![]() |
Kashumba Basil (K` Basil) |
Bidii
yake kimasomo ilimfikisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UD) ambako
alihitimu shahada ya Jiografia na Mazingira. Akiwa chuoni UD
ndipo alijijengea jina kubwa kupitia muziki wa Duniani(Circular Music).
Watanzania wengi wamefanikiwa kumfahamu vizuri K Basil mara baada ya
kutoa nyimbo yake ya Riziki aaakiwa na Mwanadada Stara Thomas ambaye
naye kwa sasa inaaminika kuwa ameyakabidhi maisha yake kwa Kristo.
![]() |
Stara Thomas naye inaaminika kwa sasa ameokoka |
Pamoja
na mafanikio aliyokuwa nayo kwa kipindi chote hicho, K Basil anasema
maisha yake yalitawaliwa na na taabu nyingi. Pombe ndio ilikuwa rafiki
mkubwa na kiongozi wa K Basil. “Nilijaribu kuacha Pombe lakini
ilishindikana, nilkuwa mlevi kupindukia na mara nyingi nililala Bar
mpaka nikawa kero kwa Rafiki zangu.”
Achilia
mbali ulevi na uzinzi anasema siku moja akiwa amelewa aliwahikupata
ajali mbaya ya gari, na katika aliwahi kutupwa jela mara kadhaa kutokana
na mikasa ya hapa na pale.” Nimepitia misukosuko mingi nay a Ajabu
lakini sasa nimekuwa mtu huru, mwenye amani, upendo na Faraja kutokana na kumtegemea Mungu”
Katika
vurugu zangu zote hizo “siku moja nikasikia Sauti ndani yangu
ikiniambia yanipasa nibadilike, niliamua kumshirikisha dada yangu kile
nilichokiskia toka ndani na nikamwambia kuwa nahitaji kuombewa. Niliamua
kwenda kanisani ambako niliongozwa sala ya toba na huo ukawa mwanzo wa safari yangu mpya ya maisha”
Kwa
sasa ninafanya Kazi ya Mungu kwa Moyo mmoja na ninaendelea na huduma ya
uimbaji, ninamshukuru Mungu kwa mafundisho niliyopata kupitia kwa
Mchungaji wangu Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ maarufu
kwa jina la Ufufuo na Uzima lililoko kawe jijini Dar es salaam.
Basil
anasema baada ya kumrudia Mungu na kusimama imara katika wokovu n
wakati wake mwafaka kuwarudisha kwa kristo watu wengine waliopotea
katika ulimwengu wa anasa na dhambi kama
ilivyokuwa kwake. Hivi sasa amezindua album yake iitwayo “YESU
ANANIPENDA” yenye jumla ya nyimbo kumi zikiwemo Namjua, wakatina bahati,
Wewe ni Baba, Rudisha, Utukuzwe, Moyo, Tunasonga Mbele, Mama na Ahsante
Yesu iliyobeba jina la album.
Tarehe
5/12/2010 Basil alifunga ndoa na Perida Mdegela ambaye wanaishi naye
kwa furaha mpaka hivi leo. Anasema anamshukuru Mungu kwa kuwa kwa sasa
akili imetulia. Aidha Basil alipoulizwa anazungumzia vipi wokovu wa
Mwanamuziki Stara Thomas Basil anasema “Kwa hakika hizi ni Habari Njema
ingawa sijui ni nini kilichomuongoza, nafikiri kuungana naye tena
kufanya nyimbo ya Injili”.
![]() |
Basil akiwa na mkewe Pelida Mdegela |
MUNGU ambariki sana mtumishi huyu ambaye anaifanya kazi yake ya uhubiri wa injili.
Basil ni moja kati ya vitendea
kazi katika ufalme wa Mungu kwa ajili ya Kuujenga na Kuuimarisha Mwili
wa Kristo hapa Tanzania na duniani kwa ujuma.
Comments