KIBALI HUPATIKANAJE ?

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla

* Je kwa kumuomba Mungu.?
*Je kwa kufunga sana?

jibu lipo katika Mwanzo 4:7
Inasema;
'' Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. ''

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...

Anasema '' kama ukitenda vyema,hutapata kibali?''
Kumbe Kibali huja kwa kutenda vyema/mema.
Yeye atendaye mema haitajiki kuomba kibali,bali kibali huja.

Anasema tena;'' Usipotenda vyema dhambi iko,''
Kumbe yeye atendaye uovu,ipo dhambi kwa ajili yake.
Dhambi hii ipo tu,yaani ni kama vile imejiaandaa kumvamia pale atendapo uovu tu.

Anasema tena ;''dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. ''
Sasa sikia;
Dahambi ya Kaini ilikuwa imemuotea mlangoni.
Hata pale alipokuwa yeye mwenyewe Kaini amekufa,lakini bado dhambi ilikuwapo MLANGONI.

Na ndio maana utaona dhambi ile ya Kaini ikaja kuendelea hata katika vizazi vitano baadaye (Mwanzo 4 :17-18)
Oooh!
Kumbe,
Nimegundua kitu.

Kumbe yatupasa kuishinda dhambi iliyotuotea mlangoni ili isije ikaendelea kizazi hata kizazi.
Tutaishinda kwa njia moja tu,
Kwanza kujisalimisha kwake Yesu Kristo,kwa kufanya ibada ya utakaso kwa kuvunja maagano yote ambayo yamesimama kwa uwepo wa dhambi.

UBARIKIWE.

Comments