![]() |
Na Mch. Josephat Gwajima |
Waefeso 3:11
“…Kwa
kadri la kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu…” Inatufundisha
hapa kwamba kila mtu alie hai ana kusudi la milele limeandikishwa ndani ya moyo
(maelekezo yako ndani ya moyo yameandikishwa ili utakapo kuwa mkubwa, ndio
yanatengeneza uwewe na mambo kadha wa kadha), hatma ya maisha yako inauhusiano
mkubwa sana na moyo wako.
Nini maana ya moyo?
Kazi
ya moyo ni kupeleka minerals (madini), ndani ya mwili kupump (kusukuma) oksijeni,
mwili mzima na kusukuma uchafu nje ya mwili. Mara moyo wa mtu utakapo acha
kufanya kazi mtu anakufa hapo hapo, sababu moyo ndiyo centre inayofanya mtu
aishi.
Kuna
utu wa ndani ya mtu ambao ni roho, na nje ya mtu ambao ni mwili, na mtu wa
ndani (ambaye ni roho) naye ana moyo pia, ndio maana Mungu ni Roho lakini ana
moyo Mwanzo 8:21 “Bwana akasikia harufu ya kumridhisha;
Bwana akasema moyoni sitailaani nchi tena”.
Mwanzo 17:17 “Ibrahimu akaanguka
kifudifudi akacheka, akasema moyoni…” Mwanzo 18:12 “Sara Moyo wake ukacheka
Mwanzo 24:45.
Mungu
anapotaka kupanda kusudi la maisha ndani ya mtu hupanda moyoni, ndio maana moyo
wa mtu ukiwa mzito mambo yake hayawezi kufanikiwa, atakuwa anaona uzito katika
kila jambo analolifanya.
Mwanzo 27:41, “…Esau akasema
moyoni mwake...” Kutoka 4:14 “… naye
atakapokuona atafurahi moyoni mwake…”
Kumbukumbu la torati 2:30 “..akamtia
ukaidi moyoni mwake..” tunajifunza unapotiwa ukaidi moyoni mwako, ukaidi huo
unajidhihilisha mwilini, unakuta mtu hupendi kuwa mkaidi, lakini ndio unakuwa
ushatiwa ukaidi. Ndio maana mtu utamsikia anasema nakupenda kutoka moyoni
mwangu, hapo cha kujiuliza je huo moyo anaouzungumzia ni wa kwake, maana watu
hutiwa mioyo tofauti na kusudi la Bwana.
Mithali 4:23 “..linda sana moyo
wako kuliko vyote ulindavyo maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima..” Biblia
ya kiingereza inasema “Keep thy heart with all diligence; for out of it are the
issues of life” Tunajifunza hapa mambo yote za maisha ya mtu huanzia moyoni,
matatizo yanayowakumba watu au mafanikio ya mtu huanzia moyoni mwa mtu, “ISSUES
OF LIFE”
Kutoka 35:35 “…Amewajaza watu hao
akili za moyoni ili atumike katika kazi ya kila aina...”
kutoka 35:34 “…nimemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha..”
Siku
hii ya leo, ninaomba Mungu apande jambo moyoni mwako, ili kutimiza kusudi la nchi
yetu Tanzania. “Utamkuta mtu mwingine anatenda jambo kwa ufanisi ulio wa juu
mpaka watu wanashangaa wanamuuliza hivi ulisoma wapi, kumbe hata hajasoma
lakini ndio kusudi la moyo wake.
Mungu
amepanda kitu ndani ya moyo wako ili kupitia kile uwe na mafanikio, shule
haiwezi kukuletea mafanikio, kile kilichopandwa ndani ya moyo wa mtu ndio mafanikio
yake. Ufufuo na Uzima imepandwa ndani
ya moyo wa Yesu, ndio maana hatuhitaji mtu atuelekeze njia ya namna ya
kwenenda.
Kumbukumbu 4:9 “..mambo
uliyoyaona yakaondoka moyoni mwako…”, Kumbukumbu 8:2 “…kuyajua yaliyo moyoni
mwako…” Hata Mungu kuwapitisha wana wa Israel jangwani ni ili Mungu ajue yaliyo
mioyoni mwao, kama watashika amri zake ama sivyo.
“Issues
za maisha zipo mioyoni mwa mtu” Nataka nianze biashara, nataka nisome shule,
nataka niache kazi vyote hivyo huanzia moyoni. Moyoni mwangu nikimtumikia Mungu
najisikia vizuri, nikimuimbia Mungu njisikia vizuri, nikimtolea Bwana moyoni
mwangu najisikia vizuri sana, ndio maana mtu anasema nasema kutoka moyoni
Mwangu. Na ukisimamia kusudi hilo utafika pale Mungu alipokukusudia.
Shetani
ana tabia ya kuiba mioyo ya watu yenye kusudi la Mungu, anaandikia maelekezo
yake yeye ambayo ni tofauti na maelekezo ya Mungu, anakutole kusudi la Mungu anaandika
maelekezo yake ili uelekee upotevuni, utasikia najisikia nikaibe kabisa,
najisikia niwe mwana mziki, najisikia nivute bangi, napenda ukahaba, kumbe ndio
maelekezo yaliyonakiriwa na shetani ndani ya moyo wako.
Unakuta
mtu alivyokuwa mtoto mdogo, alikuwa anampenda Mungu, anasema nataka nimtumikie
Mungu, niwe mchungaji, niwe mwimbaji, lakini mtu huyo akishakuwa mtu mzima anakuwa
tofauti kabisa “ukiona upo hivyo ujue umebadilishiwa moyo”.
Unakuta
mtu ameokoka anaolewa na mganga wa kienyeji, mnamuuliza mnamwambia unawaza nini
wewe anakwambia Mchungaji nampenda toka moyoni mwangu, nampenda huyu kaka toka
moyoni, ukiangalia kaka mwenyewe ni mvuta bangi, hata haeleweki. Kumbe moyo
wako uliibiwa na shetani na huyo kaka mvuta bangi akaandikishwa ndani ya moyo
wako, bila wewe kujua.
Mtu
umeokoka lakini unakuta unampenda binti/kaka wa kiislamu, kumbe umebadilishiwa
moyo, wamenakiri kwenye moyo wako kuwa utaolewa ana kuoa muislam. Leo tunarudisha
mioyo yote uliyobadilishiwa, lazima kusudi la Bwana litimie, kusudi la Bwana
ulilowekewa ndani ya moyo wako tunalirudisha leo kwa jina la Yesu. “Daudi
alisema eeh moyo wangu na vyote vilivyo ndani yangu mche Bwana”.
Shetani
anajua issues zako zote za maisha yako zinatokea moyoni, kiu yako ya kuimba,
kuhudhulia ibadani, kutoa fungu la kumi, kumtumikia Bwana vyote huanzia moyoni.
Shetani ili abadilishe kusudi lako anaiba moyo, anabadilisha kusudi lililonakiriwa
na Mungu moyoni mwako, anaweka maelekezo yake, unajikuta uliyokuwa unatenda
hutendi tena, unaingiwa na kiu ya kutenda mambo mengine ambayo hujawahi hata
kuyawaza. Lakini wewe ukikaa unaona upo sahihi sababu unachokifanya kinatoka
moyoni, kumbe umebadilishiwa moyo ili uelekee upotevuni.
Kuna
watu huwa wanajuta baada ya kutenda jambo, usiangalie kwamba hili jmbo linatoka
moyoni mwangu, cha kufahamu ujue huo moyo ni wa kwako, unayoyatenda ni kusudi
la Bwana tangu awali? Huu ni wakati wa kukana maelekezo ya moyoni mwako kama
sio kusudi la Mungu. Shetani amepanda jambo ndani ya moyo wako umeanza
kulitumikia, kumbe ni kusudi lililopandwa na shetani.
Shetani
akitaka kukuandikia maelekezo yake, huwa lazima usumbufu utokee, ulikuwa
unajiweza vizuri kifedha, ghafla unakosa hela ya kula, hata hela ya kwenda
kanisani huna, kazi unafukuzwa kumbe ni shetani anakuandaa kukuchomoa kwenye
lile kusudi la Mungu, ukishaona umechoka hueleweki shetani anakuambia hilo sio
kusudi lako, anakubadilishia maelekezo yaliyondani mwako “mara unaalikwa kwenye
semina ya “empowerment”, kumbe shetani ndio anakuwa anakutengeneza kwenye
kusudi lake.
Leo
ninamlazimisha shetani na watenda kazi wake wote kurudisha mioyo yenu ya asili
irudi kwenu, na moyo wako unarudi kwa jina la Yesu. Unarudi kwenye kusudi lako
la milele.
Namna ya kuomba
Ngo’a
maelekezo ya kishetani yaliyopandwa ndani ya moyo wako ili yakuongoze kwenda
mbali na kusudi lako la milele, nayaondoa maelekezo hayo kwa jina la Yesu.
Ninakataa maelekezo yaliyowekwa ndani ya moyo wangu kugeuza kusudi la Mungu
ndani yangu, kama niliandikiwa kuwa muombaji narudisha kusudi hilo kwangu kwa
jina la Yesu, ninakataa kiu ya miziki ya kizazi kipya ndani yangu, kiu ya
uzinzi, kiu zote za kishetani kunipindisha na kusudi langu la milele nakataa
kwa jina la Yesu.
Leo
namng’ang’aniza shetani na malaika zake na majini yake na vibwengo vyake
warudishe moyo wako kwa jina la Yesu. Maelekezo ya kishetani yalioandikishwa
ndani ya moyo wangu ili kunipeleka mbali na Mungu nayakataa kwa Jina la Yesu,
maelekezo yaliyonipeleka mbali na baraka zangu naukataa moyo wenye maelekezo
hayo kwa jina la Yesu, anza kudai moyo wako, moyo wa kumcha Bwana, moyo wa
ubunifu, moyo wa mafanikio, moyo wa safari nautaka moyo wangu kwa jina la Yesu.
Moyo
wa kiburi mlioniwekea naukataa kwa jina la Yesu, moyo wa mauti mlioniwekea
naukataa kwa jina la yesu, nautaka moyo wangu kwa jina la Yesu. Nataka moyo
wangu, moyo wa ushindi, moyo wa kushika fedha, moyo wenye msimamo, moyo unaompenda
Yesu, naurudisha moyo wangu katika jina la Yesu Kristo.
Comments