KUZIJUA NA KUWEZA KUZIINGA HILA ZA SHETANI (sehemu ya pili)

Mwl Nickson Mabena akifundisha, na hapo ni mruvango, wilayan siha mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro


Waefeso 6:11

"Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kuweza kuzipinga hila za shetani"

Ninamshukuru Mungu kwa neema yake hata amenipatia nafasi nyingine ili niweze kumalizia ujumbe huu, ni furaha yangu kuona kanisa la Mungu linasonga mbele, namshukuru sana Mungu kwa kuniokoa na kunifanya niwe mtumishi wake!!
Sifa na Utukufu Kwa MUNGU.

Hebu tuendelee na somo;

Kwa kutozijua hila za shetani wengine wameangukia katika roho zidanganyazo, hata wakafikiri wapo mahali salama, kwa utamu wa maneno ya wahubiri pasipo kuangalia kama ni neno la kweli la Mungu au ni usanii tu, wamejikuta wapo shimoni na hawajui watokeje!!
Wengine wanaabudu mizimu bila ya kujijua, ndugu yangu kumbuka Yesu alisema "Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake" Yoh 8:44b

Ndani ya mtumishi wa shetani hamna kweli, hata akiwa na maneno matamu kiasi gani ujue anatafuta namna ya kukuua tu.
Napenda sana watu waangalie kile Biblia itufundishacho kuliko kung'ang'ana na kile watu wasemacho....
ona "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu;....." 1Yoh 4:1a
Kwa nini biblia ituambie tuzijaribu!? Kuzijaribu maana yake ni kuzipima!, anhaa kumbe una haki ya kuzipima na wala sio dhambi.

Kanisa halikosi kuzijua HILA za shetani; kwani imeandikwa "Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake" 2Kor 2:11
Fikira za shetani maana yake ni hila za shetani, sasa Shetani atatushindaje? wakati hila zake hatukosi kuzijua!?. Paulo anasema shetani asije akapata kutushinda, kumbe ana uwezo wa kutushinda tusipozijua hila zake. Shetani yupo kazini, omba sana Mungu upate kuzijua hila zake!!

LAKINI HAITOSHI KUZIJUA PEKE YAKE, BALI KUZISHINDA!.

ndivyo mstari unaotuongoza kwenye somo hili unavyosema;
"Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani"
Kuzijua hila ni hatua ya kwanza, na hatua ya pili ni kuzipinga, na siri pekee ya kuweza kuzipinga hila za shetani na KUVAA silaha zote za Mungu, nafikiri nimeshawahi kuandika kuhusu silaha za Mungu kwenye page hii.
Usijaribu kuzipinga hila za shetani kama hujavaa silaha zote za Mungu; kwani hutaweza hata kidogo!!.

Pamoja na hayo yote, ila Yesu bado anaweza! Kujipanga ni haki ya Adui lakini Ushindi ni haki yetu!.

(KAMA UNAHITAJI KUOKOKA, WASILIANA NA MIMI, au kwa huduma za maombi na maombezi).

Maoni na ushauri pia unakaribishwa!

Ubarikiwe sana kwa kusoma ujumbe huu.
 
by Mwl Nickson Mabena
 

Comments