JE,MKRISTO (ALIYEOKOKA) NI VYEMA KUOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYEOKOKA (ASIYE MKRISTO)?

Utangulizi:Katika kujibu swali hili, itabidi kwanza tujifunze mambo yanayojitokeza katika swali: 
1) Mkristo ni nani

2) Asiye Mkristo ni nani

3) Ndoa ya Kikristo ikoje.

 1) Mkristo ni: a: Mtu aliyekubali kumpokea Yesu Kristo na kuamini kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yake; na mtu huyu ndiye anayepewa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu (Yn.1:12). b: Mfuasi/Mwanafunzi/Mtu wa Kristo ( ndivyo wenyeji wa Antiokia walivyowaita-Mdo.11:26) au ni mtu aliyezaliwa mara ya pili (aliyeokoka). c: Kiungo (Efe.4:25) katika mwili wa Kristo (sehemu ya Kanisa). d: Hekalu la Mungu ambalo Roho Mtakatifu anakaa ndani yake (1Kor.3:16; 6:16; 2Kor.6:16). 

2) Asiye Mkristo ni kinyume cha Mkristo, yaani:a: Mtu anayekataa kumpokea Yesu Kristo na kutoamini kuwa Yesu ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yake; na mtu huyu ndiye anayetembea katika hukumu ya adhabu (Mk.16:16; Rum.8:1). b: Mtu ambaye si mfuasi wa Kristo au ambaye hajazaliwa mara ya pili. c: Mtu ambaye si kiungo katika mwili wa Kristo ( si sehemu ya Kanisa). d: Mtu ambaye si hekalu la Mungu, hivyo Roho Mtakatifu hawezi kukaa ndani yake. 

3) Ndoa ya Kikristo ni:Agano (siyo mkataba) kati ya mume na mke (wa-Kristo) kuishi pamoja maisha yao yote bila kuachana (Mk.10:8,9; Mal. 2:16). Sasa hebu tujifunze zaidi juu ya jambo hili kwa kutafakari maandiko yafuatayo:a: Zab.133:1; inasomeka “ Tazama,jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu (walioamini/wanandoa) wakae PAMOJA, kwa UMOJA”. Maana yake hapa, nikwamba walioamini/wanandoa wanatakiwa kukaa PAMOJA kimwili (kufanya mambo kwa pamoja) na kwa UMOJA wa Roho (Efe.4:3; Mw.2:18). Umoja wa Roho ndio unaotufanya tuwe katika Mwili (Kanisa) mmoja, Roho mmoja, Tumaini moja, Bwana (Yesu) mmoja, Imani (Ukristo) moja, Ubatizo (wa maji mengi) mmoja na Mungu (Yehova) mmoja (Efe.4:4-6). Ukurasa 1b: Mw.24:3,4 . Ukisoma maandiko haya utaona kuwa Mzee Ibrahimu alipotaka kumwozesha mtoto wake Isaka alikataa kumtwalia mke katika binti za Wakanaani aliokuwa anakaa kati yao, badala yake alitaka atwaliwe mke kutoka katika nchi yake na kwa jamaa zake. Ebu tukajiulize swali kidogo hapa; hivi, ni kwanini Ibrahimu aliongozwa na Mungu kumchukulia mke mtoto wake kutoka katika nchi yake na kwa jamaa zake badala ya nchi ya Kanaani?Jibu:i: Kwakuwa Ibrahimu alikuwa ni Mwebrania (Mw.14:13), alitaka mtoto wake apate mke kutoka kwa waebrania badala ya kuchukua mke kutoka kwenye makabila mengine. (Kwa sasa tungesema “Kwakuwa mtu amekuwa Mkristo, anatakiwa mtoto wake apate mke/mume kutoka kwa Wakristo badala ya kuchukua mke/mume kutoka kwenye imani zingine”).ii: Kwakuwa Mungu alikuwa amefanya AGANO la milele na Ibrahimu (agano jipya na wanaoamini kwa sasa) na uzao wake (Mw.17:1-8), na wala hakufanya Agano na mataifa mengine (wasioamini kwa sasa), na kwa kuwa mataifa hayo yalikuwa yanaabudu miungu/masanamu; hivyo mzee Ibrahimu aliona kumchukua mke nje ya Agano kwaajili ya mtoto (Isaka) wake ni kuchafua Agano lake na Mungu.iii: Kwakuwa Wakanaani walikuwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu (wasiookoka kwa sasa), walikuwa chini ya laana (hukumu kwa sasa=Mk 16:16); na kwasababu hiyo mzee Ibrahimu aliona kumchukua mke kutoka kwa watu walio chini ya laana ni kukaribisha LAANA katika jamii ya WAEBRANIA (wa-Kristo kwa sasa).c: Kut.34:12-16. Ukisoma maandiko haya utaona kuwa Mungu anamuasa Musa kwamba asifanye Agano na wenyeji wanchi ya Kanaani ili watu wa Mungu (wana wa Izraeli) wasije wakafanya UZINZI na miungu yao, pia WASIWAOZE WANA (wavulana) WAO BINTI ZAO, NAO BINTI ZAO ili wasije wakashiriki kufanya UZINZI na miungu yao. d: 2Kor.6:14-16. Ukisoma maandiko haya utaona mtume Paulo akiongozwa na Roho anawaasa waumini (Kanisa) wa Korintho kwakusema “ (mlioamini/mliookoka) Msifungiwe nira (msioane) pamoja na wasioamini (wasiookoka), kwajinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya HAKI (wokovu) na UASI (dhambi)? Tena pana shirika gani kati ya NURU (Mkrito) na GIZA (asiye Mkristo)? Tena pana ulinganifu gani kati ya KRISTO na BELIARI (shetani)? Au yeye AAMINIYE (aliyeokoka) ana sehemu gani pamoja na yeye ASIYEAMINI? Tena pana mapatano gani kati ya HEKALU (Mkristo) la Mungu na SANAMU? Kwa maana sisi (Kanisa) tu hekalu la Mungu aliye hai; …” HITIMISHO Mtu wa Mungu; nakusihi katika jina la Yesu; usije kuingia kwenye jaribu la kumtafuta mwenzi wako wa maisha nje ya Waebrania, Agano lako na Mungu katika Yesu Kristo, Mwili wa Kristo (Kanisani); vinginevyo utajuta na utajikuta unaingia kwenye jaribu jingine la kutafuta ufunguo wako mwenyewe wa kuacha/kutoa talaka ambavyo hairuhusiwi ki-Biblia (Mal 2:16;Mt 19:6;Mk 10:9); au utajikuta unaubeba msalaba wako katika maisha yako yote ya ndoa; na ukifanya mchezo unaweza kujikuta unauacha wokovu.Ukurasa 2Tambua ya kwamba ili kumpata mwenzi wako wa maisha huitaji kwenda kwa msisimko au tamaa ya mwili bali unahitaji kutulia mbele za Mungu ili upate uongozi wa Roho Mtakatifu katika kumpata aliye wakufanana nawe (mwili mmoja, Roho mmoja, Tumaini moja, Bwana mmoja, Imani moja, Ubatizo mmoja na Mungu mmoja -Efe.4:4-6); basi wote mkiwa na mambo hayo saba ktk ndoa yenu, huko ndiko kufanana Mungu alikokukusudia na wala siyo kufanana kwa jinsi ya mwili wa nyama, kwa jinsi hiyo hatimaye wote mtanyakuliwa pamoja na kuishi ktk uzima wa milele kwa pamoja.Ninachoweza kukuhakishia na kukutia moyo ni kwamba, utambue ya kwamba KILA MTU ANAYE WAKWAKE WA KUFANANA NAYE; kama Adamu alikaa miaka mingi katika bustani ya edeni bila kudhihirishiwa mke wake Eva, na hatimaye akadhihirishiwa, basi na wewe usiwe na hofu hata kama unaona miaka imepita. Na ikitokea hukupata neema ya kumpata wakufanana naye, basi muombe Mungu ili ufanane na Yesu hatimaye uishi naye milele kuanzia duniani duniani na hata mbinguni.Mungu akubariki sanaaaaaaaaaaaaaaaaa.


Mwl.Majidu Kalokola
Mob: 0713227861; 0767227861
Email: majidukalokola@yahoo.com

Comments