingawa nimekulia Mwanza.
RM: Unamiaka mingapi?
BW: Nilizaliwa miaka 32 iliyopita, ni mtoto wa nne kati ya watoto wanne kwahio ni mtoto wa mwisho.
RM: Inasemekana umeolewa na unawatoto?
BW:
Niliolewa miaka 13 iliyopita ila kwasasa sipo kwenye mahusiano kwa muda
wa miaka minne unaelekea mwaka watano sasa. Hata wakati nashiriki Bongo
star search sikutoka kwa mume. Mimi ninawatoto watatu wa kwanza
anamiaka kumi na tatu(13), wapili kumi na moja(11) mdogo anamiaka nane
8.
RM: Ulianza lini kuvaa mavazi ya kiume?
BW: Nilipo maliza shule tu sketi nikaachana nazo sikupenda kabisa sketi.
RM: Kwanini ulipenda hayo mavazi?
BW: Kwakweli ilikuwa nikivaa hayo mavazi najisikia ninaujasiri wa ajabu sana.
RM: Mambo gani ambayo uliyafanya kabla ya kuokoka hautayasahau?
BW:
Aisee ni mengi mno, unajua mimi nilikuwa mbabe sana nilishawahi
kuchapwa viboko na sungusungu kule Mwanza kama mara mbili hadhalani
sababu ya utukutu. Kwamfano nilishawahi kumchana mtu na viwembe mgongoni
mpaka mgongo ukatapakaa damu, nimecheza sana kamali, kunasiku
nilikamatwa na watu wa usalama usiku saa tisa natembea kwa vile mavazi
yangu yalikuwa yanaonesha ni mwanaume walinipiga sana maana nilivaa pia
kofia. Wamekuja kunifunua baadae ndio wanajua alaa kumbe ni binti!!
RM: Ulishawahi kuvuta Bangi??
BW: Hapana mimi nilikuwa mlevi sana.
RM: Kwaneno moja unaweza kutuambia YESU ni nani kwako?
BW: YESU NI KILA KITU.
RM: Kwanini ni kila kitu?
BW:
Kwasabau Beatrice aliyeshindwa kubadilishwa na mtu yeyote hata Sungu
sungu walishindwa mpaka nikawa sieleweki kama ni mwanaume au mwanamke
sasa watu wananielewa ni jinsia gani Yesu ameweza kunibadilisha kwahio
ni KILA KITU.
RM:Kwanini uliokoka?
BW: Ilitokea tu, ilikuwa tar
16/03/2012 ndipo niliokoka. Kabla ya kuokoka nilikuwa nimekaa miaka
kama kumi na sita(16) bila kusali popote. Siku hiyo nilikosa amani sana
nikawa natafuta msaada kutoka kwa Mtumishi (Mchungaji) yeyote
aniombee niokoke basi ndio nikafanikiwa kupata namba ya Mama(Mchungaji
Rwakatale)akaniombea.

RM: Kunautofauti gani kabla na baada ya kuokoka?
BW: Utofauti upo ikiwemo sasa naeleweka mimi ni jinsia gani, nirahisi hata kuelekeza kuwa yule ni mwanamke.
RM: Unafanya huduma gani kanisani nje ya uimbaji?
BW: Huwa nahubiri kidogo kabla ya kuimba.

Beatrice Akimuombea mtoto aliyekuwa na mapepo(Mchunguze vizuri huyo mtoto utagundua alikuwa ameanguka chini).
RM: Hausikii kama una Uinjilisti ndani yako?
BW: Hio nikweli huwa
nasikia pia hata watu wananiambia kuhusu hicho naamini muda ukifika
nitafanya kwa sasa nafanya uimbaji kwanza. Pia huwa
naombea na watu
wanafunguliwa namshukuru Mungu.
RM: Album yako inaitwaje?
BW: WEWE SI WAKAWAIDA (Jina la Album)
RM: Kwanini sio wakawaida?
BW: Kwasababu Yesu sio wakawaida.
KAMA UNAHITAJI KUPATA ALBUM YA BEATRICE WILLIAM WASILIANA NAE KWA 0658402366 BEI NI TSH 5000 TU.
MWISHO WA MAHOJIANO.
TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WA BEATRICE WILLIAM MUNGU AMBARIKI
Source. Maisha ya ushindi kwa ushirikiano na www.injiliforever.blogspot.com
Comments