Je, utamshindaje shetani?


Shetani na malaika zake yaani mapepo, ni viumbe wa kiroho, ambao hufanya kazi zao kwa kutumia kanuni/fomula ya kiroho. Na daima, ulimwengu wa roho una nguvu kuliko ulimwengu wa mwili. Na hapo ndipo swali letu linaposimama, mwanadamu anaweza vipi kumshinda shetani?

Kabla ya kujibu swali hilo, ni vizuri kwanza tujue kua, maisha ya mwanadamu yamegawanyika katika namna mbili, ambazo ni:-

Namna ya kwanza, ni mfumo bayana, huu ni ule unaoonekana kwa macho ya kawaida, yaani mfumo wa mwili, jinsi na umbo lake. Kwamaneno mengine, ni kuwa Mungu aliuumba mfumo huo katika namna ya kuonekana kama alivyowaumba wanyama wengine (Mwanzo 1:20-25). Mfumo huu, ulitokana na udogo, na mwisho wake ni katika udongo. “uvumbini ulitoka, nawe utarudi uvumbini kwa maana u-mavumbi” huu ni uthibitisho kuwa, sehemu hii ya maisha ya mwanadamu, si ya ki-Mungu, bali ni ya kimwili, na huongozwa na “moyo”. Sehemu hii ya maisha ya mwanadamu, imetawaliwa na tabia ya asili, ambayo daima hupingana na mambo ya ki Mungu; “Basi mwanadamu wa tabia ya asili, hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake, hayo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa maana hayatambulikani kwa jinsi ya rohoni”(1Wakorintho2:14) sehemu hii ya maisha ya mwanadamu, haiwezi kumshinda shetani, kwa kuwa hutawaliwa na maisha yaliyo nje ya mfumo wa ki-Mungu. Maisha haya, yamejaa anasa, tamaa, kutoridhika, wivu, ugomvi, ulafi, husuda,hayaogopi dhambi, na hujitawala yenyewe. Maisha haya, hupingana na mwongozo wa maisha aliotoa Mungu kwakuwa si mali ya Mungu. “Yeye aliye wa Mungu,huyasikia maneno ya Mungu; hivyo, ninyi hamsikii kwasababu ninyi si wa Mungu” (Yohana 8:4). Hii ina maana kuwa, kwa kuishi katika mfumo huo, basi hujitenga na Mungu, na kujiunga katika ulimwengu wa waasi, kama alivyoasi Shetani, kwa kukataa kukaa chini ya mwongozo wa Mungu; na hatimaye akaondolewa katika ufalme wa Mungu na kutupwa chini, huku akingojea adhabu yake ya milele katika ziwa liwakalo moto na kwa kiberiti. (Ufunuo 19:20&21) na wote walaomwamini na kumfuata, watakaa katika adahabu pamoja naye. Kwa kuwa mfumo huu wa maisha, unapingana na mfumo wa Ki-Mungu, basi unakubaliana na mfumo wa ki-shetani, hivyo, mfumo huu, moja kwa moja, hauwezi kushinda dhambi hata siku moja.

Namna ya pili, ni mfumo wa kiroho; huu ni mfumo wa maisha ambao una nguvu sana. Mfumo huu,hauwezi kushindana na mfumo wa mwili, daima mfumo huu hushinda kwa kuwa mfumo wa kiroho una nguvu zaidi kuushinda mfumo wa mwili. Mfumo huu kadaharika, umegawanyika katika sehemu mbili, zinazokinzana daima, “ kwamaana, kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka , juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Efeso 6:12). Hii inadhirisha kuwa, maisha ya kiroho, yako katika namna mbili, zinazokinzana, amabo ni mfumo wa “Kiroho wa Mungu”, na “mfumo wa kiroho wa shetani”.Mifumo yote hii, hutumia fomula ya kiroho katika maisha ya mwanadamu, ila athari zake, huweza kudhihirika katika mfumo wa kimwili.

Utendaji kazi wa mfumo wa kiroho wa shetani.
Shetani hutumia mawakala wake katika kutimiza kazi zake. Moja ya mawakala wake wakuu ni wachawi. Ifahamike kuwa, biblia inawatambua wachawi, na hata imewaongelea kuwa ni watu wanaotumia nguvu za kiroho, ambazo zimetokana na baba wa uongo yaani ibilisi.

Wachawi kama mapepo mengine kama majini, mizimu n.k., hutumia mfumo wa kiroho, kumwangamiza mtu kimwili. Pia, wanauwezo wa kumfuta mtu katika mfumo wa maisha ya kimwili na kumpeleka katika mfumo mwingine wa kiroho kupitia viini macho au mazingara na kuwaaminisha watu kuwa amekufa. Hutumia mfumo wa kiroho kumwangamiza mtu kimwili. Ndiyo maana, mchawi anaweza kumloga mtu kwakutumia mfumo wa kiroho, ila akamuua katika mfumo wa kimwili. Hii inamaana kuwa, anamwekea ugonjwa, ili apate namna ya kumhamisha katika mfumo huo anaouaka. Ukweli ni kuwa yule mtu hafi kamwe, ila maisha yake, huhamishwa kutoka katika mfumo wa kimwili, (mfumo unaoonekana) na kupeelekwa katima mfumo wa kiroho, (yaani mfumo usioonekana). Wachawi, wanauwezo wa kumwingilia mtu yeyote asiye na Kristo ndani yake, na kufanya kitu chochote wanachotaka, iwe kumtumikisha, kumlisha vyakula, kuzini nae, kumnywesha pombe n.k. na kupitia mbinu hii, mtu anaweza kuhisi anaota ndoto au njozi, kumbe ni halisi yale anayoyaota. Aghalabu, watu wengi wanaouwawa na wachawi, huota ndoto kabla ya vifo vyao. Ndoto hizi,huambatana na vitisho,huondoa amani, huogofya na hu katikamwacha mtu katika hali ya taharuki . Ndoto hizi huchosha mwili na akili. (Ayubu 7 :14) Biblia inasema “ndipo unitishapo kwa ndoto,na kunitia hofu kwa maono”

Pamoja na kuwa Mungu hutoa ndoto, lakini ndoto hizi hazitoki kwake kwa kuwa kamwe hawezi kutupa ndoto za namna hii (2Timotheo 1 :7) “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”
Swali ya kujiuliza. “Ni kwa jinsi gani wachawi hupigana na wanadamu hususani kwenye ndoto na tunawezaje kuwashinda”

Iyeke Nathan Uzorma-aliyekuwa mchawi mkuu Nigeria anatoa majubu yafuatayo;-
“Karibu kila mtu aliyeuwawa na nguvu za uchawi, kwa namna moja au nyingine aliota kitu cha namna hiyo, siku moja,mbili au tatu kabla ya kifo hicho. Ndoto hizo, ni pamoja na kuota unapigwa risasi na adui unaemfahamu au usiyemfahamu. Kuota unafukuzwa na kichaa au vichaa wengi pia, huashiria mashambulizi ya kifo kutoka kwa wachawi. Vichaa hao, ni roho zinazotumwa na kiongozi wao ambaye ni mwanadamu. Vichaa hao watakuwa wanakukimbiza, na endapo watafanikiwa kukukamata, ujuwe wamekumaliza, hivyo njia pekee ya kujinasua, ni kusali na kujiwekea ulinzi wa damu ya Yesu. Tofauti na hapo, watakuwa wamekumaliza”
Kutokana na maelezo hayo, mwanadamu wa kawaida, hawezi kushindana na mchawi, ni mpaka awe na uwezo wa juu zaidi yaani, awe na Yesu Kristo, ndipo anaweza kumshinda shetani na mawakala wake. Mkumbuke Ayubu, alivyojaribiwa katika mwili wake, hata asimuweze shetani, ila kwa kupitia imani yake aliyokuwa nayo kwa Mungu,basi alimshinda katika roho.
Pia, shetani hutumia uwezo wake wa kiroho, kuharibu mali za mtu kama vile mifugo, kazi, wizi, ajali n.k. hutumia laana, mikosi na hasara katika kazi za wanadamu. Njia hizi za kiroho huweza kumkatisha tamaa, na hata mtu kumvunja moyo kabisa.

Pia, kupitia shetani hutumia, roho za mababu, maagano ya kipepo,laana na viapo(nadhiri) vilivyowekwa na mababu, katika kudhoofisha watu. Huharibu mimba nyingi kupitia njia hii, ajali na kurithisha dhambi za aina flani. Mfano, katika ardhi iliyowekewa maagano ya kimasikini, basi kila mkazi wa eneo hilo, hatafanikiwa. Hii ni kwa kuwa anakaa kwenye ardhi iliyokon kwenye mkataba flani, pengine ni sharti itolewe sadaka(kafara) flani, ndipo mafanikio yaje. Katika mazingira haya, unapaswa kujua kuwa, eneo hilo, haliko katika ulimwengu wa mwili, bali liko katika ulimwengu wa roho. Kinachotakiwa ni kulikomboa, wala si kuweka mbolea kwenye mashamba na kuendelea kulima.

Je, hujawahi kuona watu wamelima pamoja, ila mmoja navuna sana mwingine havuni kabisa? Pengine ndege wanavamia, wanyama wa mwitu wanaharibu shamba lote n.k.? au pengine mazao hayapambi kabisa? Hii ni kuwa, amewekeza kimwili,katika eneo linalotawaliwa kiroho, hivyo, lazima nguvu ya roho itashinda tu,kwa kuwa mwili siku zote ni dhaifu.
Nguvu za kimila, desturi na tamaduni, ni njia nyingine ambayo, hutumiwa sana na ibilisi, katika kutekeleza shughuli zake. Mbinu hii,humfunga mtu na mfumo wa kiroho, ambao yeye haujui bali hujikuta analazimika kuuishi. Mfumo huu, humtenga mtu na Mungu, hata kabla ya kuzaliwa, na hudhihirika mara anapojitambua.

Silaha Nyingine ya shetani ni ulevi ambapo maisha ya mtu hufichwa katika nguvu ya kiroho ya ulevi, uwe wa pombe au sigara, n.k. ndiyo maana unakuta mtu anataka kumfuata Mungu lakini anakwambia, siwezi kuacha sigara japo pombe nimeacha, inamaana maisha yake yamefichwa katika ulimwengu wa roho wa ulevi. Utankuta mtu huyu, anasali, hata anahudumu, lakini jua kabisa maisha yake yako rehani kwa Ulevi. Wengine wamefichwa kwenye uzinzi,wizi, matusi, ugomvi n.k.

Pamoja na silaha nyingine anazotumia shetani katika kumwangamiza mtu, ikiwemo uvivu,kulala fofofoo, kujilegeza/kudeka,kushiba sana, kupuuza ibada na maombi njia ya kujisahau kupitia tendo la ndoa na mahaba ya kikahaba....."uatilia sehemu inayofata" Zaidi ya hapo, tutajifunza upande wa pili wa maisha ya kiroho katika Kristo, ambaye ndiye tabibu wa kweli.

Lakini sitakuacha hivi hivi, ni vizuri walau nikudokeze mbinu ya Waganga wa kienyeji wanayotumia kuwatibu wagonjwa....."Kwanza kabisa, pepo hawezi kumtoa pepo mwingine, kinachofanyika hapa ni kutunishiana misuli na kushindana, mganga anachofanya ni kumteau pepo mmoja na kumfanya kiranja wa mapepo mengine na hapo humopa maelekezo kuwa wasimsumbue mtu huyo kwa kipindi flani" ila baada hali hubadirika na kuwa mbaya zaidi.

Dawa ni kuja kwa YESU KRISTO ndipo kuna pumziko la Kweli

Comments