KKUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA
UZIMA-MOSHI
Na Mchungaji Kiongozi: JOSEPHAT GWAJIMA
Matatizo
haya yanaweza kuwa ya ndoa,ama ya kifamilia,ama ni matatizo ya kimaisha ama ni
ya kibiashara.
Matatizo mengi katika maisha yanaondoka kwa;
- Kuombewa
- Kusoma neno.
Lakini
kuna namna moja ya kumaliza matatizo yote,ambayo hii ndiyo nataka nishirikiane
na wewe,na wewe ukiishika utashangaa sana,hebu tuiangalie namna hiyo kwenye maandiko matakatifu.
Kutoka 23:25
“Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye
atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako”.
Faida za
kumtumikia Mungu.
- Mungu atabarikia chakula chako.
- Mungu atabariki maji yako.
- Mungu anakuondolea ugonjwa kati yako
- Hapatakuwa na mtu mwenye kuharibu mimba.Maana ya kuharibu mimba ni kwamba kila kitu unachokianza kinaharibika kabla hujakimaliza
- Hapatakuwa na aliye tasa.
- Atawafadhaisha wote watakaokufikiria. Kila mtu atakayefanya vita na wewe atafadhaisha na ataachana na wewe
- Hesabu ya siku zako ataitimiza
Kutoka 23:26 “Hapatakuwa na
mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza”.
- Bwana Mungu atatuma utisho wake utangulie mbele yako.
- Bwana atawafanya hao adui zako wakuoneshe maungo yao.
Kutoka.23:27
“Nitatuma utisho wangu utangulie mbele
yako, nami nitawafadhaisha watu wote
utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao”.
Utamtumikiaje
Bwana Mungu.?
Watu wengine wanafikiri ili kumtumikia Mungu lazima uwe huna au
uache kazi yako,Haiko hivyo maana kuna Watu ambao walimtumikia Bwana huku wakifanya
kazi zao kama kawaida, tuwaone wachache kutoka kwenye Biblia;
1.DANIEL.
-Alikuwa
makamu wa watu wa Raisi.
Danieli
5:29 “Ndipo Belshaza akatoa
amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa
dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni
mtu wa tatu katika ufalme”.
-Mbunge wa jimbo la Babeli.
Danieli.2:48
“Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya
kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote
wenye hekima wa Babeli”.
-Waziri mkuu.
Danieli
6:1-3
“1.Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme
maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;
2 na juu
yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa
watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
3 Basi
Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora
ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote”.
2.LUKA,amabaye
alikuwa Daktari.
Wakolosai 4:14 “Luka, yule tabibu
mpendwa, na Dema, wanawasalimu”.
3.MTUME PAULO.
-Alikuwa mshona mahema
Mdo 18:1-4 “1.Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika
Korintho.
2
Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka
nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio
amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao;
3 na kwa
kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa
maana walikuwa mafundi wa kushona hema.
4 Akatoa
hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu
kuwavuta Wayahudi na Wayunani”
4.LIDIA.
-Alikuwa akiuza rangi ya zambarau.
Mdo.16:13-15 “13.Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda
kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi,
tukasema na wanawake waliokutana pale.
14
Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa
Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana,
ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.
15 Hata
alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake,
akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani
mwangu mkakae. Akatushurutisha.”.
5.MAWAKILI WALIOMTUMIKIA BWANA.
Luka 8:1-4 “1.Ikawa baada ya
hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza
habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2
na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa
wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3
na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa
wakimhudumia kwa mali zao.
4 Mkutano
mkuu ulipokutanika, na wale waliotoka kila mji wakimjia, alisema kwa mfano”
Comments